Ubora wa kitiba unaohimili uchunguzi

Kampuni zote za teknolojia ya afya zinatetea aina zao bora zaidi za masuluhisho. 

Tafiti isiyo na upendeleo, mapitio ya wataalamu na kuchapishwa na jumuiya ya kisayansi, husaidia watu kutofautisha kati ya madai na ushahidi wa kitiba ili kuamua wao wenyewe. 

Uwekaji alama teule (benchmarking) kwenye tasnia huruhusu kampuni za afya kushindana. Uchunguzi wa kisayansi huwaruhusu kuongoza.

Tafiti zilizopitiwa na wataalamu wengine na machapisho kwa kushirikiana na Ada

 • Matumizi ya wagonjwa na mtazamo wa teknolojia ya tathmini ya dalili na ushauri inayoendeshwa na akili bandia katika chumba cha kusubiria huduma ya msingi Uingereza: Utafiti wa majaribio ya uchunguzi.
  JMIR Hum Factors (2020) doi: 10.2196/19713.

  Miller, S., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa majaribio ya uchunguzi
  Matokeo
  • Ada ilifanya vizuri kwenye utafiti wa wagonjwa 523 katika mpangilio wa huduma ya msingi.
  • Ada ilikadiriwa kuwa rahisi au rahisi sana kutumia kwa asilimia 97.8 ya washiriki.
  • Kwa ushauri wa Ada, asilimia 12.8 ya washiriki wangetumia huduma ya kiwango cha chini au wangechelewesha miadi yao.
 • Magonjwa adimu 2030: Namna AI iliyoboreshwa itasaidia utambuzi na matibabu ya magonjwa adimu katika siku zijazo.
  Ann. Rheum. Dis. (2020) doi: 10.1136/annrheumdis-2020-217125.

  Hirsch, M. C., et al.

  Aina ya chapishoMtazamo wa siku za baadaye
  Matokeo
  • Katika miaka kumi ijayo, wataalamu wanaweza kufanya kazi kwa karibu na vifaa kama Ada ili kurahisisha hatua za huduma ya magonjwa adimu.
  • Ada inaweza kusaidia kutambua magonjwa ya kinga nafsia ya kurithi kama vile homa ya mediterania ya kurithi.
  • Chatiroboti huuliza dalili za tahadhari ili kutenga dharura.
 • Je, mfumo wa msaada wa uamuzi unaweza kuharakisha utambuzi wa ugonjwa adimu? Kutathmini uwezekano wa athari ya utambuzi wa magonjwa (DX) wa Ada katika utafiti wa kutazama matukio ya nyuma.
  Orphanet J Rare Dis (2019) doi: 10.1186/s13023-019-1040-6.

  Ronicke, S. et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kutazama matukio ya nyuma ya wagonjwa-halisi
  Matokeo
  • Pendekezo la juu la Ada lililingana na utambuzi uliothibitishwa katika kesi 89.25% (kesi 83 kati ya 93).
  • Katika zaidi ya kesi 56%, Ada ilitoa madokezo sahihi ya ugonjwa mapema kuliko wakati wa utambuzi wa kitiba.
  • Zaidi ya 33% ya wagonjwa wangeweza kutambuliwa kuwa na ugonjwa adimu katika ziara ya kwanza ya kitiba iliyoandikishwa.

Mabango ya mkutano na machapisho ya awali ya tafiti, yaliyofanywa na au kwa kushirikiana na Ada, yaliyowasilishwa kwa ukaguzi wa wataalamu

 • Je, app za tathmini ya dalili za kidijitali ni sahihi kivipi katika kupendekeza magonjwa na ushauri wa dharura?: Kesi za kitiba kulinganisha na madaktari (GPs).
  medRxiv (2020) doi: 10.1101/2020.05.07.20093872.

  Gilbert, S. et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Ada iliwashinda washindani wake, kwa kutoa ushauri salama asilimia 97 ya wakati na asilimia 99 ya ugonjwa.
  • Ada ilipata usahihi wa asilimia 70 katika tatu bora ya maoni yanayofaa. Mshindani wa karibu alipata usahihi wa asilimia 43, na wastani wa washindani kwa ujumla ulikuwa asilimia 38.
 • Ufahamu wa ufuatiliaji wa ugonjwa kutoka kwenye app ya tathmini ya dalili kabla na wakati wa ukabilianaji wa COVID-19 Ujerumani na Uingereza: Matokeo kutoka kwa urudiaji wa changanuzi wakilishi.
  medRxiv (2020) doi: 10.1101/2020.06.16.20126466.

