Sera ya Kidakuzi ya Ada Health GmbH
Ilibadilishwa mwisho: 23 Juni 2022
Ada Health GmbH (“Ada”, “sisi”, au “yetu”) inatumia vidakuzi na vifaa vinavyofanana na hivyo katika tovuti yake ya ada.com (“Tovuti”) ili kusaidia kukupatia Tovuti , rafiki, rahisi kutumia, salama na yenye ufanisi. Sera hii inaeleza namna tunavyofanya hivyo.
Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya ufuatiliaji wakati wowote kupitia .
1. Maelezo ya jumla kuhusu vidakuzi
Vidakuzi ni faili ndogo za maandishi ambazo tovuti inaweza kuhifadhi katika kifaa chako unapoitembelea kwa mara ya kwanza. Kidakuzi husaidia tovuti kutambua kifaa chako unapoitembelea mara nyingine. Tunatumia neno “vidakuzi” katika sera hii kumaanisha faili zote zinazokusanya maelezo kwa njia hii.
Kuna kazi nyingi vidakuzi hutekeleza. Kwa mfano, vinaweza kutusaidia kukumbuka jina lako la mtumiaji na vitu unavyopendelea, kuchanganua ubora wa utendaji kazi wa tovuti, au hata kuturuhusu kupendekeza maudhui tunayoamini yatakufaa zaidi.
2. Tovuti hii hutumia aina gani ya vidakuzi?
Kwa jumla, vidakuzi vyetu hutekeleza angalau mojawapo wa ya kazi zifuatazo:
- Lazima. Vidakuzi vya lazima ni muhimu ili kukupatia Huduma zetu. Vinawezesha kazi za msingi kama vile kuvinjari kwenye ukurasa na kufikia sehemu salama za Huduma.
| Jina | Mtoa huduma | Dhumuni | Mwisho | Aina |
|---|---|---|---|---|
| cookie_settings | ada.com | Huwezesha tovuti kuhifadhi maamuzi ya watumiaji kuhusu matumizi ya vidakuzi katika tovuti. | Siku 365 | HTTP Cookie |
| locale_redirected | ada.com | Huwezesha tovuti kutambua kama mtumiaji ameshaelekezwa kwenye lugha yake ili kuzuia uelekezaji mwingine wa moja kwa moja. | Siku 365 | HTTP Cookie |
| recent_help_articles | ada.com | Huwezesha tovuti kuhifadhi makala 5 za mwisho zilizopitiwa ili kurahisisha matumizi ya mtembeleaji wa tovuti. Taarifa hii inahifadhiwa na kutumika tu kwenye kifaa. | Siku 365 | HTTP Cookie |
- Masoko. Vidakuzi vya masoko hutumika kufuatilia watembeleaji wa tovuti na maeneo wanayobofya wakiwa kwenye tovuti. Kusudi lake ni kuwa na matangazo yenye walengwa na kupima ufanisi wa kampeni zetu.
Tovuti hii haitumii vidakuzi vyovyote vya masoko kwa wakati huu.
3. Vifaa vya watoa huduma wengine vinavyotumika katika Tovuti yetu
Tunatumia au kuruhusu mtoa huduma mwingine afuataye kutumia vidakuzi ambavyo vipo katika makundi yaliyoainishwa hapo juu:
4. Haki ya kukataa
Zaidi ya haki yako ya kukataa kwa mujibu wa Kifungu cha 21 GDPR, unaweza kukataa kukusanywa na kuchakatwa kwa maelezo ya ufuatiliaji kwa kufuata maagizo ya kujiondoa ya mtoa huduma husika kama ilivyoelezwa hapo juu.
Aidha, ikiwa ungependa kuzima vidakuzi basi unaweza kufanya hivyo kwa kubadilisha mipangilio katika kivinjari au simu yako ya mkononi. Tafadhali kumbuka kuwa iwapo utachagua kuzima vidakuzi, unaweza kukuta kwamba vipengele fulani vya tovuti haviyafanyi kazi vizuri.
Kwa maelezo zaidi kuhusu haki zako chini ya Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data na namna tunavyochakata data katika huduma zetu, rejea Sera yetu ya Faragha.