Ada2020, ni mradi unaodhaminiwa na Umoja wa Ulaya kupitia mpango wa kuongeza kasi ya ukuaji wa makampuni madogo na ya kati (SME Instrument)

Ada imeunda maunzi laini (software) ambayo hutoa msaada wa kifikra wa kipekee kwa wataalamu wa matibabu wakati wa mchakato wa utambuzi.

Kiolesura michoro cha mtumiaji (user-interface) cha Ada kilichoshinda tuzo kinatoa taarifa zote muhimu kwa madaktari, na kinawezesha tathmini zao za hali ya mgonjwa kwa ujumla. Kinawezesha daktari kufanya uamuzi wenye vigezo na wenye kuaminika zaidi. Baada ya miaka mitatu ya utafiti wa msingi kwenye teknolojia mpya za kufikiri, sasa Ada ipo tayari kunasa maarifa kutoka kwa wataalamu wa matibabu, kuyageuza kuwa mtambo wa fikra wa matibabu na kuyapeleka moja kwa moja kwenye hatua ya namna fulani maalum ya uhudumiaji wa mgonjwa.

Malengo Yetu

1. Kuepuka Makosa ya Utambuzi wa Ugonjwa

Makosa ya utambuzi wa ugonjwa na vipimo vilivyopitiliza hutokea haswa wakati wa matibabu ya magonjwa makubwa/ hatari, kama vile saratani na magonjwa adimu.

2. Kuorodhesha Mchakato

Utaratibu wa kazi wa kila siku unasaidiwa na chombo chenye maono, akili, na uwezo wa kubaini ugonjwa (kupima).

3. Kusaidia Ufanyaji wa Maamuzi

Madaktari 8 kati ya 10 wana hofu juu ya kushindwa kutambua ugonjwa hatari wa mgonjwa kwasababu ya kutingwa na kazi nyingi.

Faida

_ Kupunguza namba ya makosa ya utambuzi wa magonjwa na matibabu kunaweza kusaidia kupunguza mateso binafsi ya wagonjwa na gharama za huduma za afya kwa wakati mmoja._

Tafiti moja ilibainisha kwamba makosa ya utambuzi na matibabu ya magonjwa ya kizunguzungu yana gharama ya takriban Euro Bilioni 1 kwa mwaka Ujerumani. Kwa mujibu wa tafiti moja ya hivi karibuni (WinterGreen research - 2013) katika uwezeshaji wa maamuzi ya huduma za afya, vipimo vya makosa na vipimo ambavyo havihitajiki kwenye ugonjwa fulani, vinabeba 30% ya gharama za utoaji wa huduma ya afya Marekani. Bidhaa tatu za watumiaji lengwa zitatayarishwa, kushughulikia makundi matatu yafuatayo ya soko: GP-Huduma (GP-Service), Huduma ya Wataalamu (Expert-Service), Huduma ya Kuzuia (Prevention-Service).

Henry Hoffmann Mkuu wa Utafiti
Mkuu wa Utafiti Henry Hoffmann
Mkuu wa Utafiti Henry Hoffmann

Henry anaongoza timu ya utafiti ya Ada. Mzawa huyu wa Berlin anaongoza ustawishaji wa mahesabu ya kikompyuta (algorithm), anaunda mifano ya lugha bandia (modeling languages) na kutengeneza njia mpya za uwakilishi wa maarifa. Henry amehitimu Uhandisi wa Kompyuta katika Chuo cha Ufundi Berlin na mpaka sasa ameshatengeneza teknolojia kadhaa za akili bandia.

Dr. Martin Hirsch Mwanzilishi Mwenza & Mwanasayansi Mkuu
Mwanzilishi Mwenza & Mwanasayansi MkuuDr. Martin Hirsch
Mwanzilishi Mwenza & Mwanasayansi MkuuDr. Martin Hirsch

Martin ana Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Sayansi ya Mishipa ya Fahamu na Diploma ya Fiziolojia (Elimu ya mwili). Ni mtafiti wa tiba aliyegeuka mjasiriamali na kutoka kwenye nadharia hadi uvumbuzi baada ya kuchapisha kazi yake kuhusu miundo ya mishipa kwenye jarida la kisayansi la Nature. Aliunda toleo la kwanza la Ada kwa ajili ya madaktari na leo anaendelea kuboresha namna Ada inavyojifunza. Martin ni mjukuu wa Werner Heisenberg, ambaye ni mshindi mashuhuri wa tuzo ya Nobeli.

Huu mradi umepata udhamini kutoka kwa mpango wa utafiti na uvumbuzi wa Umoja wa Ulaya Horizon 2020 chini ya makubaliano ya ruzuku nambari 674459 ya uongezaji wa kasi ya ukuaji wa makampuni madogo na ya kati (SME Instrument).