Wataalamu wetu wa tiba

Wajue baadhi ya madaktari, wanasayansi, na wastadi wa tiba wanaofanya kazi Ada. Pamoja na wataalamu wengine wa tiba, hawa wastadi kutoka ndani wanatoa ufahamu na usimamizi wa bidhaa zetu zote, utafiti, tathmini za tafiti, mwongozo wa kitiba, mashirikiano, maarifa ya kitiba, na maudhui ya kitiba ya mtandaoni (intaneti).

Wajumbe wa timu hii wanafanya kazi pamoja kuhakikisha maudhui yetu ya tiba ya mtandaoni ni sahihi, ya wakati, na rahisi kuyasoma na kuyaelewa. 

Uongozi wa Masuala ya Kitiba

Claire Novorol

Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mkuu wa Tiba

Dk. Claire Novorol

Mwanzilishi-mwenza & Afisa Mkuu wa Tiba

Dk. Claire Novorol

Kabla ya kuwa mwanzilishi mwenza wa Ada, Dk. Novorol alihitimu shahada ya Patholojia (utafiti wa magonjwa) na tiba, pamoja na shahada ya uzamivu ya Mishipa ya Fahamu (Neuroscience) kutoka chuo cha Cambridge. Amefanya kazi kama daktari wa watoto kupitia Mpango wa Huduma za Afya ya Taifa - NHS (Uingereza) kabla ya kujikita kwenye masuala ya chembe za urithi (clinical genetics). Claire pia ni mwanzilishi wa “Doctorpreneurs”, ambayo ni jumuiya inayojumuisha wataalamu wa huduma za afya kutoka pande zote za dunia wanaovutiwa na uvumbuzi na ujasiriamali.

Martin Hirsch

Mwanzilishi-mwenza & Mshauri Mkuu wa Kisayansi

Dk. Martin Hirsch

Mwanzilishi-mwenza & Mshauri Mkuu wa Kisayansi

Dk. Martin Hirsch

Kabla ya kuwa mwanzilishi mwenza wa Ada, Dk. Hirsch alihitimu shahada ya Nadharia ya Tiba kutoka Chuo cha Philipp cha Marburg na kufanya kazi kama mtafiti wa kujitegemea. Martin pia ana shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Mishipa ya Fahamu (Neuroscience). Maeneo anayopendelea kufanya utafiti ni pamoja na kwenye sayansi ya tambuzi za mishipa ya fahamu, semantiki (elimu-maana katika lugha), na matumizi ya teknolojia kwenye kusaidia binadamu kufikiri na kufanya maamuzi.

Utawala wa Masuala ya Kitiba

Matthew Fenech

Dk. Matthew Fenech

Kiongozi wa Usalama wa Tiba

Dk. Fenech amehitimu Shahada ya Tiba kutoka Chuo cha Malta. Baada ya kuhitimu na kuendelea na masomo ya uzamili, alianza mafunzo yake ya vitendo katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Cambridge. Matthew alijikita kwenye kisukari na magonjwa ya homoni na kupata Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha East Anglia kwa utafiti wake kwenye mahusiano baina ya unene wa kupita kiasi (obesity) na kisukari. Pia alihitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Tambuzi za Kikompyuta kutoka Chuo cha London, Birkbeck.  

Shubhanan Upahyay

Dk. Shubhanan Upadhyay

Stadi wa Tiba

Dk. Upadhyay ni mmoja wa madaktari wa dharura wa mpango wa Huduma za Afya ya Taifa - NHS (Uingereza) na mshiriki wa mpango wa Wajasiriamali wa Tiba (2018/19). Ana Shahada ya Udaktari na Shahada ya Upasuaji kutoka Chuo cha Imperial. Maeneo aliyo na utaalamu nayo ni pamoja na masuala ya afya duniani, tiba ya kitropiki, na elimu ya tiba. Kikazi anafahamika zaidi kama “Dk. Shubs” na huandika kuhusu masuala ya afya duniani, tiba ya kitropiki, elimu ya tiba, na uwezo wa teknolojia kusaidia huduma ya mgonjwa na usimamizi thabiti wa afya.  

Adel Baluch

Dk. Adel Baluch

Stadi wa Tiba

Dk. Baluch anafanya kazi kama daktari chini ya Mpango wa Huduma za Afya ya Taifa - NHS (Uingereza). Ni mhitimu wa Bartholomew’s na Chuo cha Udaktari cha Royal London, na ana Shahada ya Udaktari na Shahada ya Upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Queen Mary cha London. Adel pia ana sifa za uzamili baada ya kufaulu mitihani yake na kufuzu uwanachama wa Chuo cha Madaktari cha Royal (Royal College of Physicians), Chuo cha Royal cha Madaktari wa Magonjwa ya Jumla (General Practitioners), na Bodi ya Marekani ya Tiba ya Mtindo wa Maisha (American Board of Lifestyle Medicine).

