Sera ya Faragha ya Ada Health GmbH
Mabadiliko ya mwisho: 19 Machi 2021
TAFADHALI SOMA SERA HII KWA MAKINI KABLA YA KUTUMIA HUDUMA ZA ADA HEALTH GMBH
Unapaswa kuwa na umri wa miaka 16 au zaidi ili kutumia Huduma zetu.
Kulinda data zako, faragha na data binafsi (kama ilivyofasiriwa katika Kifungu cha 4(1) cha Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data (EU) 2016/679 (“GDPR”)) ni muhimu sana kwa Ada Health GmbH ( “sisi”, au “yetu”). Ni muhimu sana kwetu kwamba wateja wetu (“watumiaji”) wanajihisi salama wanapotumia bidhaa na huduma zetu.
Sera hii ya faragha (“Sera ya Faragha”), (pamoja na Sheria & Masharti yetu yaliyo katika ada.com/sw/terms-and-conditions, Sera yetu ya Vidakuzi iliyo katika ada.com/sw/cookie-policy na hati zinginezo zote zilizorejelewa ndani yake), inaweka msingi wa kuchakata data yoyote binafsi tunayokusanya kutoka kwako, au ambayo unatupa. Tafadhali soma sera hii ya faragha kwa umakini ili uelewe aina ya data tunayokusanya kutoka kwako, tunavyoitumia, hali inayoweza kupelekea sisi kuishiriki na watu wengine, na haki zako kuhusiana na data zako binafsi.
Wakati wa kutumia “Ada’ (kupitia programu yetu ya kidijitali (“App”)), wakati na pale inapopatikana programu yetu kwa njia ya tovuti (“Tovuti-pachika“) na kifaa chetu cha ukaguzi (“Kifaa cha Ukaguzi”), kwa pamoja (“Kifaa cha Kitiba”), au wakati wa kutumia tovuti yetu ya ada.com (“Tovuti”), au huduma yoyote na/ au bidhaa tutakayoweza kukupatia (Tovuti pamoja na Kifaa cha Kitiba na bidhaa na huduma zetu zozote, “Huduma”), utaombwa kuonyesha kuwa unatambua uwepo wa sera hii, na inapofaa, kutoa idhini yako kwa shughuli za uchakataji kama ilivyoelezewa katika Sera hii ya Faragha.
1. Sisi ni nani
Sera hii ya faragha inatumika kwa uchakataji wa data yoyote binafsi unaofanywa na Ada Health GmbH (HRB 189710), Neue Grünstraße 17, 10179 Berlin, Ujerumani kuwa mdhibiti wa data (kama inavyofafanuliwa chini ya Kifungu cha 4(7) cha GDPR) za masuala yote ya uchakataji yanayohusiana na Huduma.
Maswali, maoni na maombi kuhusu Sera hii ya Faragha yanakaribishwa na yanapaswa kutumwa kupitia fomu yetu ya mawasiliano hapa. Inawezekana kuwasiliana na afisa wetu wa ulinzi wa data kupitia [email protected].
2. Maelezo ya jumla ya uchakataji wetu wa data kuhusiana na Huduma
Kabla ya kuanza kutumia huduma zetu, unatakiwa kuthibitisha kwamba umesoma Sera yetu ya Faragha kwa umakini, na kuridhia Ada kuchambua data binafsi ya afya unayotoa ili kupatiwa tathmini na ushauri wa afya, ambao unaweza kupata muhtasari wa taarifa hapa.
Sehemu hii ya 2 inakusudia kukupa maelezo ya jumla na ya haraka ya shughuli za uchakataji wa data kuhusiana na huduma tunazokupatia.
Ikiwa ungependa kusoma kwa kina shughuli zote za uchakataji wa data tunazofanya, tunakushauri kusoma kifungu cha 3 kinachofuata kuhusiana na kila shughuli mahsusi ya uchakataji wa data, na sehemu za 4 mpaka 9 zinazohusiana na:
- vidakuzi vyetu & sera ya ufuatiliaji (Sehemu ya 4),
- mahala tunapohifadhi data zako binafsi (Sehemu ya 5),
- wakati gani tunaweza kufichua data zako binafsi (Sehemu ya 6),
- sera yetu ya kubaki na data (Sehemu ya 7),
- haki zinazohusiana na data zako (Sehemu ya 8),
- haki zako mahsusi ikiwa wewe ni mkazi wa California (Marekani) (Sehemu ya 9), na
- sera yetu ya mabadiliko (Sehemu ya 10).
Maelezo ambayo unatupatia: tunaweza kukusanya na kuchakata data binafsi utakayoombwa kutupatia wakati:
- unajaza fomu kwenye Tovuti yetu, unatuma maombi kwa ajili ya ofa ya kazi, au vinginevyo unawasiliana nasi kwa njia zozote zilizopo;
- unajiandikisha kutumia Huduma zetu, kujiunga na kijarida chetu, barua pepe za matangazo au nyenzo nyingine zozote za masoko;
- unatumia Huduma zetu;
- unaripoti hitilafu kuhusiana na Huduma zetu; au
- Kamilisha kujaza tafiti zozote au kutoa mrejesho ambao tunaweza kuutumia kwa madhumuni ya utafiti na uboreshaji (ingawa ni hiari, na haulazimiki kushiriki katika hizi tafiti ikiwa hutaki).
Maelezo ambayo tunaweza kukuomba utoe yanajumuisha, lakini hayaishii tu kwenye, jina lako, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, anwani ya barua pepe, nambari ya simu, dalili za ugonjwa wako, mambo yanayoweza kuwa visababishi vya dalili za ugonjwa wako, bima ya afya (hiari), historia ya matibabu, mizio yoyote uliyonayo, au maelezo zaidi yanayohitajika ili kuthibitisha utambulisho wako.
Maelezo tunayokusanya kukuhusu: Ingawa hatutayatumia kukutambua, tunaweza kukusanya maelezo yafuatayo kila wakati unapotembelea na kutumia Huduma zetu:
- Data ya matumizi: maelezo ya kiufundi kuhusu kifaa chako ikijumuisha maelezo maalum ya kifaa kama vile muundo wa kifaa chako, toleo la mfumo wa uendeshaji, vitambulisho maalum vya kifaa, na maelezo ya mtandao wa kifaa; maelezo ya kina ya mara ulizotembelea, pamoja na mtiririko wa Vitambuzi Sare vya Rasilimali (“URL”) vya kuingia, kupitia na kutoka kwenye Huduma zetu (pamoja na tarehe na saa); maelezo ya kina ya magonjwa na dalili zilizotafutwa;
- Data ya uchambuzi: anwani yako ya IP, mfumo wa uendeshaji wa kifaa na aina ya kivinjari; maelezo kuhusu duka gani la app ulilopakulia App yetu; urefu wa muda uliotumia kwenye kurasa fulani, na maelezo ya matumizi kwenye ukurasa (kama vile misogeo ya kiteuzi, ishara za vidole, mibofyo na matumizi ya kiteuzi).
Ikiwa unatumia Huduma zetu kwa niaba ya mtu mwingine, sharti uwe umepata ruhusa isiyo na mashaka kutoka kwa watu ambao unatupatia data zao kabla ya kushiriki data hizo. Ili kuepusha mashaka yoyote, marejeo yoyote katika Sera hii ya Faragha kwenye "data zako" yatajumuisha data zinazohusu watu wengine ambazo umetupatia.
Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo vya tovuti nyingine. Ikiwa unafuata kiungo chochote cha hizo tovuti nyingine, tafadhali tambua kwamba zina sera zake za faragha na kwamba hatuna jukumu lolote au dhima itokanayo na sera zao au uchakataji wa data zako binafsi. Tafadhali kagua sera hizi kabla ya kuwasilisha data zozote binafsi kwenye tovuti nyingine kama hizi.
3. Ni data zipi binafsi tunaweza kukusanya na kuchakata, kwanini na kwa muda gani
3.1 Unapotumia Tovuti yetu
- Aina za data: Anwani ya IP ya kifaa kinachotumika, tarehe na saa za kufikia, jina na URL ya faili iliyoombwa, Tovuti iliyotoa njia ya kufikia (“Rufaa ya URL"), kivinjari kilichotumika na, ikihitajika, mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako na kitambulisho cha mtoa huduma za ufikiaji wako.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia data zilizo hapo juu ili kukuwezesha kufikia Tovuti yetu, kuhakikisha kwamba Tovuti inaweza kamata intaneti kiulaini na ni rahisi kutumia; kuchambua usalama na uthabiti wa mfumo, na pia kwa madhumuni ya ziada ya kiusimamizi.
- Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea madhumuni ya kukusanya data yaliyoorodheshwa ndani ya “Dhumuni la uchakataji.” Hatutumii data zilizokusanywa kwa dhumuni la kukutambua. Haulazimiki kutoa data binafsi zilizoanishwa hapo juu. Hata hivyo, hautoweza kufikia Tovuti ikiwa data binafsi za aina hiyo hazikutolewa.
