1. Ada
  2. Editorial
  3. Kampuni & utamaduni
  4. Devugees: kujenga mahusiano mapya kupitia msimbo (code)

Devugees: kujenga mahusiano mapya kupitia msimbo (code)

The Devugees students on their visit to Ada.

Maelfu ya watu wanahamia Berlin kila mwaka, wakivutiwa na historia yake, utamaduni na fursa katika eneo hili la Ujerumani linalokua tech kiteknolojia. Berlin ni nyumbani kwa moja kati ya idadi kubwa ya wahamiaji katika Umoja wa Ulaya, na wengi zaidi wakija Berlin kutafuta hifadhi kutoka kwenye uvunjivu wa haki za binadamu kwenye nchi zao za asili na kuanza maisha mapya.

Kwa kawaida ya mandhari ya ujasiriamali wa Berlin, biashara kadhaa zimekuwa zinashirikiana na serikali kurahisisha mchakato wa mawasiliano baina ya makundi ya wahamiaji na wenyeji kupitia mipango ya uwezeshaji kijamii na kiuchumi.

Mapema juma hili katika ofisi za Ada Berlin Kreuzberg, tulipata fursa ya kuwa wenyeji wa moja kati ya hiyo mipango kupitia taasisi ya kazi za kidijitali (Digital Career Institute), yenye mpango uitwao Devugees. Mpango wa Devugees unaendeshwa na timu ya wajasiriamali, waajiriwa, na wafanyakazi huria (freelancers) ndani ya eneo la biashara changa (startup) Berlin. Mpango huu hutoa ushauri, mafunzo ya usimbaji (coding) na mtandao wa kitaalamu wa mawasiliano kwa wakimbizi ambao wanajaribu kuanza maisha mapya Berlin.

Ikiwa moja ya sehemu ya mpango, wanafunzi hutembelea kampuni za teknolojia ndani ya jiji ili kupata mwangaza wa hali ilivyo kufanya kazi katika kampuni changa, kujionea wenyewe namna mafunzo yao yatakavyoweza kutumika na kujenga mahusiano mapya kwenye maeneo ya kazi za kiteknolojia Berlin.

Ada ilikuwa ni moja kati ya kampuni za mwisho ambazo wanafunzi wa mpango wa Devugees walitembelea. Tulitumia masaa mawili tukibadilishana mawazo, ambapo moja kati ya wahandisi wetu wa maunzi laini (software) na mameneja wa bidhaa yetu, Valentin na David, walitoa madokezo ya mbinu za usimbaji na usimamiaji wa bidhaa na timu ya wafanyakazi. Kwa upande wa wanafunzi wa Devugees, wao walitoa madokezo mapya ya namna Ada inaweza kusaidia watu wengi zaidi duniani. Mpango kama wa Devugees ni ukumbusho muhimu wa nguvu ya teknolojia ya kubadilisha maisha kwenye ngazi ya kimataifa na kibinafsi. Kama Devugees wanavyosema kwenye tamko lao la misheni kwamba, “Tunaufahamu uwanja wa teknolojia na tunajua namna ya kupanga, kuunda na kutekeleza miradi,” na wakati mwengine msaada mahsusi unaweza ukawa wenye thamani kama thamani ya kuendeleza uvumbuzi ujao.


Mwandishi:

Ada

Your health companion