Maktaba ya Magonjwa

Taarifa sahihi za masuala ya afya husababisha hatua sahihi za kukabiliana na matatizo ya kiafya. Maktaba hii ina vidokezo vinavyoweza kukusaidia kuwa na afya njema na ina taarifa za kweli kuhusu magonjwa. Kama ilivyo kwa app ya Ada, kila kitu utakachojifunza hapa kinatokana na uzoefu wa madaktari wetu katika masuala ya afya na tafiti za hivi karibuni.

Ipakue kwenye App StoreIpate kwenye Google Play

  Vidokezo vya kukusaidia kuitunza afya yako

  Mfano wa mtu akijishughulisha

  Kujishughulisha

  Kwanini usiwe na uthubutu? Muda wowote unaoutumia ukiwa umesimama ni uamuzi wenye mwelekeo sahihi. Utajihisi vizuri zaidi kwa kufanya hivyo.

  Mchoro wa mbu mwenye vimelea vya plasmodium

  Ugonjwa wa malaria

  Elewa malaria ni nini, dalili zake, na pata vidokezo kadhaa vya kujikinga vitakavyokufanya wewe na familia yako kuwa na afya njema.

  Mfano wa mtu akizungumza na mtaalam wake wa tiba kuhusu wasiwasi

  Kudhibiti wasiwasi

  Tenga muda kwa ajili yako. Kwa kuwa na uvumilivu kidogo na pia kujitunza, unaweza kudhibiti hali yako ya kuhisi wasiwasi, ili isiweze kuteka maisha yako.

  Mfano wa watu wanaotazama skrini za simu zao karibu na shisha

  Kupunguza muda wa skrini

  Tuangalie jinsi gani muda wa skrini unaweza kuathiri afya yako, kiasi gani cha utazamaji kinatambulika kama ni kingi kupita kiasi, na vidokezo kadhaa vya jinsi ya kupunguza.

  Mfano wa mtu aliyelala akiwa amefunika macho kwa barakoa ili kuboresha usingizi wake

  Usingizi bora

  Kwa kufuata kanuni rahisi za elimusiha ya usingizi, unaweza kupata usingizi kwa urahisi zaidi mwisho wa siku na kuamka ukijihisi ni mwenye nguvu mpya.

  Mfano wa mtu anayefurahia shughuli mbalimbali zinazowezekana kufanyika unapofanyia kazi nyumbani

  Kufanya kazi ukiwa nyumbani

  Kutoka nyumbani na kwenda eneo jingine kila siku kwa ajili ya kazi hujenga desturi katika maisha yako, husaidia kudumisha afya bora na ustawi.

  Mfano wa mtu akiota jua

  Kuota mwanga wa jua na vitamini D

  Tuangalie kwa karibu vitamini ya mwanga wa jua, jinsi unaweza kubaki salama wakati unapoiongeza mwilini, na nini cha kufanya ikiwa haupati ya kutosha.

  Mifano ya watu wajawazito katika hali za kila siku

  Utunzaji wa ujauzito wenye afya

  Wakati unajiandaa kumkaribisha mtu mpya duniani, mwili wako utapitia mabadiliko makubwa, yanayoonekana na yasiyoonekana.

  Mfano wa mtu akizungumza na mtaalam wa tiba kuhusu afya yake ya akili

  Ufahamu wa afya ya akili ya wanaume

  Uzoefu wako katika suala la afya ya akili unaweza kutegemea maumbile yako, uzoefu wa maisha, hali ya kijamii na kiuchumi, jinsia, na mengineyo.

  Mfano wa mtu anayekimbia ili kuepuka uchovu mwingi

  Kuepuka uchovu mwingi

  Kadiri msongo unavyoongezeka, ndivyo uchovu mwingi hunyemelea. Mara nyingi, inaweza kuwa ngumu kutambua, lakini kuna dalili kadhaa za kuzingatia.

  Mfano watu wenye ugonjwa wa kisukari wakikagua kiwango cha sukari katika damu

  Kupunguza hatari: ugonjwa wa kisukari aina ya 2

  Tafiti zinaonyesha kuwa hata dakika 30 tu za kutembea haraka kila siku zinaweza kupunguza hatari yako ya kupata ugonjwa wa kisukari aina ya 2. 

  Rafiki wa afya ya kibinafsi duniani

  Wakati tunaendelea kuunda maktaba yetu ya magonjwa kwa Kiswahili, unaweza kupata makala zaidi zinazohusiana na magonjwa mbalimbali kwenye tovuti yetu ya Kiingereza. Pata taarifa za afya zinazolenga profaili yako ya afya kwa kupakua app ya Ada.

  Anza kutumia app ya Ada leo

  Pakua app ya Ada