Kikaguzi cha COVID-19
Wakati COVID-19 inaendelea kuenea, tunataka kukusaidia wewe na uwapendao kujiandaa na kujilinda kila mmoja. Ikiwa wewe au mtu wa karibu anajihisi mgonjwa, tumia tathmini na kikaguzi chetu cha COVID-19 kukagua dalili na kutambua nini chakufanya baada ya hapo.

Anza tathmini
Jifunze kuhusu COVID-19
Jinsi ya kujilinda wewe na wengine dhidi ya COVID-19
Osha mikono yako kwa angalau sekunde 20.
Jaribu kutogusa macho yako, pua, au mdomo.
Epuka kukaribiana kwa karibu na wengine.
Kaa nyumbani ikiwa una dalili kidogo.
Ziba mdomo unapokohoa au ziba mdomo kwa karatasi ya tishu unapopiga chafya.
Takasa (kwa kemikali) mara kwa mara maeneo yanayoguswa.
Kuhusu tathmini ya COVID-19 ya Ada na kikaguzi
Kikaguzi chetu cha COVID-19 kinaweza kusaidia kupunguza mahitaji yasiyo ya lazima ili wataalamu wako wa tiba waweze kuweka msisitizo wa matunzo yao kwa wale wanaoyahitaji zaidi. Kulingana na miongozo bora ya utendaji duniani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Vituo vya Marekani vya Kudhibiti Magonjwa (CDC), Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza (NHS), na Taasisi ya Robert Koch, kikaguzi chetu kinapatana na mfumo wako na rahisi kukibadilisha ili kuendana na machaguo yako ya utunzaji wa afya. Jifunze namna ya kufanya.
Nyenzo za ziada
Shirika la Afya Duniani (WHO). “Coronavirus disease (COVID-19) advice for the public”
Wizara ya Afya ya Tanzania. “Taarifa kuhusu COVID-19”
Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC). “Coronavirus (COVID-19)”
Kituo cha Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (ECDC). “COVID-19”
Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza (NHS). “Advice for everyone. Coronavirus (COVID-19)”