Usalama

Unaweza ukafikiria kuhusu usalama ndani ya Ada katika namna tatu:

 1. Watumiaji salama wanafahamu kwamba wakati wowote wanaweza kumwambia Ada wanapojihisi wagonjwa na kupata utaalamu wa matibabu wa kuaminika popote walipo.

 2. Madaktari salama wanawezesha ufanyaji wao wa maamuzi ya matibabu kwa kutumia akili bandia za Ada na maktaba iliyo sheheni maelfu ya magonjwa ya kawaida na adimu.

 3. Watumiaji na madaktari salama wanajua kwamba taarifa (data) wanazotupa zipo sehemu salama, na hazigawiwi kwa mtu au kampuni yeyote bila ruksa zao. Taarifa zinatumika kuboresha tu upatikanaji wa utaalamu wa kuaminika wa matibabu.

Aina zote tatu za usalama zinahitaji uaminifu na uwazi.

Ada isingeweza kusaidia mamilioni ya watu kusimamia afya zao bila imani yao kwetu. Kwa maana hiyo, tunakuwa wawazi juu ya kile tunachofanya kudumisha usalama.

Hivi ndivyo tunavyosimamia usalama

Taarifa

Tunafuata ‘usalama kwa njia ya muundo,’ hii ina maanisha Ada inatekeleza usalama kuanzia mwanzoni mwa uhai wa bidhaa, na sio baada na wala sio kama kitu cha ziada. Kwa maneno mengine, usalama na bidhaa za Ada vinakwenda sambamba.

Hifadhi

Tunatenganisha wasifu wa mtu na taarifa zake za kiafya na kuhifadhi tofauti kila moja ya taarifa hizo kwenye mifumo ya kuhifadhi (servers) taarifa za intaneti Ulaya.

Wafanyakazi/ Waajiriwa

Afisa wetu wa Usalama wa Taarifa, Jens, anahakikisha kila mfanyakazi wa Ada anatimiza majukumu yake binafsi ya kiusalama.

Ofisi

Tunasimamia usalama wa ofisi zetu ili kulinda taarifa, kuanzia kwenye kompyuta mpakato zenye viwambo vinavyojizima vyenyewe (automatic screenlocks) mpaka kwenye milango ya chuma.

Majaribio

Mara kwa mara huwa tunajaribu miundombinu yetu ya usalama ili kubaini sehemu dhaifu na kuzirekebisha.

Ukaguzi

Ada inakaguliwa mara kwa mara na mamlaka za nje na za ndani ya kampuni ili kuhakikisha tunakidhi matakwa ya kisheria, na pia kuwa na bidhaa zenye viwango vinavyokubalika.

Ada inatimiza matakwa ya kisheria yafuatayo:

 • ISO 27001

  Imethibitishwa kwa kiwango cha ubora wa usalama wa taarifa (data)

 • Inakidhi viwango vya ISO 13485

  Inakidhi kiwango cha ubora kwa vifaa vya matibabu

 • Nembo ya CE

  Bidhaa zetu zote zimesajiliwa kama kifaa cha matibabu daraja la kwanza katika Eneo la Kibiashara la Ulaya (European Economic Area) (EEA). Nembo ya CE inathibitisha ubora wa bidhaa ndani ya soko la Ulaya.

 • Inakidhi mahitaji ya EU-GDPR

  Sheria za jumla za Uthibiti wa Data katika Umoja wa Ulaya

 • Nembo ya BiM

  Nembo ya BiM inawakilisha Shirika la Ujerumani la usimamizi wa ubora wa matibabu ya intaneti.

Bado unataka kujua zaidi kuhusu suala la usalama ndani ya Ada?

Soma Privacy Policy, Terms & Conditions, FAQs yetu, au wasiliana na sisi kupitia hello@ada.com.