Ada na magonjwa adimu

Ada na magonjwa adimu

Shirikiana nasi kuboresha matokeo ya magonjwa adimu kwa wagonjwa

Adimu, lakini yameenea: ugonjwa unatambulika adimu kama chini ya watu 5 kati ya 10,000 wameathirika. Hata hivyo, watu zaidi ya milioni 350 duniani wanaishi na ugonjwa adimu. [1] Dalili za magonjwa haya siyo za kawaida, na hufanya utambuzi kuwa mgumu. Ada inasaidia kufanya utambuzi wa wakati na matibabu sahihi ili kuboresha maisha ya wagonjwa wa maradhi haya.

Changamoto ya ugonjwa adimu duniani

Magonjwa Adimu
 • 1 kati ya 17 ya watu wanaishi na ugonjwa adimu [2]

 • 50% ya wagonjwa wa magonjwa adimu ni watoto [1]

 • miaka 6 na madaktari 7.3 mpaka utambuzi sahihi [1][3]

 • 7,000 magonjwa adimu yanayofahamika [1]

Suluhisho Letu

“Hatuwezi kukubali ukweli kwamba watu wanaoishi na ugonjwa adimu mara nyingi wanasubiri miaka sita kwa utambuzi sahihi. Akili bandia inatupa fursa ya kubadilisha hili na kuleta tofauti ya msingi kwenye maisha ya mamilioni ya watu duniani kote.”
Dr. Martin Hirsch
Mwanzilishi Mwenza & Mwanasayansi Mkuu

Uvumbuzi wa akili bandia wa Ada huwezesha wagonjwa na madaktari kufikia matokeo bora zaidi ya afya ya ugonjwa adimu kama ifuatavyo:

 • App ya Ada inasaidia wagonjwa kuelewa dalili za ugonjwa adimu.
 • Kifaa cha Ada cha kazi kwa madaktari kinawezesha ufanyaji wao wa maamuzi ya matibabu kwa wakati na utambuzi sahihi wa ugonjwa adimu. Soma utafiti wetu hapa, ili kujifunza kuhusu uwezekano wa Ada kuongeza kasi ya utambuzi wa ugonjwa adimu.
 • Maelfu ya Magonjwa na Dalili
 • Miaka 8 ya utafiti na maendeleo ya teknolojia yenye faida kwa biashara na soko la ushindani
 • Kufundishwa na maelfu ya matukio halisi

Malengo yetu

 1. Kuwezesha wagonjwa na kuongeza ufahamu

  Ada husaidia mamilioni ya watu duniani kutathmini dalili za magonjwa adimu na ya kawaida, na hutoa taarifa rafiki kwa mgonjwa ili kusaidia watu kuelewa hali zao na jinsi ya kuzidhibiti.

 2. Punguza muda wa ugunduzi

  Za wakati, tambuzi sahihi husaidia kuzuia vipimo visivyo vya lazima, kuboresha ufanisi wa rufaa, na kuanzisha matibabu sahihi.

 3. Kusaidia ushirikiano na utafiti wa matibabu

  Ushahidi uliokusanywa kwenye sehemu moja ya uwazi huwawezesha wataalamu kupitia mapendekezo ya Ada na kugawana taarifa/ mifano isiyo na utambulisho (anonymized cases) kwa ajili ya ushirikiano miongoni mwao.

Shirikiana nasi:
partnerships@ada.com