Ridhaa kwenye uchakataji wa data zako za afya binafsi ili kukupatia huduma zetu
Tarehe: 13 Novemba 2019
Kwa kuweka alama ya vema kwenye kisanduku, unatoa ridhaa ya uchakataji wa data za afya binafsi unazotupatia wakati wa kutmia app. Data hizi ni kama vile jinsia, tarehe ya kuzaliwa, data kwa ujumla kuhusu afya yako, dalili zako, uwezekano wa visababishi vya dalili, mizio, hali ya ujauzito, na historia husika ya matibabu, ili tuweze kukupatia Huduma zetu, k.v., tathmini ya data za afya yako binafsi na ushauri wa kiafya. Bila ridhaa yako kwenye uchakataji wa data hizi haiwezekani kutumia app yetu kwani ni hatua ya lazima inayohitajika ili kukupa tathmini yetu na ushauri wa kiafya.
Madhumuni zaidi tunayotumia data hizi yanajumuisha uchanganuzi wa maelezo ya kesi kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa mfumo wetu wa fikra za kitiba na utayarishaji wa takwimu zisizo na utambulisho katika usambazaji wa kijiografia wa dalili fulani za ugonjwa na magonjwa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu namna na kwa madhumuni gani tutatumia na kuchakata data zako binafsi, tafadhali rejea Sera yetu ya Faragha.