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itaondolewa baada ya siku 15, isipokuwa likitokea tukio lolote linalohusiana na usalama (kwa mfano, shambulio la DDoS). Ikiwa kuna tukio linalohusiana na usalama, faili za kumbukumbu za seva zitahifadhiwa hadi tukio hili linalohusiana na usalama limeondolewa na kufafanuliwa kabisa.
3.2 Unaposajili akaunti ya mtumiaji au kuunda maelezo mafupi (profile) mapya
- Aina za data: Anwani ya barua pepe na nywila, Kitambulisho (ID) cha akaunti, Kitambulisho cha kifaa, jina la maelezo mafupi, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, bima ya afya (hiari), maelezo ya jumla kuhusu afya yako (hiari) kama vile uvutaji sigara, kuongezeka kwa shinikizo la damu, kisukari na hali ya ujauzito, tarehe, muda na mahali pa usajili.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia data zilizo hapo juu ili kukupa akaunti ya mtumiaji na kukuwezesha kutumia Kifaa chetu cha Kitiba. Tunatumia maelezo ya jumla ya afya kwa uchambuzi wa msingi. Haiwezekani kutumia Kifaa chetu cha Kitiba ikiwa data (zisizo za hiari) hazijatolewa. Ikiwa unatumia Kifaa chetu cha Kitiba kupitia programu ya Tovuti-pachika, kwa idhini yako tunaweza kufichua matumizi ya data zilizofichwa utambulisho (bila kujumuisha data zozote binafsi za afya) kwa washirika wetu ambao ni wenyeji wa Tovuti-pachika hiyo.
- Uhalalishaji wa matumizi: Utendaji wa mkataba (Kifungu cha 6 (1) (b) GDPR / Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR) kwa uchakataji wa data zako za afya.
- Muda wa kuhifadhi: Tunachakata data zako kwa madhumuni yaliyoanishwa hapo juu mpaka utakapoomba kufutwa kwa akaunti yako au utakapofuta akaunti yako. Ikiwa haujatumia akaunti yako kwa zaidi ya miezi 24, tutawasiliana na wewe kubaini ikiwa unataka kuendelea kutumia Kifaa chetu cha Kitiba. Ikiwa utaacha tena akaunti yako ya mtumiaji bila matumizi kwa miezi mingine 3, tutafuta akaunti yako. Katika hali hizo zote mbili, tutafuta akaunti yako ndani ya mwezi 1 na kufuta au kuficha moja kwa moja utambulisho wa data zako (ili zisiweze kuhusishwa na mtu mahsusi asilia). Tutabaki na data zako kwa muda zaidi (angalia sehemu ya 7 kwa maelezo zaidi), kwa mfano, kwa madhumuni ya kuanzisha, kutekeleza au kujitetea dhidi ya madai ya kisheria na kutimiza viwango vya juu vya ubora na usalama, hususani wajibu wetu katika uchambuzi na uelewa wa data kuhusiana na soko la Kifaa chetu cha Kitiba (Post-Market Surveillance) lakini hatutachakata data hizo kwa madhumuni mengine yoyote.
3.3 Maelezo mafupi ya Afya
- Aina za data: Urefu wa mwili na uzito, dawa zozote unazotumia (za kudumu au sio) na mizio yoyote unayoweza kuwanayo.
- Dhumuni la uchakataji: Kipengele hiki kinakuruhusu kuunda maelezo ya kina ya afya ili kusimamia data zako za afya katika Kifaa chetu cha Kitiba. Hata hivyo, hatutachakata data unazotoa kwa uundaji wa maelezo mafupi ya afya ili kubaini matokeo ya tathmini kwa mujibu wa sehemu ya 3.5.
- Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 9(2)(a) GDPR). Unaweza kubatilisha/kuondoa idhini yako muda wowote.
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa hadi wakati ambapo haitahitajika tena kwa dhumuni ambalo ilikusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.
3.4 Kuingia kwa Facebook/ Kuingia kwa Apple
- Aina za data: Kitambulisho cha Facebook, Kitambulisho cha mtumiaji cha Apple, anwani ya barua pepe (ikiwa unaipa Facebook ruhusa ya kutupa hiyo anwani), muda na tarehe ya kuingia.
- Dhumuni la uchakataji: Ukichagua kutumia na kuingia kwa kutumia Facebook au Apple, tutapokea data zilizoorodheshwa hapo juu kutoka Facebook au Apple na idhini yako kujaza data zako za mtumiaji kwenye App, na kuthibitisha utambulisho wako. Tafadhali tambua kwamba ikiwa unaingia kupitia Facebook au Apple, Facebook au Apple wanaweza pia kuchakata data zako (ID ya Facebook/ ID ya Apple, metadata, baadhi ya matukio ya app na kipimo cha kifaa). Hatuwajibiki na uchakataji wa data hizi; unaweza kujifunza zaidi kuhusu hili katika Sera ya Faragha ya Facebook / Sera ya Faragha ya Apple.
- Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali ni kuwapa watumiaji ambao hawana akaunti ya barua pepe au wanaotaka kuingia kwa kutumia akaunti yao ya Facebook au akaunti yao ya Apple chaguo la kutumia Huduma zetu / Utendaji wa mkataba (Kifungu cha 6 (1) (b) / Idhini (Kifungu cha 6 (1)(a) GDPR).
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa madhumuni haya unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Data inayochakatwa na Facebook au Apple, ambayo hatuidhibiti ikiwa utachagua kuingia kwa kutumia Facebook au Apple, inaweza kusalia kwenye seva za Facebook au Apple. Ikiwa unafuta akaunti yako ya Facebook au acha kutumia kifaa chako cha Apple na unataka kutumia App, utaelekezwa kuingia kwa kutumia anwani ya barua pepe au utaratibu mwingine wa kuingia.
3.5 Unda kesi ya tathmini
- Aina za data: ID ya maelezo mafupi, jina la maelezo mafupi (ikiwa inahusu) na data husika za afya binafsi zinazohitajika ili kutoa tathmini kama vile umri, jinsia, dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, mizio, hali ya ujauzito, na historia muhimu na/au inayohusiana na matibabu, mahali pa kijiografia, muda na tarehe ya tathmini.
- Madhumuni ya uchakataji: Ili kukupa tathmini yetu kwa kutumia Kifaa chetu cha Kitiba, kwa mfano, lakini haiishii tu kwenye, kupendekeza uwezekano wa visababishi vya dalili zilizotolewa (tathmini), na kufuatilia dalili zako.
- Uhalalishaji wa matumizi: Utendaji wa mkataba (Kifungu cha 6 (1) (b) GDPR / Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR) kwa uchakataji wa data zako za afya. Unaweza kubatilisha/ kuondoa idhini yako wakati wowote; hata hivyo, haiwezekani kuruhusu matumizi ya Kifaa chetu cha Kitiba (yaani, kutoa tathmini) bila idhini kama hiyo.
- Muda wa kuhifadhi: Kwa kawaida, muda wa kuhifadhi unakwenda sambamba na muda wa kuchakata kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Isitoshe, unaweza kuomba ufutaji wa kesi mahsusi au kufuta kesi hiyo mwenyewe. Halafu ndani ya mwezi 1 tutafuta au kufanya data za kesi yako zisitambulike tena(ili zisiweze kuhusishwa na mtu mahsusi asilia). Tutabaki na baadhi ya data zako kwa muda zaidi (angalia sehemu ya 7 kwa maelezo zaidi) lakini hatutachakata data hizo kwa madhumuni mengine yoyote.
3.6 Uchanganuzi wa maelezo ya kesi ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba
- Aina za data: ID ya akaunti (ikiwa inahusu), ID ya maelezo mafupi (ikiwa inahusu), ID ya kesi, muda na tarehe ya tathmini, eneo la kijiografia la tathmini, data zilizotolewa kwenye kesi (data binafsi zinazohitajika ili kutoa tathmini kama vile umri, jinsia, dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, mizio, hali ya ujauzito, na historia muhimu na/ au inayohusiana na matibabu), nakala ya mrejesho, matokeo ya tathmini, na data kuhusiana na maunzi laini na kifaa (kama vile namba za toleo, mfumo wa uendeshaji, na ID ya kifaa).
- Dhumuni la uchakataji: Ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba, ni lazima kukagua ubora wa matokeo ya tathmini (“Uchanganuzi”). Timu ya usalama na ubora (“Wastadi wa Tiba”) hutumia data ya majina bandia, na inapofaa, data za jumla, ili kutathmini matokeo ya tathmini na kubaini kama uboreshaji wowote unahitajika ili Kifaa chetu cha Kitiba kikidhi viwango vya juu kabisa vya ubora na usalama.
- Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji huo unahitajika ili kutimiza viwango vya lazima vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba ambacho kinakidhi sifa za kuwa kifaa cha kitiba chini ya kanuni za kifaa cha kitiba na kama ilivyoainishwa katika maandishi ya kisheria yafuatayo (Sehemu ya 22 (1) (1)(c) BDSG, Kifungu cha 9 (2) (i) GDPR), kutokana na msingi wa wajibu wa kufanya Uchunguzi wa data baada ya mauzo ya kifaa (Post-Market Surveilance) chini ya Sehemu ya 6 (1), (2) MPG kuhusiana na Sehemu ya 7 (4) ya Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Kijerumani kuhusiana na Viambatisho vya X, VII, (4) vya Maagizo ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (93/42 / EC) (au uchakataji unahusika moja kwa moja kuanzia tarehe 26.05.2021 na siyo mbele ya hapo, lakini ikichukuliwa kama tayari unahusika ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba, Kifungu cha 83 na Kiambatisho cha III cha Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (2017/745/EU)).
- Muda wa kuhifadhi: Tunachakata data zako mpaka pale haitokuwa lazima tena kwa madhumuni yaliyoanishwa hapo juu. Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na wajibu wetu wa kukidhi viwango vya lazima vya ubora na usalama wa App yetu.
3.7 Kutathmini ufaafu wako na kukualika katika utafiti wa kitiba na kukuelekeza kwenye huduma za afya kwa uchunguzi zaidi wa aina na sababu za ugonjwa
- Aina za data: Anwani ya barua pepe, ID ya akaunti, jina la maelezo mafupi, tarehe ya kuzaliwa, dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio, mahali pa kijiografia, muda na tarehe ya tathmini, na data nyingine ambazo umetupa.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia data zilizo hapo juu kutathmini ufaafu wako wa kushiriki katika utafiti wa kitiba na kuwasiliana nawe ili kukualika kushiriki katika utafiti wa kitiba na mmoja wa washirika wetu wa utafiti wa kitiba ambaye anaweza kuwa na maslahi kwako na/au kukuelekeza kwenye huduma za afya kwa uchunguzi zaidi wa aina na sababu za ugonjwa. Ili kuepuka mashaka, hatutumi data yoyote binafsi kwa washirika wetu wa utafiti wa kitiba bila idhini yako na ushiriki wowote kwenye tafiti za kitiba za aina hiyo na uelekezaji kwenye huduma za afya ni hiari na inategemea na idhini yako kabla ya hatua hizo.
- Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 6(1)(a) na Kifungu cha 9 (2)(a) GDPR utakaporidhia kushiriki kwenye tafiti za kitiba za aina hiyo na kwamba data zako zinahitajika kuchakatwa kwa madhumuni yaliyotangulia kutajwa. Unaweza kubatilisha/kuondoa idhini yako muda wowote (maelezo zaidi kuhusu haki zinazohusiana na data zako yapo katika sehemu ya 8 hapo chini).
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitatumika tena kwa dhumuni hili.
3.8 Matumizi ya data za afya kwa madhumuni ya takwimu na utafiti
- Aina za data: ID ya akaunti (ikiwa inahusu), ID ya kesi, ID ya maelezo mafupi (ikiwa inahusu), umri, jinsia, dalili za ugonjwa, mahali pa kijiografia, sababu hatarishi, matokeo ya tathmini kama vile uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio, muda na tarehe ya tathmini, na data nyingine husika na zinazohusiana unazoweza kuwa umetupatia.
- Madhumuni ya uchakataji: Tunachakata data zilizofichwa utambulisho ili kukusanya takwimu za jumla za ueneaji wa kijiografia wa aina fulani za dalili na magonjwa, na kuwasilisha muhtasari wa aina hizo za takwimu kwa washirika wetu katika utaratibu ambao zinakuwa zimefichwa utambulisho usiobatilishika.
- Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji huo ni muhimu kwa madhumuni ya kitakwimu na tunawapa washirika wetu muhtasari tu wa takwimu zilizofichwa utambulisho ambapo haiwezekani kumtambua mtu mahsusi asilia (Kifungu cha 9 (2) (j) GDPR; Sehemu ya 27 (1) BDSG). Maslahi yetu halali katika uchakataji wa data kwa madhumuni haya ni kusaidia maendeleo ya utafiti wa kitiba sambamba na malengo yetu ya kiujasiriamali ambayo pia ni kwa maslahi ya umma kuboresha huduma za afya kama vile, lakini hayaishii tu kwenye, kuchanganua utokeaji na tabia za magonjwa. Unaweza, kwa sababu zinazotokana na hali yako mahsusi, kupinga kufanyika kwa uchakataji huo wakati wowote kwa kutuandikia hapa (maelezo zaidi kuhusu haki yako ya kupinga yapo katika Sehemu ya 8 hapo chini).
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data yako kwa msingi wa uundaji takwimu hizi unategemea kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitatumika tena kwa madhumuni haya. Utambulisho wa takwimu umefichwa.
3.9 Matumizi ya data za afya kwa madhumuni ya afya ya jamii
- Aina za data: ID ya akaunti (ikiwa inahusu), jina la maelezo mafupi (ikiwa inahusu), ID ya kesi, ID ya kifaa, umri, jinsia, dalili za ugonjwa, mahali pa kijiografia, mambo yenye kuhatarisha, matokeo ya tathmini kama vile uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio, muda na tarehe ya tathmini, na data nyingine husika na zinazohusiana unazoweza kuwa umetupatia.
- Dhumuni la uchakataji: Tunachakata data za kiafya zilizofichwa utambulisho kwa madhumuni ya afya ya jamii (kama ilivyoelezewa na GDPR kariri 54) kama vile kuchanganua data za kesi zinazohusiana na mwenendo wa afya ya jamii, magonjwa adimu na matishio na kutambua mambo yatakayoweza kuboresha afya ya jamii kama vile kutafuta kuhusu ueneaji wa magonjwa mahususi, sifa za magonjwa mahususi na kupata ufahamu kwenye vipengele mahususi vya tathmini. Kwa changanuzi hizi tunasaidia kubaini milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na kufuatilia maendeleo yake kiwakati na kimaeneo (k.m. wakati wa ueneaji wa ugonjwa wa COVID-19). Kwasababu data zetu zinajumuisha pia watu ambao bado hawajawasiliana na mfumo wa huduma ya afya, tunaweza tukakadiria vizuri zaidi gharama halisi ya magonjwa.Tunaweza kushiriki (share) na kuwasilisha matokeo kama muhtasari wa takwimu kwa washirika wetu, k.m. katika afya ya jamii na jumuiya ya kisayansi, sikuzote zikiwa zimefichwa utambulisho usiobatilishika. Tunaweza pia kuchakata data za aina hiyo ili kukupatia mwongozo bora kabisa kadiri iwezekanavyo, kwa mfano, kwa kukuelekeza kwenye kituo cha huduma kinachofaa zaidi na kukusaidia kupunguza majukumu yasiyo ya lazima, lakini pia kupunguza majukumu kwenye mifumo ya huduma za afya.
- Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji ni lazima kwa sababu ya maslahi ya jamii katika eneo la afya ya jamii (Kifungu cha 9 (2)(i) GDPR, kifungu cha 22 (1) (1) c) BDSG)). Maslahi yetu halali katika kuchakata data kwa madhumuni haya ni kusaidia maendeleo ya afya ya jamii kwa kudhibiti matishio makubwa ya kimipaka kwa afya. Kwasababu zinazotokana na hali yako mahsusi, unaweza kukukataa kufanyika kwa uchakataji wa aina hiyo wakati wowote kwa kutuandikia hapa (maelezo zaidi kuhusu haki yako ya kukataa yanapatikana katika Sehemu ya 8 hapo chini).
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako zilizofichwa utambulisho katika msingi ambao tunaunda takwimu unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitotumika tena kwa dhumuni hili.
3.10 Kufuatilia na kuboresha usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba
- Aina za data: Dalili za ugonjwa wako, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa wako, ID ya akaunti (ikiwa inahusu), jina la maelezo mafupi (ikiwa inahusu), umri, jinsia, mahali pa kijiografia (nchi), anwani ya IP, ID ya kifaa, matukio yoyote wakati wa kutumia Kifaa cha Kitiba kama vile, lakini hayaishii tu kwenye, tathmini iliyoanza au tathmini iliyomalizika.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia seti ndogo ya data ya matumizi (ambayo inaweza kujumuisha data za afya binafsi) kwa ajili ya masuala mawili, yaani kufuatilia utumiaji ili kuhakikisha kuwa Kifaa chetu cha Kitiba kinakidhi viwango vya juu vya ubora na usalama vinavyohitajika kwa vifaa vya kitiba, na kugundua uwezekano wa hitilafu zozote, tathmini zisizo sahihi, au matatizo katika upatikanaji au utumiaji. Kwa mfano, ikiwa unamaliza kufanya tathmini na kuipa alama kuwa ‘haijasaidia’, halafu kuonyesha kwamba haijasaidia kwasababu imekupa matokeo yasiyo sahihi, upatikanaji wa data hii husaidia madaktari wetu kuangalia tathmini husika na kuamua ikiwa kubadilisha mtiririko wa maswali kunaweza kuboresha usalama wa kitiba.
- Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji huo unahitajika ili kutimiza viwango vya lazima vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba ambacho kinakidhi sifa za kuwa kifaa cha kitiba chini ya kanuni za kifaa cha kitiba na kama ilivyoainishwa katika maandishi ya kisheria yafuatayo (Sehemu ya 22 (1) (1)(c) BDSG, Kifungu cha 9 (2) (i) GDPR), kutokana na msingi wa wajibu wa kufanya Uchunguzi wa data baada ya mauzo ya kifaa (Post-Market Surveilance) chini ya Sehemu ya 6 (1), (2) MPG kuhusiana na Sehemu ya 7 (4) ya Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Kijerumani kuhusiana na Viambatisho vya X, VII, (4) vya Maagizo ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (93/42 / EC) (au uchakataji unahusika moja kwa moja kuanzia tarehe 26.05.2021 na siyo mbele ya hapo, lakini ikichukuliwa kama tayari unahusika ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba, Kifungu cha 83 na Kiambatisho cha III cha Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (2017/745/EU)).
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na wajibu wetu wa kutimiza viwango vya lazima vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba.
3.11 Shiriki taarifa chache na ongeza athari ya Ada
- Aina za data: ID ya mtangazaji, upakuaji na usanikishaji wa App kwenye kifaa chako cha mkononi, maelezo ya namna ulivyofahamu kuhusu sisi (kwa mfano., kupitia mitandao ya kijamii au makala ya mtandaoni), ikiwa usajili wako na uundaji wa kesi mpya kwenye App yetu ulifanikiwa, na ukadiriaji wako wa ubora wa App yetu kwenye Maduka ya App, mahali pa kijiografia, muda na tarehe.
- Dhumuni la uchakataji: Tunachakata baadhi ya data za matumizi (ambayo haijumuishi data binafsi za afya) ikiwa unatumia App, ili kuelewa namna Ada inavyowafikia watu mtandaoni. Hii inatusaidia kushiriki taarifa husika na wewe na wengine wenye uwezekano wa kuwa watumiaji. Kwa mfano, ikiwa umeshapakua Ada, hii inamaanisha hautoona tena matangazo yanayokutaka upakue Ada unapokuwa mtandaoni. Taarifa hii inatusaidia pia kuelewa namna tunayoweza kufikia watu wengi zaidi mtandaoni ambao wanaweza kunufaika na utaalamu wa kitiba wa Ada. Tunatumia tu data ya matumizi iliyoondolewa majina ambayo tunakusanya kupitia mchakataji wetu wa kandarasi Adjust GmbH (Saarbrücker Str. 38a, 10405 Berlin, Ujerumani). Hatutoshiriki kamwe taarifa zako binafsi za afya na watengeneza matangazo au watu wengine.
- Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 6 (1) (a) GDPR).
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa hadi wakati ambapo haitahitajika tena kwa dhumuni ambalo ilikusanyiwa. Tutafuta data hizi ndani ya siku 45.
3.12 Kufuatilia matumizi ili kuhakikisha utumiaji sahihi, utendaji, udumishaji na uboreshaji wa huduma na barua pepe husika
- Aina za data: ID ya kifaa, anwani yako ya IP, mfumo wa uendeshaji na aina ya kivinjari, urefu wa muda uliotumia kwenye kurasa fulani, na maelezo ya matumizi kwenye ukurasa, kama vile misogeo, ishara za vidole, mibofyo na matumizi ya kiteuzi, mahali pa kijiografia, muda na tarehe, matukio yoyote wakati wa kutumia Kifaa cha Kitiba kama vile, lakini hayaishii tu kwenye, tathmini iliyoanza au tathmini iliyomalizika.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia kiasi kidogo cha data za matumizi (ambacho hakijumuishi data binafsi za afya) kuhakikisha utumiaji sahihi, utendaji, udumishaji na uboreshaji wa Huduma zetu kwa watumiaji wote.
- Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea matumizi yaliyotajwa awali ya madhumuni hayo ya data. Katika hali yoyote ile hatutatumia data tuliyoikusanya kubaini utambulisho wako. Tunaweza kuchakata matumizi ya ukurasa wakati unatumia Huduma zetu au unapokea barua pepe tunazoweza kukutumia ili kuhakikisha unazipokea bila shida na kutathmini huduma kwa lengo la kuiboresha. Kwasababu zinazotokana na hali yako mahsusi, unaweza kukataa kufanyika kwa uchakataji huo wakati wowote kwa kutuandikia hapa (maelezo zaidi kuhusiana na haki yako ya kukataa yapo katika sehemu ya 8 hapo chini).
- Muda wa kuhifadhi: Data yako inaondolewa baada ya siku 15, isipokuwa likitokea tukio lolote linalohusiana na usalama (kwa mfano, shambulio la DDoS). Ikiwa kuna tukio linalohusiana na usalama, faili za kumbukumbu za seva zitahifadhiwa hadi tukio hili linalohusiana na usalama limeondolewa na kufafanuliwa kabisa.
3.13 Masoko ya moja kwa moja kwa bidhaa na huduma zetu zinazofanana
- Aina za data: Anwani ya barua pepe, jina la maelezo mafupi (profile), pendekezo la jinsia.
- Dhumuni la uchakataji: Kupokea matangazo ya moja kwa moja (bidhaa na huduma) au mawasiliano kuhusu utafiti wowote ambao tunaamini utakuwa na maslahi kwako. Unaweza kurekebisha mipangilio yako ya matangazo wakati wowote kwa kutumia kiungo kilicho chini ya kila barua pepe ya matangazo, au kwa kutuma ombi lako la kujiengua hapa.
- Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR)
- Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.
3.14 Kuboresha mipango yetu ya masoko
- Aina za data: ID ya kifaa, anwani ya IP, mfumo wa uendeshaji na aina ya kivinjari, urefu wa muda uliotumia kwenye kurasa fulani, na maelezo ya matumizi kwenye ukurasa, kama vile misogeo, ishara za vidole, mibofyo na matumizi ya kiteuzi, mahali pa kijiografia, muda na tarehe.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia kiasi kidogo cha data za matumizi (ambacho hakijumuishi data binafsi za afya) kufuatilia matumizi ya ukurasa wako na kuchanganua data ili kuboresha mipango yetu ya masoko.
- Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 6 (1) (a) GDPR). Unaweza kupangilia utakavyo muda wowote namna ya ufuatiliaji kupitia mipangilio ya faragha katika App, au kwa kutuandikia hapa.
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa mpaka itakapokuwa haihitajiki tena kwa dhumuni iliyokusanyiwa, au utakapobatilisha idhini yako. Muda wa kuhifadhi data yako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na muda wa kuchakata kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2. Data tunayochakata kwa dhumuni la kufuatilia inaondolewa ndani ya siku 45.
3.15 Ripoti za utendaji
- Aina za data: Hitilafu, ripoti za hitilafu pamoja na kifaa, app na taarifa mahsusi za tukio (k.m. Toleo la App), anwani ya IP, URL, eneo la kijiografia, muda na tarehe.
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia data iliyo hapo juu (ambayo haijumuishi data ya kibinafsi ya afya) ili kuhakikisha utendaji wa Huduma zetu (Huduma zetu haziwezi kufanya kazi vizuri bila uchakataji huu) na pia kuzuia utenganishaji wowote au vinginevyo kunakili uhandisi wa bidhaa yetu. Tunatumia tu data ya matumizi yenye majina bandia ambayo tunaweza kukusanya kupitia huduma ya mchakataji wetu Functional Software Inc., 132 Hawthorne Street, San Francisco, California 94107 USA ("Sentry"). Data hii inaweza kutumwa na kuhifadhiwa kwenye seva za Sentry. Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma sera ya faragha ya Sentry hapa. Tunaweza pia kutuma data za kibinafsi za hapo juu kwa mchakataji wetu Sumo Logic, kampuni yenye makao makuu yake katika anwani ifuatayo: 305 Main Street, Redwood City, CA 94063, USA. Data iliyokusanywa katika maudhui haya haitumiki kuunganisha profaili yoyote ya matumizi na data zako za kibinafsi. Data zako za kibinafsi zinaweza kupelekwa na kuhifadhiwa katika seva za Sumo Logic. Taarifa zaidi zinaweza kupatikana katika tamko la Faragha la Sumo Logic hapa.
Pia tunahamisha data za kibinafsi kwa mchakataji wetu Hound Technology, Inc., 548 Market Street, 25362 San Francisco, CA 94104-5401 ("Honeycomb"). Data zilizochakatwa katika maudhui haya zimefichwa utambulisho na Honeycomb haiwezi kuziunganisha kwako. Ada haiunganishi profaili yoyote ya matumizi na data yako ya kibinafsi. Taarifa zaidi zinaweza kupatikana katika Sera ya Faragha ya Honeycomb hapa.
Tumekubaliana katika Vifungu vya Kawaida vya Mkataba na majukumu ya ziada ya kimkataba na kila mmoja wa watoa huduma hawa. Zaidi, tutatathmini, kwa kesi-na-kesi, hatari zilizopo kwenye haki zako na faragha, pamoja na ulazima wa kuendelea nao ili kukupatia Huduma zetu. Ikiwa una swali lolote kuhusu hatua za ziada tunazochukua, tafadhali jisikie huru kuwasiliana nasi kupitia barua pepe ifuatayo: [email protected]. - Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea matumizi yaliyotajwa awali ya madhumuni hayo ya data. Katika hali yoyote ile hatutatumia data tuliyoikusanya kubaini utambulisho wako.
