Sera ya Faragha ya Ada Health GmbH

Ilibadilishwa mwisho: 29 Aprili 2020

TAFADHALI SOMA SERA HII KWA MAKINI KABLA YA KUTUMIA HUDUMA ZA ADA HEALTH GmbH.

Unapaswa kuwa na umri wa miaka 16 au zaidi ili kutumia Huduma zetu.

Kulinda data yako, faragha na data ya kibinafsi (kama ilivyofasiriwa katika Kifungu cha 4(1) cha Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data (Mataifa ya Umoja wa Ulaya) 2016/679 (“GDPR”)) ni muhimu sana kwa Ada Health GmbH ( “sisi”, au “yetu”). Ni muhimu sana kwetu kwamba wateja wetu (“watumiaji”) wanajihisi salama wanapotumia Huduma hizi.

Sera hii ya faragha (“Sera ya Faragha”), (pamoja na Sheria na Masharti yetu iliyo katika ada.com/sw/terms-and-conditions, Sera yetu ya Vidakuzi iliyo katika ada.com/sw/cookie-policy na hati zinginezo zote zilizorejelewa ndani yake), inaweka msingi wa kuchakata data yoyote binafsi tunayokusanya kutoka kwako, au ambayo unatupa. Tafadhali soma sera hii ya faragha kwa umakini ili uelewe aina ya data tunayokusanya kutoka kwako, tunavyoitumia, hali inayoweza kupelekea sisi kuishiriki na watu wengine, na haki zako kuhusiana na data ya kibinafsi unayotupatia.

Wakati wa kutumia “Ada” kupitia programu yetu ya kidijitali (“App”), wakati na pale inapopatikana programu yetu kwa njia ya tovuti (“Tovuti-pachika“), kifaa chetu cha ukaguzi (“Kifaa cha Ukaguzi”), au makati wa kutumia tovuti yetu ya ada.com (“Tovuti”), au huduma yoyote na/ au bidhaa tutakayoweza kukupatia (Tovuti pamoja na App, Tovuti-pachika, Kifaa cha Ukaguzi, na bidhaa yetu yoyote na huduma, “Huduma”), utaombwa kuonyesha kuwa unatambua uwepo wa sera, na inapofaa, kutoa idhini yako ya mambo yaliyoelezewa ndani ya sera hii.

Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo vya tovuti nyingine. Ikiwa unafuata kiungo chochote cha hizo tovuti nyingine, tafadhali tambua kwamba zina sera zao za faragha na kwamba hatuna jukumu lolote au dhima itokanayo na sera zao au uchakataji wa data zako binafsi. Tafadhali kagua sera hizi kabla ya kuwasilisha data zozote binafsi kwenye tovuti kama hizi.

1. Sisi ni nani

Sera hii ya faragha inatumika kwa uchakataji wa data yoyote binafsi unaofanywa na Ada Health GmbH (HRB 189710), Karl-Liebknecht-Straße 1, 10178 Berlin, Ujerumani kuwa mdhibiti wa data (kama inavyofafanuliwa chini ya Kifungu cha 4(7) cha GDPR) za masuala yote ya uchakataji yanayohusiana na Huduma.

Maswali, maoni na maombi kuhusu Sera hii ya Faragha yanakaribishwa na yanapaswa kutumwa kwa dpo@ada.com. Afisa wetu wa ulinzi wa data ni Jens Pahl.

2. Maelezo ya jumla ya uchakataji wetu wa data kuhusiana na Huduma

Tunaweza kukusanya na kuchakata data ifuatayo kukuhusu:

Maelezo ambayo unatupa. Utaombwa utupe maelezo yako wakati:

 • unajaza fomu kwenye Tovuti au App yetu, au kuwasiliana nasi kwa simu, barua pepe au kwa njia nyingine;
 • unajiandikisha kutumia Huduma zetu, kujiunga na kijarida chetu, barua pepe za matangazo au nyenzo nyingine za masoko;
 • unatumia Huduma;
 • Una ripoti kuhusu hitilafu ya Huduma zetu; au
 • Shiriki katika tafiti na kamilisha kutoa maelezo ambayo tunayatumia kwa madhumuni ya utafiti huo (ingawa sio lazima ushiriki katika hizi tafiti ikiwa hutaki).

Maelezo ambayo utaombwa utupe kwa madhumuni haya yanaweza kujumuisha jina lako, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, anwani ya barua pepe, nambari ya simu, dalili za ugonjwa wako, mambo yanayoweza kuwa visababishi vya dalili za ugonjwa wako, bima ya afya, historia ya matibabu, mzio wowote ulio nao, au maelezo zaidi yanayohitajika ili kuthibitisha utambulisho wako.