Maarifa ya Kitiba

Ewelina Türk

Ewelina Türk

Makamu wa Rais wa AI ya Kitiba

Ewelina anaongoza timu yetu ya maarifa ya kitiba. Amezaliwa Poland na kukulia Ujerumani. Ewe amesomea udaktari katika chuo cha tiba cha Charité, Berlin, akiweka maslahi zaidi kwenye magonjwa ya watoto, haswa huduma za dharura na kinga. Zaidi ya hayo, Ewelina hivi sasa anamalizia shahada ya uzamivu katika magonjwa ya baridi yabisi kwa watoto.

Sampuli ndogo ya madaktari ndani ya timu yetu ya Maarifa ya Kitiba

Michal Stebnicki

Dk. Michal Stebnicki

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Stebnicki alisomea udaktari Lodz na Wroclaw kabla ya kuhitimu Shahada yake ya Udaktari kutoka Chuo cha Udaktari cha Wroclaw Kitivo cha Tiba. Michal amebobea mahsusi kwenye magonjwa ya akili na katika eneo hilo, alipata uzoefu zaidi wa kikazi kama mkurufunzi na kama daktari msaidizi katika kliniki za Berlin.

Chi-Yu Liu

Dk. Chi-Yu Liu

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Liu alifanya kazi kama daktari mashariki mwa Taiwani. Shauku yake ya kusimamia haki na ustawi wa watoto, haswa katika afya, ilimfanya asomee Shahada ya Uzamili katika masuala ya Haki za Watoto huko Potsdam, Ujerumani.

Yusuf Cem Kaplan

Dk. Yusuf Cem Kaplan

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Kaplan alipata mafunzo ya taaluma ya madawa Uturuki na pia ni daktari wa magojwa ya binadamu. Kabla ya Ada, alifanya kazi kama mwalimu wa taaluma ya madawa na kuongoza “Teratology Information and Research Center,” ambacho ni kituo kilichoundwa kusaidia wanawake wajawazito na wanaonyonyesha na madaktari wao. Kituo hicho pia kipo kwa ajili ya kujibu maswali kuhusiana madhara ya madawa wakati wa ujauzito na kunyonyesha. Kitiba, Dk. Yusuf amejikita kwenye matatizo ya kiafya yanayohusiana na sumu na madawa. 

Kirsten Gray

Dk. Kirsten Gray

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Gray alipata Shahada yake ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Otago nchini New Zealand, na wakati huo alishiriki pia katika miradi ya utafiti katika maeneo ya magonjwa ya akili. Baada ya kuhitimu, alifanya kazi kama daktari hospitalini kwa miaka kadhaa, akiweka masilahi katika magonjwa ya akili na watoto. Kabla ya kujiunga Ada, Kirsten alifanya kazi katika Hospitali ya Watoto ya Starship huko Auckland (New Zealand). 

Nisha Kini

Dk. Nisha Kini

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Kini amehitimu Shahada zake za Udaktari na Upasuaji kutoka Chuo Kikuu Cha Maharashtra Cha Sayansi ya Afya na Shahada yake ya Uzamili ya Afya ya Jamii katika elimu ya magojwa ya mlipuko na takwimu za Kibiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Massachusetts Amherst. Alifanya kazi kama afisa mkazi wa tiba nchini India, na halafu akafanya kazi kama mtafiti katika ulimwengu wa taaluma na sekta ya tiba ndani ya Marekani na Ulaya. Anajihisi kupata heshima kwa kuwa sehemu ya timu inayochanganya tiba na teknolojia ya akili bandia (AI) ili kusaidia mamilioni ya watu ulimwenguni kote. 

Nils Metzger

Nils Metzger

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Nils amehitimu Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Rheinische Friedrich-Whilhelms,  Bonn. Akiwa kama mwanafunzi msaidizi, alihudumu kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na wodi ya kawaida ya Kliniki ya Chuo Kikuu cha Bonn na kumaliza mafunzo yake kwa vitendo (internship) Berlin ambapo alijikita kwenye taaluma ya magonjwa ya watu wazima na taaluma ya magonjwa ya mfumo wa mkojo. Wakati wa masomo yake, Nils alitoa mchango katika uundaji wa hifadhidata ya watu wenye kifafa kinachotokana na inflamesheni kwenye ubongo (limbic encephalitis). Nils ana shauku ya kusaidia kuboresha maisha ya watu duniani kote kupitia teknolojia ya Ada.

Dk. Malek Hamzeh

Mhandisi wa Maarifa ya Kitiba

Dk. Hamzeh alipata msaada wa masomo ili kusomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Istanbul, Uturuki, na kuhitimu Shahada ya Udaktari. Alifanya kazi kama daktari wa familia kwenye kituo cha afya ya jamii Istanbul, ambapo kwa kiasi kikubwa wagonjwa walikuwa ni wakimbizi walioshindwa kupata huduma za afya hapo awali. Anaamini upatikanaji wa huduma za afya ni haki ya kila mtu, na anafurahi kujiunga na Ada ili kuwezesha upatikanaji huo.