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itaondolewa baada ya siku 60, isipokuwa likitokea tukio linalohusiana na usalama (kwa mfano, shambulio la Kuzuia Kutoa Huduma). Ikiwa tukio linalohusiana na usalama linatokea, faili za kumbukumbu za seva zitahifadhiwa hadi tukio hili linalohusiana na usalama limeondolewa na kufafanuliwa kabisa.
3.16 Maoni / Uchunguzi
- Aina za data: nakala ya maoni ambayo inaweza kujumuisha data binafsi, anuani ya barua pepe, (hiari), data zilizotolewa kwenye kesi (ikiwa tu unatupa anwani yako ya barua pepe, na umefungua akaunti kwetu, ambayo inaturuhusu kukutambua, kwa madhumuni tu yaliyoainishwa hapo chini).
- Dhumuni la uchakataji: Tunatumia maoni unayoweza kutupa (hiari) kuchanganua ikiwa umeridhika au haujaridhika na bidhaa na huduma zetu, na kutathmini mtazamo wako kwa ujumla. Hii ni nyenzo ya msingi kwetu katika kuboresha urahisi wa utumiaji wako na kurekebisha matendo yetu kulingana na mahitaji yako. Tunaweza pia kutumia maoni unayoweza kutupa (hiari) kukuhakikishia viwango vya juu vya ubora na usalama wa Kifaa chetu cha Kitiba, kama ilivyoelezewa katika Sehemu ya 3.5 hapo juu.
- Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR): ili kuboresha urahisi wa utumiaji wako na kurekebisha matendo yetu kulingana na mahitaji yako. Katika hali yoyote ile hatutatumia data tulizokusanya kubaini utambulisho wako.
- Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa mpaka itakapokuwa haihitajiki tena kwa lengo ililokusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data zako kwa lengo hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.
3.17 Usajili wa kutumia Tovuti na Kifaa cha Matokeo
- Aina za data: ID ya akaunti, jina, anwani, tarehe ya kuzaliwa, jinsia ya kuzaliwa, anwani ya barua pepe, matokeo ya kipimo
- Dhumuni la uchakataji: Tunakupa usajili wa kutumia tovuti na kifaa cha matokeo (“Kifaa cha Usajili na Matokeo”) kwa kushirikiana na Labor Berlin - Charité Vivantes GmbH. Tunachakata data zako ili kuwasilisha usajili wako kwa Labor Berlin na kukutaarifu kuhusu matokeo. Isitoshe, tunatumia data za hapo juu kukupa akaunti ya mtumiaji. Labor Berlin ndio mdhibiti pekee wa uchakataji unaohusiana na utekelezaji wa kipimo. Sisi ni wadhibiti wa uchakataji unaohusiana na utumiaji wako wa Kifaa cha Usajili na Matokeo.
- Uhalalishaji wa matumizi: Utendaji wa mkataba (Kifungu cha 6(1)(b) GDPR / Idhini (Kifungu cha 9(2)(a) GDPR kwa ajili ya data zako za afya). Unaweza kubatilisha/ kuondoa idhini yako wakati wowote; hata hivyo, haitowezekana kukupa huduma yetu ya Kifaa cha Usajili na Matokeo bila idhini ya namna hiyo.
- Muda wa kuhifadhi: Tunachakata data zako kwa madhumuni yaliyoanishwa hapo juu mpaka utakapoomba kufutwa kwa akaunti yako au utakapofuta akaunti yako. Ikiwa haujatumia akaunti yako kwa zaidi ya miezi 24, tutawasiliana na wewe kubaini ikiwa unataka kuendelea kutumia Kifaa chetu cha Usajili na Matokeo. Ikiwa utaacha tena akaunti yako ya mtumiaji bila matumizi kwa miezi mingine 3, tutafuta akaunti yako. Katika hali hizo zote mbili, tutafuta akaunti yako ndani ya mwezi 1 na kufuta au kuficha moja kwa moja utambulisho wa data zako (ili zisiweze kuhusishwa na mtu mahsusi asilia). Tutabaki na data zako kwa muda zaidi (angalia sehemu ya 7 kwa maelezo zaidi), kwa mfano, kwa madhumuni ya kuanzisha, kutekeleza au kujitetea dhidi ya madai ya kisheria lakini hatutachakata data hizo kwa madhumuni mengine yoyote.
3.18 Maombi ya kazi
- Aina za data: Jina la mwanzo, jina la mwisho/ukoo, anwani ya barua pepe, namba ya simu, mahali pa kijiografia (mji), wasifu wa kazi, akaunti ya Linkedin (hiari), muda na tarehe ya maombi.
- Dhumuni la uchakataji: Ikiwa ni mtuma maombi ya kazi kupitia tovuti yetu, tunaweza kuchakata data za hapo juu ili kukagua ufaafu wako wa nafasi unayoomba (au nafasi nyingine zilizo wazi ndani ya kampuni yetu) na kuendesha mchakato wa maombi.
- Uhalalishaji wa matumizi: Ili kuchukua hatua kwenye ombi lako kabla ya kuingia mkataba (Kifungu cha 6 (1)(b) GDPR).
- Muda wa kuhifadhi: Ikitokea ombi la kazi halijakubaliwa, data za muombaji zitafutwa baada ya miezi 6. Ikiwa umetoa idhini ya muendelezo wa kuhifadhi data zako binafsi, tutaongeza data zako kwenye hifadhi yetu ya waombaji. Data zitafutwa baada ya miaka miwili kutoka wakati huo. Ikiwa unapata kazi katika muktadha wa mchakato wa maombi, data kutoka kwenye mfumo wa data zitahamishiwa kwenye mfumo wetu wa Rasilimali Watu.
4. Vidakuzi na ufuatiliaji kwenye Tovuti yetu
Tovuti yetu hutumia vinavyojulikana kama "vidakuzi". Vidakuzi ni faili za maandishi zilizohifadhiwa kwenye kivinjari cha Intaneti au zilizohifadhiwa na kivinjari cha Intaneti kwenye kifaa chako (kompyuta, kompyuta kibao au simu). Tunatumia neno "vidakuzi" kumaanisha vifaa vyote ambavyo vinakusanya data kwenye Tovuti yetu (k.m. anwani za IP, mahali na wakati wa kutembelea). Data yako iliyokusanywa kwa njia hii hupewa jina bandia na haihifadhiwi pamoja na data zako nyingine binafsi. Uchakataji huu hufanywa kwa msingi wa kisheria na, pale inapotakiwa kisheria, kwa mujibu wa idhini yako.
Kwa maelezo ya kina kuhusu ufuatiliaji wa watumiaji wetu na vidakuzi tunavyotumia, madhumuni ya kuvitumia na kudhibiti mapendeleo yako ya Vidakuzi, rejelea Sera yetu ya Vidakuzi.
5. Tunahifadhi wapi data zako binafsi
Data binafsi ambazo tunakusanya kutoka kwako huhifadhiwa katika Umoja wa Ulaya kwenye Cloud Servers za Amazon Web Services EMEA S.A.R.L. (“AWS”) zenye makao ya kibiashara nchini Luxembourg na kwenye Cloud Servers za Google Commerce Limited (“GCL”), kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Ireland, yenye ofisi zake katika Gordon House, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland. Hata hivyo, data hizi zinaweza kuchakatwa na wachakataji wadogo wanaofanya kazi nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya ("EEA") kulingana na makubaliano ya uchakataji wa data, mradi tu kama masharti ya ziada ya Kifungu cha 44 (na kadhalika) GDPR kuhusu uchakataji wa data binafsi katika nchi nyingine yametimizwa (k.m., ikiwa mchakataji msaidizi anaweza kutoa ulinzi sahihi chini ya Kifungu cha 46 GDPR, kama vile lakini hauishii tu kwenye vifungu vya kawaida vya ulinzi wa data, kanuni zinazoongoza makampuni, sheria za maadili zilizopitishwa au hali za kipekee chini ya Kifungu cha 49 GDPR).
Maelezo nyeti yanayotumwa kutoka kivinjari chako na Tovuti yetu hutumwa yakiwa yamesimbwa kwa kutumia Usalama wa Safu ya Kutuma (“TLS”). Wakati wa kutuma maelezo nyeti, unapaswa kuhakikisha kuwa kivinjari chako kinaweza kuthibitisha cheti chetu.
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu usalama maalum unaotumika wakati wa kutuma data zako binafsi nje ya EEA.
