Biashara ya afya ya AI
Matokeo bora ya afya yanahitaji teknolojia ya kitiba iliyo erevu. Tuboreshe pamoja afya na huduma za afya.
Tathmini za kiafya zenye akili
Mwongozo wa kuaminika kuelekea maamuzi sahihi ya huduma za afya.
- Hutoa tathmini za dalili zenye ubora wa hali ya juu kwa mamilioni ya watu na ushauri wa utunzaji wa afya ulio salama zaidi ndani ya dakika kadhaa
- Huongeza ubora wa kitiba: Tafiti zinaonyesha Ada inatoa ujumuishaji wa magonjwa kwa 99% na ni sahihi zaidi kwa 35%, kwa wastani, kuliko app nyingine za tathmini ya dalili 1
- Hugundua matatizo makubwa ya kiafya kuliko bidhaa nyingine za aina yake, ikiwemo ugunduzi wa magonjwa adimu, watoto, uzazi, na akili
Uongozaji wa huduma ya kibinafsi ya afya
Msaidizi wa vipaumbele vya tiba mwenye akili.
- Hutoa mwongozo wa huduma za afya 24/7 na uhifadhi wa miadi ili kuunganisha watu na huduma sahihi kwa wakati unaofaa
- Huongeza ushiriki katika huduma ya afya ya kidijitali na ya simu - mshirika 1 alielekeza 14% kwenye ushiriki wa afya ya kidijitali
- Huongeza ufanisi wa rasilimali kwa kuelekeza watu kwenye chaguo la huduma ya afya lifaalo zaidi - mshirika 1 alielekeza 42% kwenye huduma ya afya isiyo ya dharura
Makabidhiano ya mgonjwa kwa daktari
Ripoti ya afya yenye violesura 2: 1 rafiki kwa mgonjwa, 1 tayari kwa daktari.
- Huwapa madaktari muhtasari wa ushauri wa kitiba kwa ajili ya muda wenye uelewa zaidi kuhusu wagonjwa
- Husaidia wagonjwa kutoa maelezo yao mara moja tu
- Hujiunganisha na mifumo ya rekodi za afya za kielektroniki (EHR) ili kuunganisha huduma za afya
Ufahamu wa data za kitiba
Dashibodi jumuishi ya data za afya zilizofichwa utambulisho.
- Huelewa tabia ya mtumiaji na maamuzi anayofanya kuhusiana na huduma za afya katika wakati halisi
- Husaidia kutoa taarifa muhimu kwenye ufanyaji wa maamuzi ya biashara, upangaji wa huduma, na muundo wa huduma
- Hukuwezesha kutambua mapungufu katika huduma na fursa za kuboresha
Mshirika wako wa kuaminika kwa ubora wa kitiba katika AI
- Imeundwa na madaktari kwa mpangilio wa kitiba
- Imethibitishwa na tafiti za kitiba zilizopitiwa na wataalamu wengine
- Inatekeleza kanuni zote za kifaa cha kitiba na viwango vya usalama wa data – HIPAA, MDD, GDPR, ISO 27001, ISO13485, BiM Badge
Gilbert, S. et al. BMJ Open, (2020). doi: 10.1136/bmjopen-2020-040269