  Mehl, A., et al.

  Aina ya chapishoUchanganuzi wa maelezo linganishwa
  Matokeo
  • Ada inaweza kuwa kama mfumo wa ufuatiliaji wa muda halisi wa ugonjwa ambao huzalisha ufahamu mpya wa afya.
  • Ada inaweza kusaidia kuwezesha uelewa wa athari za sera za afya ya jamii kama zuio la watu kutembea wakati wa kukabiliana na COVID-19. 
  • Ada inaweza kusaidia kutimiza na kudhibiti nadharia tete (hypotheses) kutokana na data zilizokusanywa kupitia njia za kawaida zaidi.
 • Uwezekano wa kurekodi dalili za mgonjwa wa kidijitali kupitia programu za tathmini ya dalili ili kuboresha utoaji huduma kwa mgonjwa na kupunguza nyakati za kusubiri katika Vituo vya Huduma ya Dharura: utafiti wa kuiga.
  medRxiv (2020) doi: 10.1101/2020.06.19.20135590.

  Montazeri, M., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa hali bandia (simulation)
  Matokeo
  • Ada inaweza kupunguza wastani wa muda wa mgonjwa kusubiri kumuona muuguzi wa kutathmini dharura ya tiba (triage) kwa asilimia 54.
  • Kupunguza muda wa kumuona muuguzi wa kutathmini dharura ya tiba kunaweza kuwa na athari chanya kwa mgonjwa na mhudumu wa afya na kuboresha ubora wa huduma.
 • Je, magonjwa adimu ni adimu namna gani kwa Ada, kikagua dalili cha kitiba?
  Matokeo
  • Magonjwa adimu yalikuwa pendekezo linalofaa la Ada katika asilimia 4 ya tathmini za watumiaji milioni 15, kulingana na viwango vya makadirio ya idadi ya watu kwa ujumla. 
  • Magonjwa adimu yalionekana katika mapendekezo matano bora ya Ada katika asilimia 17 ya tathmini.
  • Ada inaweza kupunguza hatua ndefu za utambuzi wa watu wanaoishi na magonjwa adimu.

Tafiti zilizopitiwa na wataalamu na matoleo ya awali katika machapisho ya watafiti wengine ambayo yanachanganua au kujadili Ada

 • Tafiti yenye msimamo wa tume juu ya uchunguzi wa kidijitali wa magonjwa ya baridi yabisi wa Jumuiya ya Magonjwa ya Baridi Yabisi Ujerumani: Majukumu, malengo, na mitazamo ya utafiti wa kisasa wa magonjwa ya baridi yabisi.
  Zeitschrift für Rheumatologie (2020) doi: 10.1007/s00393-020-00834-y.

  Knitza, J., Callhoff, J., Chehab, G., Hueber, A., Kiltz, U., Kleyer, A., Krusche, M., Simon, D., Specker, C., Schneider, M., Voormann, A., Welcker, M., & Richter, J. G.

  Aina ya chapishoTafiti yenye msimamo
  Matokeo
  • Ada ilithibitishwa kama kifaa cha tathmini ya dalili chenye taaluma mchanganyiko ambayo inaunda orodha za mapendekezo ya ugonjwa.
  • Ada ilitoa ushauri juu ya kiwango cha udharura na mahali mwafaka kupata huduma.
 • Usahihi wa vikaguzi vya dalili vya mtandaoni na uwezekano wa athari kwenye matumizi ya huduma.
  medRxiv (2020) doi: 10.1101/2020.07.07.20147975.

  Ceney, A., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Ada ilipata usahihi wa asilimia 73 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 38 wa app zote. 
  • Usahihi wa mapendekezo matano ya juu ya Ada ulikuwa asilimia 84 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 51 wa app zote.
  • Ada ilikuwa na mwelekeo wa usalama kwa asilimia 97 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 83 wa app zote.
 • Changamoto za kimaadili na kisheria za huduma za afya zinazoendeshwa na akili bandia.
  Artificial Intelligence in Healthcare(2020) doi: 10.1016/B978-0-12-818438-7.00012-5.

  Gerke, S., Minssen, T., & Cohen, G.