6. Kufichuliwa kwa data zako binafsi
6.1 Tunatumia watoa huduma za kiufundi kuendesha na kudumisha Huduma zetu, ambao hutumika kama wachakataji wetu kulingana na makubaliano ya uchakataji wa data. Orodha nzima ya wachakataji wetu wengine, wanaochakata data zako binafsi kwa niaba yetu na kwa udhibiti mkali kwa mujibu wa Sehemu ya 3 hapo juu inaweza kupatikana hapa. Watoa huduma ambao huchakata data binafsi kwa niaba yetu nje ya EEA (au “nchi nyingine”) watatumika tu ikiwa mpokeaji amepokea uamuzi wa Tume ya Ulaya kuhusu ufaafu au dhamana mwafaka au zinazofaa kwa nchi hii nyingine. Isitoshe, hatutatuma data zako binafsi kwa watu wengine - isipokuwa, ikiwa inahusu, kwa madhumuni yaliyoorodheshwa hapa chini.
-
Uhalalishaji wa matumizi: Msingi wa kisheria wa kuhamisha na mchakataji kuchakata data zako binafsi unalingana na msingi wa kisheria, ambao sisi kama wadhibiti wa data tunautegemea (sikuzote kwa kutii sehemu ya 3 hapo juu).
6.2 Ikiwa tunauza au kununua biashara au mali yoyote, tunaweza kufichua data zako binafsi kwa muuzaji mtarajiwa au mnunuzi wa biashara au mali hiyo.
-
Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR): ya kuuza biashara au mali yetu/ inapohitajika na sheria husika: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR): kwa kuchakata makundi maalum ya data, k.v., data zako binafsi za afya.
6.3 Ikiwa sisi au, kwa kiasi kikubwa, mali zetu zote zitanunuliwa na mtu mwingine, data binafsi kuhusu watumiaji wetu zitakuwa moja ya mali zitakazohamishwa.
-
Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR): kuuza Kampuni au mali zetu/ inapohitajika na sheria husika: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR): kwa kuchakata makundi maalum ya data, kv., data zako binafsi za afya.
6.4 Ikiwa tunalazimika kwa mujibu wa sheria za EU au sheria za nchi Mwanachama kufichua au kushiriki data zako binafsi.
-
Uhalalishaji wa matumizi: Wajibu wa kisheria (Kifungu cha 6 (1) (c) GDPR).
6.5 Tunaweza kufichua data fulani kwa mashirika yanayojishughulisha na majaribio ya kitiba na aina nyingine za utafiti pale mbapo umeturuhusu waziwazi kufanya hivyo.
-
Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR).
7. Ni kwa muda gani tunahifadhi data zako binafsi
Tutashikilia data zako binafsi kwa kadri itakapolazimika au hitajika na sheria au chombo chochote husika cha udhibiti, na sikuzote kwa kutii kanuni ya kupunguza ushikiliaji wa data. Vipindi maalum vya kuhifadhi kuhusiana na shughuli za uchakataji vimeelezewa kwa kina katika Sehemu ya 3 hapo juu.
Ikiwa data yako binafsi inatumiwa kwa sababu zaidi ya moja, tutaihifadhi mpaka dhumuni la kipindi kirefu zaidi likamilike, lakini tutaacha kuitumia kwa dhumuni la kipindi kifupi mara tu kipindi hicho kifupi kitakapomalizika (ili kutii kanuni ya dhumuni lenye mipaka). Tunazuia ufikiaji wa data yako binafsi kwa watu isipokuwa tu wale wanaohitaji kuitumia kwa dhumuni/madhumuni husika, sikuzote kwa kutii kanuni ya uadilifu na usiri.
Baada ya uchakataji wa data yako kutokuwa wa lazima tena kwa madhumuni yaliyoainishwa katika sehemu 3 au akaunti yako imefutwa (angalia sehemu ya 3.2), tutazitenganisha na kuzihifadhi baadhi ya data zako kwa njia salama kulingana na majukumu ya kisheria ya kubaki na data yanayotuhusu na sababu za maana za mahitaji ya biashara.
Tutabaki na data za uhasibu kwa mujibu wa majukumu ya uhifadhi wa sheria za kibiashara na kodi za miaka sita au kumi (Sheria ya Kodi ya Kijerumani § 147, Sheria ya Biashara ya Kijerumani § 257).
Tutabaki na data za Uchunguzi Baada ya Mauzo (Post-Market-Surveillance) (pamoja na data za afya) kulingana na majukumu yetu ya uhifadhi kwa mujibu wa sheria ya kifaa cha kitiba.
Tutabaki na data (pamoja na data za afya) kuhusiana na utumiaji wako wa Huduma yetu kwa miaka mitatu au kumi kulingana na mahitaji yetu ya kibiashara kwa madhumuni ya kuanzisha, kutekeleza au kujitetea dhidi ya madai ya kisheria.
Ikiwa ulikuwa mtumiaji wa huduma za UK Doctor Chat (ambazo hazipatikani tena tangu tarehe 23 Machi 2018), maelezo yako ya mashauriano yanaweza kuhifadhiwa na sisi kwa kipindi cha hadi miaka 10 kulingana na Ratiba ya Kuhifadhi ya Maadili ya Usimamizi wa Rekodi nchini Uingereza, au ikiwa inahitajika vinginevyo na Tume ya Ubora wa Huduma “CQC”).
Ikiwa uchakataji wa data yako ya binafsi hauna ulazima tena kwa dhumuni lolote, aidha inafichwa utambulisho na kutoweza kutambulika tena kwa jina (na data iliyofichwa utambulisho inaweza kuhifadhiwa) au kufutwa kwa njia salama.
8. Haki zako kuhusiana na data
Chini ya GDPR, una haki mbalimbali kuhusiana na data zako binafsi (kama ilivyoorodheshwa hapa chini).
Haki hizi zote zinaweza kutekelezwa kwa kuwasiliana nasi kupitia fomu yetu ya mawasiliano, kwa kuchagua “Natumia Haki Zangu za Data & Faragha”.
Uthibitisho: ili kuthibitisha ombi lako, tutachukua hatua za kutosha kama vile kukuomba ututumie uthibitisho kupitia barua pepe inayohusiana na akaunti yako, ili tuweze kuhakikisha kwamba wewe ndio mmiliki wa akaunti ya barua pepe hii. Ikiwa hakuna anwani ya barua pepe inayohusiana na akaunti yako, tunaweza kukuuliza uthibitisho wa Kitambulisho (ID).
- Haki ya kuondoa idhini: Ambapo uchakataji unategemea idhini yako ya hapo awali, una haki ya kuondoa idhini ya namna hiyo wakati wowote kwa kutuarifu hapa. Kwa kuondoa idhini yako, uhalali wa kuchakata maelezo kwa mujibu wa idhini ulliyotoa hadi wakati wa kujiondoa hautaathiriwa.
- Haki ya kupinga: Una haki ya kupinga chini ya masharti ya Kifungu cha 21 GDPR. Utapata maelezo zaidi hapa chini:
— Haki ya kupinga ambapo uchakataji unategemea msingi wa maslahi halali: Kama mtoaji data, una haki ya kupinga, kwa misingi inayohusiana na hali yako maalum, wakati wowote, uchakataji wa data zako binafsi kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) (e) au (f) GDPR, pamoja na kupinga kupangwa kwa maelezo kwa msingi wa vifungu hivyo. Pingamizi linalohusiana na hali yako likitokea, hatutachakata tena datazako binafsi isipokuwa kama tunaweza kuonyesha sababu mwafaka za kuchakata data ambazo zinazidi maslahi yako, haki na uhuru au ili kuanzisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria.
— Haki ya kupinga ikiwa tunachakata data yako binafsi kwa madhumuni ya kuzalisha takwimu: Ikiwa tutachakata data zako binafsi kwa sababu za kuzalisha takwimu kulingana na Kifungu cha 9 (2) (j) GDPR/ sehemu ya 27 (1) BDSG, una haki ya kupinga uchakataji kama huu kwa sababu zinazotokana na hali yako maalum. Pingamizi kama hilo likitokea, hatutachakata tena data binafsi husika kwa madhumuni haya, isipokuwa kama uchakataji ni lazima ili kutimiza jukumu la manufaa kwa jamii, au usitishaji wa uchakataji kama huo kunaweza kuzuia au kuathiri sana utekelezaji wa madhumuni ya kitakwimu na kuendeleza uchakataji kunahitajika ili kutimiza madhumuni ya kitakwimu.
— Haki ya kuping ambapo tunachakata data zako binafsi kwa madhumuni ya afya ya jamii: Ikiwa tunachakata data zako binafsi kwa madhumuni ya afya ya jamii kwa mujibu wa Kifungu cha 9 (2)(i)GDPR, / sehemu ya 22 (1)(1)(c) BDSG, una haki ya kupinga uchakataji kama huu kwa sababu zinazotokana na hali yako maalum. Pingamizi kama hilo likitokea, hatutachakata tena data binafsi husika kwa madhumuni haya, isipokuwa kama uchakataji ni lazima ili kutimiza jukumu la manufaa kwa jamii, au usitishaji wa uchakataji kama huo kunaweza kuzuia au kuathiri sana utekelezaji wa madhumuni ya afya ya jamii na kuendeleza uchakataji kunahitajika ili kutimiza madhumuni ya afya ya jamii.
