Timu yetu ya uongozi
Daniel Nathrath
Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mtendaji Mkuu
Daniel anaongoza kwa ujumla mafanikio ya kampuni ya Ada kwa kuendeleza na kusambaza mkakati wake wa muda mrefu kwa ushirikiano wa karibu na timu ya uongozi. Daniel ana uzoefu wa karibia miaka 20 akiongoza mapambano ya kuleta teknolojia badilishi kwenye sekta mpya za biashara. Katika maisha yake ya kikazi, ameanzisha na kuongoza biashara kadhaa za wavuti nchini Denmark, Ujerumani, Marekani na Uingereza. Baada ya kusoma sheria kama mdhaminiwa wa Fulbright katika chuo cha Houston, alihitimu Shahada ya Uzamili ya Biashara (MBA) katika chuo cha Chicago. Baadae alifanya kazi Boston Consulting Group kabla ya kuanza safari yake ya ujasiriamali.
Dk. Claire Novorol
Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mkuu wa Masuala ya Kitiba
Claire ni daktari. Alifanya kazi kama daktari wa watoto jijini London kabla ya kubobea katika jenetikia. Amehitimu Shahada mbili, yaani ya Patholojia na ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Bristol, na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Mfumo wa Neva kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, nchini Uingereza. Claire anasimamia ubora wa kitiba pamoja na timu zetu za kitiba. Anawakilisha sauti za wagonjwa na wataalamu wa huduma za afya ili kuhakikisha bidhaa zetu zinakidhi mahitaji yao.
Prof. Dk. Martin Hirsch
Mwanzilishi-mwenza & Mshauri Mkuu wa Masuala ya Kisayansi
Martin ana Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Mfumo wa Neva na diploma katika Fiziolojia. Martin ni mtafiti wa masuala ya kitiba aliyegeuka kuwa mjasiriamali, na alihama kutoka nadharia hadi uvumbuzi baada ya kuchapisha kazi yake kuhusu miundo mfano ya neva (nerve modeling) katika Jarida la Kisayansi la Nature. Ubia wake wa kwanza ulikuwa kwenye mpango wa uundaji wa neva ambao uliokoa maelfu ya wanyama kutoka kwenye jaribio la maabara. Alitengeneza toleo la kwanza la Ada kwa ajili ya madaktari na anaendelea kutoa mwelekeo wa namna Ada inavyojifunza leo. Martin ni mjukuu wa Werner Heisenberg, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobeli.
Vanessa Lemarié
Afisa Mkuu wa Utekelezaji
Vanessa anahakikisha mashirikiano yetu yanakuwa na manufaa makubwa kwa washirika wetu na watumiaji wa huduma zao kupitia AI ya kitiba ya Ada. Kabla ya kujiunga na Ada, aliongoza timu za masoko na biashara kwenye kampuni ya Bayer kwa miaka 15. “Tunashirikiana na kampuni zenye ubunifu zaidi katika tasnia yetu. Lengo letu ni kuwezesha utambuzi wa mapema na sahihi zaidi wa magonjwa na uaguzi huku tukifanikisha uendelevu wa kibiashara.”
Graham French
Chief Technology Officer and SVP Engineering
Graham anaongoza mkakati na utekelezaji wa timu ya teknolojia ya Ada. Graham ni kiongozi mtendaji wa masuala ya teknolojia mwenye uzoefu wa miaka 25 unaojumuisha teknolojia mbalimbali, ikiwemo uchakataji wa lugha halisi, grafu za maarifa, biashara, na miundombinu ya wasanidi programu. Kabla ya kujiunga na kampuni ya Ada, ana uzoefu wa miaka 10 wa kufanya kazi kampuni ya Amazon na Meta katika majukumu ya juu ya kiungozi. Katika majukumu yake hayo alianzisha Kituo cha Maendeleo cha Amazon huko Cambridge (UK) ili kuunda na kuzindua uwezo wa teknolojia ya Alexa.
Ewelina Türk
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Bidhaa ya Kitiba
Ewelina anaongoza idara yetu ya msingi wa teknolojia inayotoa maarifa ya kitiba ya Ada. Amesomea udaktari katika chuo cha tiba cha Charité, Berlin, akiweka maslahi zaidi kwenye magonjwa ya watoto, haswa huduma za dharura na kinga. Pamoja na majukumu yake ya kikazi kwetu, Ewelina anamalizia Shahada ya Uzamivu katika Magonjwa ya Baridi Yabisi kwa watoto. “Ninasaidia timu zetu kuunda AI ya kitiba bora kabisa duniani."
Marvin Rottenberg
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Soko la Watumiaji
Kabla ya Ada, Marvin alifanya kazi Google na alijikita kwenye utendaji & bidhaa sokoni ambapo alifanya mashauriano na makampuni na mashirika ya kimataifa kuhusu mikakati ya ukuaji kidijitali. Anaongoza timu zetu za masoko na anawajibu wa kuthaminisha bidhaa kwa watumiaji ili kukusanya mapato (monetization) na kusimamia mashirikiano yanayolenga kutoa huduma kwa watumiaji. "Watu bilioni 3 wanashindwa kupata huduma muhimu za afya. Nakata Ada ipunguze hiyo namba mpaka 0."
Henry Hoffmann
Mkurugenzi wa Utafiti
Henry ameongoza ukuzaji wa teknolojia ya msingi ya Ada, anakuza mahesabu ya Akili Bandia (AI), mifano ya lugha bandia, na njia mpya za uwakilishi wa maarifa. Akiwa kama Mkurugenzi wa Timu ya Utafiti ya Ada, anaongoza ukuzaji wa teknolojia ya baadaye ya Ada. “Kwangu mimi, daima ni kuhusu hatua inayofuata - kuendelea kusonga mbele na kwenda ambapo hamna aliyewahi kabla kwenda.”
Hila Azadzoy
Mkurugenzi Mtendaji, Global Health Initiative
Hila anaongoza Mpango wetu wa Afya Duniani (Global Health Initiative) ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwenye nchi zisizo na rasilimali za kutosha. Kabla ya Ada, Hila alikuwa ni mmoja wa waanzilishi na Mkuu wa Taaluma wa Chuo Huria cha Kiron. Ni mnufaika wa Tuzo ya Digital Female Leader, mwanachama wa MIT Solve, na mzungumzaji hodari wa hadhara (TEDx, Clinton Global Initiative, UNESCO NGO Forum). “Nimejitolea kutumia teknolojia kwa manufaa ya jamii.”
Daniel Nathrath
Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mtendaji Mkuu
Dk. Claire Novorol
Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mkuu wa Masuala ya Kitiba
Prof. Dk. Martin Hirsch
Mwanzilishi-mwenza & Mshauri Mkuu wa Masuala ya Kisayansi
Vanessa Lemarié
Afisa Mkuu wa Utekelezaji
Graham French
Chief Technology Officer and SVP Engineering
Ewelina Türk
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Bidhaa ya Kitiba
Marvin Rottenberg
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Soko la Watumiaji
Henry Hoffmann
Mkurugenzi wa Utafiti
Hila Azadzoy
Mkurugenzi Mtendaji, Global Health Initiative