  Aina ya chapishoSura/ Mlango wa kitabu
  Matokeo
  • Ada ni mfano muhimu wa programu ya afya inayoendeshwa na AI iliyoundwa katika mpangilio wa uthibiti wa Kiulaya.
  • Ada ilitambuliwa kama kifaa cha kitiba chenye nembo ya CE (Kifaa cha Kitiba daraja la kwanza chini ya Maagizo ya Kifaa cha Kitiba) ambacho kinatii Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data katika Umoja wa Ulaya (EU) 2016/679 (GDPR).
 • Je, app za simu za kiganjani zinaweza kuchukua nafasi za madaktari (GPs)? Mapitio ya malinganisho kati ya app za simu za kiganjani na majukumu ya madaktari.
  BMC Med Inform Decis Mak (2020) doi: 10.1186/s12911-019-1016-4.

  Wattanapisit, A., et al.

  Aina ya chapishoMapitio
  Matokeo
  • Ada inaweza ikatoa taarifa za huduma ya msingi ya afya na mapendekezo yanayohusiana na afya kwa watumiaji.
  • Ada inaweza kutoa orodha ya tambuzi za muda na tofauti kulingana na taarifa zilizokusanywa kwa AI.
  • Utaalam unaohusiana na afya ya kidigitali (mHealth) unapaswa kutambuliwa kama uwezo muhimu kwa madaktari.
 • Usahihi wa Chatiroboti (Ada) katika utambuzi wa magonjwa ya akili: Utafiti wa kulinganisha kesi kwa kutumia watumiaji wa Kawaida na wataalamu.
  JMIR Form Res (2019) doi: 10.2196/13863.

  Jungmann, S. M., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Ada inaweza kusaidia wataalamu wa utambuzi kama kifaa cha kukagua ili kutambua magonjwa ya akili kwa watu wazima.
  • Ada ilijaribiwa kwa kesi 20 zinazojumuisha wigo mpana wa magonjwa ya akili.
  • Ada iliuliza wastani wa maswali 34 na ilichukua dakika saba kumaliza tathmini za ugonjwa wa akili.
 • Kutoka kwa dalili hadi kutathmini upya vikaguzi utambuzi-dalili: Je, vikagua dalili hatimaye vinatosha na sahihi kutumia? Sasisho kutoka kwa mtazamo wa ENT
  HNO (2019) doi: 10.1007/s00106-019-0666-y.

  Nateqi, J., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Ada ilikuwa app ya pili bora zaidi kiutendaji kati ya 24 zilizojaribiwa katika katika somo la ENT.
 • Nini kilitokea wakati Pulse alivyojaribu app za ukaguzi wa dalili.
  Pulse Today (2019).

  Aina ya chapishoTathmini ya kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Madaktari wenye uzoefu walijaribu app nne za tathmini ya dalili dhidi ya kila mmoja: NHS, Babylon, Ada, na Your.MD.
  • Ada ilionyesha usahihi wa hali ya juu kwa ushauri na pendekezo la ugonjwa.
  • Ada ina kasi, rahisi kutumia, na inaweza kusaidia kutambua magonjwa makubwa kama vile mshtuko wa moyo.
 • Je, unaweza kweli kuamini app za kitiba kwenye simu yako?
  Wired UK (2017).

  Burgess, M.

  Aina ya chapishoTathmini ya kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Utendaji wa app za tathmini ya dalili zinaweza kutofautiana sana wakati zinajaribiwa dhidi ya kila mmoja kwa kutumia dalili sawa.
  • App tatu za tathmini ya dalili zilijaribiwa dhidi ya kila mmoja: Ada, Babylon, and Your.MD.
  • Ada ilikuwa kwa mbali sana app ‘bora zaidi’ iliyojaribiwa, ikiuliza maswali yanayoeleweka kuhusu dalili muhimu zaidi na kutoa mapendekezo bora zaidi kuhusu magonjwa.

Matoleo ya awali ya tafiti na machapisho ya Ada au kwa kushirikiana nayo

 • Ubora wa mapendekezo ya ugonjwa na ushauri wa dharura uliotolewa na app ya Ada ya tathmini ya dalili vilitathminiwa kwa kesi zilizozalishwa kwa uhuru na zilizoboreshwa kwa ajili ya Australia.
  medRxiv (2020) doi: 10.1101/2020.06.16.20132845.

  Gilbert, S., et al.

  Aina ya chapishoUtafiti wa kulinganisha kesi
  Matokeo
  • Pendekezo la juu kabisa la ugonjwa la Ada lilikuwa sahihi katika asilimia 65 ya kesi, na ugonjwa sahihi ulikuwa kwenye tatu bora katika asilimia 83.
  • Ushauri wa dharura wa Ada ulilingana na kiwango cha kipimo cha ubora katika asilimia 63 ya kesi, pamoja na asilimia 67 ya kesi za dharura na asilimia 57 ya zile zisizo za dharura.