— Haki ya kupinga matangazo ya moja kwa moja: Pale data zako binafsi zitachakatwa kwa madhumuni ya matangazo ya moja kwa moja, una haki ya kupinga wakati wowote uchakataji wa data zako binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya aina hiyo, ikijumuisha kupanga maelezo kwa kiwango ambacho kinahusiana na matangazo ya moja kwa moja ya aina hiyo. Ikiwa utapinga uchakataji kwa madhumuni ya matangazo ya moja kwa moja, hatutochakata tena data zako binafsi kwa madhumuni haya. Ili kutumia haki zako za pingamizi, unaweza kujibu kwa barua pepe kwa barua pepe ya matangazo ya moja kwa moja unayopokea kutoka kwetu, au kwa kuwasiliana nasi wakati wowote kupitia hapa. - Haki ya kufahamishwa: Kama mtoaji data, una haki ya kufikia data na kupata maelezo kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 15 GDPR. Hii inamaanisha hasa kwamba una haki ya kupata uthibitisho kutoka kwetu kuhusu ikiwa tunachakata data zako binafsi au sio. Ikiwa ni hivyo, pia una haki ya kuwezeshwa kufikia data binafsi na maelezo yaliyoorodheshwa katika kifungu cha 15 (1) GDPR. Hii inajumuisha maelezo kuhusu madhumuni ya uchakataji, aina za data binafsi ambazo zinachakatwa, pamoja na wapokeaji au aina za wapokeaji ambao wamepewa au watapewa data binafsi.
- Haki ya kufuta / 'Haki ya kusahaulika': Kama mtoaji data, una haki ya kufuta ("haki ya kusahaulika") chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 17 GDPR. Hii inamaanisha kwamba kwa ujumla una haki ya kupata kutoka kwetu ufutwaji wa data yako binafsi na tunawajibika kufuta data zako binafsi bila kukawia pasipo sababu wakati sababu moja iliyoorodheshwa katika kifungu cha 17 (1) GDPR inahusika. Unaweza kufanya hivyo kwa kufuta akaunti yako, kwenye App, wakati wowote. Ikiwa tumeweka data binafsi hadharani na tunawajibika kuifuta, tunawajibika pia, kwa kuzingatia teknolojia iliyopo na gharama ya utekelezaji, kuchukua hatua stahiki, ikijumuisha hatua za kiufundi, kuwataarifu wadhibiti wanaochakata data binafsi ambazo umeomba wadhibiti hao wafute viungo vyovyote vya maelezo, au kunakili au kurudufisha data hizo binafsi (Kifungu cha 17 (2) cha GDPR. Isipokuwa, haki ya kufuta (“Haki ya kusahaulika”) haitekelezeki ikiwa uchakataji ni lazima kwa moja ya sababu zilizoorodheshwa katika Kifungu cha 17 (3) GDPR. Hii inaweza kuwa hivyo, kwa mfano, ikiwa uchakataji ni lazima katika kutimiza wajibu wa kisheria au kuanzisha, kutumia, au kutetea madai ya kisheria (Kifungu cha 17 (3) (b) na (e) GDPR).
- Haki ya kuzuia uchakataji: Kama mtoaji data, una haki ya kuzuia uchakataji kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 18 GDPR. Hii inamaanisha kuwa una haki ya kupata kutoka kwetu uzuiaji wa uchakataji wakati sababu moja iliyoorodheshwa katika kifungu cha 18 (1) GDPR inahusika. Hili linaweza kutokea, kwa mfano, ikiwa unapinga usahihi wa data binafsi. Katika hali kama hiyo, hatua ya kuzuia uchakataji hudumu kwa kipindi ambacho kinatuwezesha kuthibitisha usahihi wa data binafsi (Kifungu cha 18 (1) (a) GDPR). Kuzuia kunamaanisha kuwa data binafsi zilizohifadhiwa huwekwa alama kwa lengo la kuzuia uchakataji wake wa baadaye (Kifungu cha 4 (3) GDPR).
- Haki ya kuhamisha data: Kama mtoaji data, una haki ya kuhamisha data kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 20 GDPR. Hii inamaanisha kuwa kwa ujumla una haki ya kupokea data zako binafsi ambazo umetupatia katika muundo, unaotumika kwa kawaida, na unaosomeka na kompyuta na kuzipeleka data hizo kwa mdhibiti mwingine bila kipingamizi kutoka kwetu ambapo msingi wa uchakataji ni idhini kwa (mujibu wa Kifungu cha 6 (1) (a) au Kifungu cha 9 (2)(a) GDPR au kwa mkataba kwa (mujibu wa Kifungu cha 6 (1)(b) GDPR), na ambapo uchakataji unafanyika kwa njia za kiotomatiki (kwa kompyuta) (Kifungu cha 20 (1) GDPR). Katika kutumia haki yako ya kuhamisha data, pia una haki kwa ujumla ya kutaka data zako binafsi kuhamishwa moja kwa moja kutoka kwetu kwenda kwa mdhibiti mwingine ambapo inawezekana kiufundi (Kifungu cha 20 (2) GDPR).
- Haki ya Marekebisho: Kama mtoaji data, una haki ya kurekebisha maelezo chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 16 GDPR. Hii inamaanisha hasa kwamba una haki ya kupokea kutoka kwetu, bila kuchelewa, marekebisho ya makosa katika data zako binafsi na kukamilishwa kwa data binafsi ambazo hazikukamilika.
- Haki ya kulalamika: Kama mtoaji data, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 77 GDPR. Mamlaka ya usimamizi inayohusika na masuala yetu ni Mamlaka ya Ulinzi wa Maelezo ya Berlin nchini Ujerumani (Berliner Beauftragte für Datenschutz und Informationsfreiheit, Anwani: Friedrichstr. 219, 10969 Berlin; Simu: 030 13889-0; Barua-pepe: [email protected]).
Kutuomba tuache kuchakata data zako binafsi au kufuta data zako binafsi itaelekea kumaanisha kama hauwezi tena kutumia Huduma zetu, au angalau hautoweza kutumia sehemu za Huduma ambazo zinahitaji uchakataji wa aina za data binafsi ambazo umetuomba tufute, hatua ambayo inaweza kusababisha usiweze kutumia tena Huduma.
9. Taarifa ya Faragha kwa wakazi wa California
Ikiwa wewe ni mkazi wa California (kama ilivyoainishwa katika sehemu ya 17014 ya Mada ya 18 ya Kanuni za Usimamizi za California), Sheria ya California inatulazimu kukupatia maelezo kadhaa ya ziada kuhusiana na haki zako kwa kuzingatia “maelezo yako binafsi” (kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Faragha ya Mtumiaji (hapa itafahamika baadaye kama “CCPA”) ambayo imeanza kutekelezwa Januari 1, 2020).
Hatukuuza au kuhamisha data zako binafsi kwa watu wengine katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, hatufanyi hivyo sasa, na hatutofanya hivyo baadaye (na hatutofanya hivyo kamwe bila kukupatia haki ya kukataa).
Tunaweza kuhamisha data zako binafsi kwa wachakataji wengine ili kufanikisha madhumuni ya uchakataji yaliyoorodheshwa katika Sehemu ya 3 hapo juu, lakini tutafanya hivyo kwa kushirikiana na wachakataji wengine embao tuna makubaliano nao ya ulinzi wa data. Orodha kamili ya wachakataji wetu wengine inaweza kupatikana hapa [a list of processors].
CCPA inawapa watumiaji wa California haki zifuatazo (ambapo haiingiliani na GDPR):
- Haki ya kuomba kufichua taarifa yoyote binafsi tuliyokusanya (Kifungu cha (1789.100) (a) CCPA). Hii inamaanisha kwa ujumla kwamba unayo haki ya kuomba kufichuliwa kwa aina ya taarifa binafsi tuliyokusanya kutoka kwako, pamoja na aina ya vyanzo vilivyotumika kupata taarifa hiyo, dhumuni la ukusanyaji, aina ya watu wengine ambao tumeshirikisha kwenye taarifa yako binafsi, na vipande maalum vya taarifa binafsi ambayo tumekusanya (Kifungu cha 1798.110 (a) CCPA).
- Haki ya kuomba kufutwa kwa taarifa yoyote binafsi ambayo tulikusanya kutoka kwako (Kifungu cha 1798.105) CCPA). Hii inamaanisha kwamba baada ya kuthibitisha ombi lako la kutaka kufuta taarifa yako binafsi, tutaifuta taarifa hiyo kutoka kwenye rekodi zetu na kumuelekeza mtoa huduma wa moja kwa moja yoyote kufuta taarifa yako binafsi kutoka kwenye rekodi zao, isipokuwa wakati Kifungu cha 1798.105 (d) CCPA kinahusika (kwa mfano, taarifa binafsi ni ya lazima ili kutoa huduma, kubaini matukio ya kiusalama, kubaini na kukarabati makosa ambayo yanaharibu utendaji uliokusudiwa wa Huduma, kufanya utafiti wa takwimu kwa maslahi ya jamii, au kutimiza wajibu wa kisheria).