Daniel Glauert

Daniel Glauert

Mwanafunzi wa Maarifa ya Kitiba

Daniel ni mtahiniwa wa udaktari katika Chuo cha Udaktari cha Charité, Berlin na mmoja wa wanafunzi wetu wa maarifa ya kitiba. Ana uzoefu katika Chama cha Kitaifa cha Wanafunzi wa Udaktari, bunge la Chuo Kikuu cha Humboldt, mafunzo ya udaktari kwa vitendo katika nchi zinazoendelea. Daniel anavutiwa na siasa za masuala ya afya na masuala ya afya ulimwenguni. Amejidhatiti kuleta mustakabali wa tiba katika mitaala ya chuo kikuu na anashirikiana kuendeleza na kufundisha vipindi kadhaa juu ya afya ya kidijitali. 

Usimamizi wa Maudhui ya Kitiba

Fabio Pereira

Dk. Fabio Pereira

Meneja wa Maudhui ya Kitiba

Dk. Pereira alisomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Porto, na alihitimu masomo yake ya udaktari kwa kupata Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Tiba za Viumbe katika Chuo cha Udaktari cha Charité, Berlin. Wakati hafanyi maudhui yetu ya tiba yawe sahihi, rafiki kwa mgonjwa, na ya kuvutia kadri iwezekanavyo, Fábio hufanya utafiti wa mifano ya utambuzi wa muziki kupitia shahada yake ya Uzamili ya utafiti wa sauti katika Chuo cha Goldsmiths jijini London. 

Magonjwa ya Mlipuko & Afya ya Jamii

Andreas Gilsdorf

Dk. Andreas Gilsdorf

Mkurugenzi wa Magonjwa ya Mlipuko na Afya ya Jamii

Dk. Gilsdorf ni daktari aliyebobea kwenye magonjwa na majeraha yatokanayo na kazi na magonjwa ya kuambukiza. Kabla ya Ada, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi na Naibu Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Kuambukiza katika Taasisi ya Robert Koch. Huko, Andreas alikuwa na jukumu la mfumo wa kitaifa wa uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza na alikijenga na kukiongoza Kituo cha Operesheni ya Dharura. Pia ana uzoefu wa kufanya kazi katika ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Ulaya. 

Alicia Mehl

Alicia Mehl

Mtaalamu wa Magonjwa ya Mlipuko

Alicia alipata mafunzo ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kule London School of Hygiene & Tropical Medicine na ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Mlipuko katika timu yetu ya Magonjwa ya Mlipuko & Afya ya Jamii. Ana uzoefu wa maeneo mbalimbali akifanya kazi katika nchi zenye rasilimali chache, ikiwemo Msumbiji, Nigeria, na Saint Lucia. Alicia anapendelea kuunganisha nguvu ya Akili Bandia (AI) na mbinu za kukabiliana na magonjwa ya milipuko ili kufanikisha kufikia matokeo bora zaidi ya afya kwa wote.  

Tathmini ya Kitiba

Stephen Gilbert

Dk. Stephen Gilbert

Mkurugenzi wa Tathmini ya Kitiba

Dk. Gilbert alihitimu Shahada ya Uzamivu katika Uchakatishaji wa data za Biolojia (Computational Biology) kutoka Chuo Kikuu cha Leeds. Ni mtaalamu wa tafiti za kitiba na mwanafiziolojia. Anafanya kazi katika sekta ya vifaa vya kitiba katika tathmini na changanuzi za kitiba, maandiko ya kitiba, na masuala ya udhibiti. Stephen ana uzoefu mpana katika fiziolojia ya moyo na tiba.

Magonjwa Adimu

Fiona Pick

Dk. Fiona Pick

Mkurugenzi wa Tiba, Magonjwa Adimu

Dk. Pick ametumia miaka 19 akifanya kazi kama daktari katika mpango wa Huduma za Afya ya Taifa - NHS (Uingereza). Amebobea kwenye magonjwa ya watoto, na katika miaka 10 iliyopita alifanya kazi kama mshauri wa kasoro za chembe za urithi (clinical geneticist) jijini London. Fiona alihitimu Shahada yake ya Uzamivu katika Utafiti wa Kitiba, akijikita kwenye chembe za urithi za magonjwa ya limfu (lymphatic disorders). Kama Mkurugenzi wa Tiba, anasimamia operesheni za utawala za masuala ya kitiba za Ada, akifanya kazi kwa karibu katika miradi ya tathmini za kitiba, ujengaji wa mahusiano na wadau wa tiba kwa maendeleo ya biashara, masuala ya afya duniani, na mipango inayohusu magonjwa adimu.