Pamoja na uwezekano wa kuwasiliana nasi kwa kutumia fomu yetu ya mawasiliano kwa kuchagua “Natumia Haki Zangu za Data & Faragha,” unaweza kutumia haki zozote chini ya CCPA au kuomba maelezo zaidi kuhusiana na haki zako kwa kutupigia simu kupitia namba ya dharura.
10. Taarifa kuhusu Faragha kwa wakaazi wa Brazili
Ikiwa wewe ni mkazi wa Brazili, sheria ya Brazili inatutaka tukupe taarifa zingine za ziada kuhusu haki zako kuhusiana na "taarifa zako binafsi" (kama ilivyofafanuliwa kwenye "Lei Geral de Proteção de Dados” (hapa itafahamika kama "LGPD") kwamba ilianza kutumika mnamo Septemba 18, 2020).
Ili kufahamu ni aina gani za taarifa zako binafsi zinachakatwa na kwa madhumuni gani, unaweza kusoma sehemu ya 3 yenye kichwa cha taarifa "Ni data gani binafsi tunaweza kukusanya na kuchakata, kwanini na kwa muda gani" ndani ya hati hii.
Tunaweza kuchakata maelezo yako binafsi ikiwa tu tuna msingi wa kisheria wa uchakataji kama huo. Misingi ya kisheria ni kama ifuatavyo:
- idhini yako kwenye masuala ya uchakataji husika;
- ulinzi au usalama wa mwili wako wewe au mtu mwingine;
- kutii jukumu la kisheria au kiudhibiti ambalo tunalo;
- utekelezaji wa sera za jamii zilizotolewa katika sheria au kanuni au kwa mujibu wa mikataba, makubaliano na nyenzo nyingine za kisheria zinazofanana na hizo;
- tafiti zilizofanywa na vyombo vya utafiti, ikiwezekana tafiti zilizofanywa kwenye taarifa binafsi zilizofichwa utambulisho (anonymous);
- utekelezaji wa mkataba na taratibu zake za awali, katika hali ambazo wewe ni mshiriki katika mkataba husika;
- kutumia haki zetu katika taratibu za kimahakama, kiutawala au kisuluhishi;
- ulinzi wa afya - katika taratibu zinazofanywa na vyombo vya afya au wataalamu;
- masilahi yetu halali, ilimradi haki zako za msingi na uhuru wako visishinde masilahi ya aina hiyo;
10.1 Haki zako za faragha za Brazili
Una haki ya:
- kupata uthibitisho wa uwepo wa shughuli za uchakataji kwenye taarifa zako binafsi;
- kuweza kupata taarifa zako binafsi;
- kuwezesha marekebisho ya taarifa binafsi zisizo kamili, zisizo sahihi au za zamani;
- kuzuia utambulisho na upatikanaji wa taarifa zako binafsi au ondoa taarifa zako binafsi zisizo za lazima au zilizopita kiasi au taarifa binafsi ambayo haichakatwi kwa kutii LGPD;
- kupata taarifa juu ya uwezekano wa kutoa au kukataa kutoa idhini yako na athari zinazohusiana na uamuzi huo;
- kupata taarifa juu ya watu wengine ambao tunawashirikisha kwenye taarifa zako binafsi;
- kupata, unapoomba, uhamishaji wa taarifa zako binafsi (isipokuwa kwa taarifa zisizo na utambulisho) kwenda kwa mtoa huduma au bidhaa mwingine, mradi tu siri zetu za kibiashara na kitasnia zinalindwa;
- kupata ufutwaji wa taarifa zako binafsi zinazochakatuliwa ikiwa uchakataji ulitokana na idhini yako, isipokuwa moja au zaidi ya masuala ya kipekee yaliyotolewa kwenye kifungu cha 16 cha LGPD yanahusika;
- batilisha idhini yako wakati wowote;
- kuwasilisha malalamiko yanayohusiana na taarifa zako binafsi kwa ANPD (the National Data Protection Authority) au kwa vyombo vya ulinzi wa wateja;
- kupinga shughuli ya uchakataji katika hali ambazo uchakataji haufanyiki kwa kufuata masharti ya sheria;
- kuomba taarifa za wazi na za kutosha kuhusiana na vigezo na taratibu zinazotumika kwa uamuzi wa kiotomatiki; na
- kuomba uhakiki wa maamuzi yaliyofanyika kupitia tu msingi wa uchakataji wa kiotomatiki wa taarifa zako binafsi, ambao unaathiri masilahi yako. Haya ni pamoja na maamuzi ya kufafanua maelezo yako binafsi, ya kitaalam, maelezo mafupi ya utumiaji na ukopaji (consumer and credit profile), au vipengele vya utu wako.
Kamwe hutabaguliwa, au vinginevyo utopata hasara yoyote, ikiwa utatumia haki zako.
10.2 Jinsi ya kufungua ombi lako
Unaweza kuwasilisha ombi lako la kutumia haki zako bila malipo yoyote, wakati wowote, kwa kutumia maelezo ya mawasiliano yaliyotolewa kwenye hati hii (k.m., barua pepe kwa [email protected]), au kupitia mwakilishi wako wa kisheria.
10.3 Namna gani na lini tutajibu ombi lako
Tutajitahidi kujibu haraka maombi yako.
Katika hali yoyote, ikiwa haitowezekana kwetu kufanya hivyo, tutahakikisha tunakufahamisha sababu za uhalisia au kisheria zinazotuzuia kutii maombi yako mara moja, au vinginevyo kutotii kabisa. Katika hali ambazo hatuchakati taarifa zako binafsi, tutakufahamisha kuhusu mtu husika au mwenye mamlaka ya kisheria ambaye unapaswa kuelekeza maombi yako, ikiwa tunaweza kufanya hivyo.
Iwapo utatuma ombi la kupata taarifa za uthibitisho wa uchakataji wa taarifa zako binafsi, tafadhali hakikisha kwamba unabainisha ikiwa ungependa taarifa zako binafsi zitolewa kwa njia ya kieletroniki au kwa njia ya chapisho.
Utahitaji pia kutujulisha ikiwa unataka tujibu ombi lako mara moja, ambapo katika hali hiyo tutajibu kwa namna iliyorahisishwa (kwa ufupi), au ikiwa badala yake unahitaji taarifa kamili.
Ikiwa unataka taarifa kamili, tutajibu ndani ya siku 15 kuanzia wakati uliotoa ombi lako, tukikupatia taarifa zote kuhusu chanzo cha taarifa zako binafsi, uthibitisho wa ikiwa rekodi zipo au hazipo, vigezo vyovyote vinavyotumika kwenye uchakataji na malengo ya uchakataji, wakati huo huo tukiwa tunalinda siri zetu za kibiashara na kitasnia.
Iwapo utaomba urekebishaji, ufutaji, kutotambulika au kutoa ombi la kuzuia taarifa binafsi, tutahakikisha tunawasiliana mara moja na wahusika wengine tulioshiriki nao taarifa zako binafsi ili kuwawezesha pia kutekeleza ombi lako - isipokuwa katika hali ambapo mawasiliano kama hayo yamethibitishwa kutowezekana au yanajumuisha juhudi kubwa kwa upande wetu.
10.4 Uhamisho wa taarifa binafsi nje ya Brazili unaoruhusiwa na sheria
Kwakuwa Ada iko nchini Ujerumani, tunahamisha tu data ikiwemo data zinazohusiana na afya kwenda Ujerumani ili kutoa huduma zetu. Pia Ada inatumia huduma za watoa huduma wengine zilizoainishwa katika kifungu cha 3 kuhamisha data kwenda nchi nyingine.
Tunaruhusiwa kuhamisha taarifa zako binafsi nje ya eneo la Brazili katika hali zifuatazo:
- wakati uhamishaji ni lazima kwa ushirikiano wa kisheria wa kimataifa kati ya vyombo vya ujasusi vya umma, uchunguzi na mashtaka, kwa mujibu wa njia za kisheria zinazotolewa na sheria ya kimataifa;
- wakati uhamisho ni lazima ili kulinda maisha yako au usalama wako wa kimwili au wa watu wengine;
- wakati uhamishaji umeidhinishwa na ANPD;
- wakati uhamishaji unatokana na ahadi iliyofanywa katika makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa;
- wakati uhamishaji ni lazima kwa utekelezaji wa sera ya umma au matakwa ya kisheria ya utumishi wa umma;
- wakati uhamishaji ni lazima katika kutii wajibu wa kisheria au wa kiudhibiti, kutekeleza mkataba au taratibu za awali zinazohusiana na mkataba, au utekelezaji wa haki za kawaida katika taratibu za kimahakama, kiutawala au kiusuluhishi.
11. Mabadiliko kwenye sera hii
Mabadiliko yoyote ambayo tutafanya kwa Sera yetu ya Faragha katika siku zijazo yatachapishwa kwenye ukurasa huu, na inapofaa, utafahamishwa kwa barua pepe au taarifa kupitia App, au kwa njia zozote nyingine zilizopo. Kwa hivyo tunakuhimiza uisome mara kwa mara ili uendelee kupata maelezo kuhusu namna tunavyochakata data zako.