Maelezo tunayokusanya kukuhusu. Ingawa hatutayatumia kukutambua, tunaweza kukusanya maelezo yafuatayo kila unapotembelea Tovuti na App yetu:

 • Data ya matumizi: maelezo ya kiufundi kuhusu kifaa chako ikijumuisha maelezo maalum ya kifaa kama vile muundo wa kifaa chako, toleo la mfumo wa uendeshaji, vitambulisho maalum vya kifaa, na maelezo ya mtandao wa vifaa vya mkononi; maelezo ya mara ulizotembelea Tovuti na App yetu, pamoja na mtiririko wa Vitambuzi Sare vya Rasilimali (“URL”) vya kuingia, kupitia na kutoka kwenye Tovuti na Programu yetu (pamoja na tarehe na saa); maelezo ya magonjwa na dalili zilizotafutwa.
 • Data ya uchambuzi: anwani yako ya IP, mfumo wa uendeshaji wa kifaa na aina ya kivinjari; maelezo kuhusu duka gani la app ambalo ulipakulia App yetu; urefu wa muda uliotumia kwenye kurasa fulani, na maelezo ya matumizi kwenye ukurasa (kama vile misogeo ya kiteuzi, ishara za vidole, mibofyo na matumizi ya kiteuzi).

Ikiwa unatumia Huduma zetu kwa niaba ya mtu mwingine, sharti uwe umepata ruhusa isiyo na mashaka kutoka kwa watu ambao unatupatia data zao kabla ya kushiriki data hizo. Ili kuepusha mashaka yoyote, marejeo yoyote katika Sera hii ya Faragha kwenye “data zako” yatajumuisha data zinazohusu watu wengine ambazo umetupatia.

3. Shughuli maalum za uchakataji, aina na madhumuni ya matumizi yake

3.1 Unapotumia Tovuti yetu

 • Aina za data: Anwani ya IP ya kifaa kinachotumika, tarehe na saa za kufikia, jina na URL ya faili iliyoombwa, Tovuti iliyotoa njia ya kufikia (“Rufaa ya URL”), kivinjari kilichotumika na, ikihitajika, mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako na kitambulisho cha mtoa huduma za ufikiaji wako.
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia data zilizo hapo juu ili kukuwezesha kufikia Tovuti yetu, kuhakikisha kwamba Tovuti inaweza kamata intaneti kiulaini na ni rahisi kutumia; kuchambua usalama na uthabiti wa mfumo, na pia kwa madhumuni ya ziada ya kiusimamizi.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea madhumuni ya kukusanya data yaliyoorodheshwa hapo juu. Hatutumii data zilizokusanywa kwa madhumuni ya kukutambua. Haulazimiki kutoa data binafsi zilizoanishwa hapo juu. Hata hivyo, hautoweza kufikia Tovuti ikiwa data binafsi za aina hiyo hazikutolewa.
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itaondolewa baada ya siku 14, isipokuwa likitokea tukio lolote linalohusiana na usalama (kwa mfano, shambulio la DDoS). Ikiwa kuna tukio linalohusiana na usalama, faili za kumbukumbu za seva zitahifadhiwa hadi tukio hili linalohusiana na usalama limeondolewa na kufafanuliwa kabisa.

3.2 Unaposajili akaunti ya mtumiaji katika App yetu

 • Aina za data: Anwani ya barua pepe na nywila, kitambulisho cha mtumiaji, jina la maelezo mafupi, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, bima ya afya (hiari), maelezo ya jumla kuhusu afya yako (hiari) kama vile uvutaji sigara, kuongezeka kwa shinikizo la damu, kisukari na hali ya ujauzito.
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia data zilizo hapo juu ili kukupa akaunti ya mtumiaji na kukuwezesha kufikia Huduma zetu. Tunatumia maelezo ya jumla ya afya kwa uchambuzi wa msingi. Haiwezekani kufikia huduma zetu ikiwa data (zisizo za hiari) hazijatolewa.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Utendaji wa mkataba (Kifungu cha 6 (1) (b) GDPR / ridhaa (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR).
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itafutwa au haitatambuliwa kwa majina (na haiwezi kuhusishwa na mtu mahsusi asilia) unapoomba kufutwa kwa akaunti yako au unapofuta akaunti yako kwenye App. Ikiwa hujatumia akaunti yako kwa zaidi ya miezi 24, tutawasiliana na wewe kubaini ikiwa unataka kuendelea kutumia Huduma zetu. Usipotumia akaunti yako ya mtumiaji kwa miezi mingine 12, tutafuta akaunti yako na kuficha utambulisho wa data zako (ili isiweze kuhusishwa na mtu mahsusi asilia).

3.3 Kuingia kwa Facebook

 • Aina za data: Kitambulisho cha Facebook, anwani ya barua pepe (ikiwa imetolewa katika akaunti ya Facebook), na nambari ya simu (ikiwa imetolewa katika akaunti ya Facebook) na muda na tarehe ya kuingia.
 • Matumizi ya data hizo: Ukichagua kutumia na kuingia kwa kutumia Facebook, tutapokea data zilizoorodheshwa hapo juu kutoka Facebook na idhini yako kujaza data zako za mtumiaji kwenye App, na kuthibitisha utambulisho wako. Tafadhali tambua kwamba ikiwa unaingia kupitia Facebook, Facebook pia itachakata data zako (kuingia). Hatuwajibikii na uchakataji wa data hizi. 
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali ni kuwapa watumiaji ambao hawana akaunti ya barua pepe au wanaotaka kuingia kwa kutumia akaunti zao za Facebook chaguo la kutumia Huduma zetu.
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa madhumuni haya unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Kifungu cha 3.2. Data inayochakatwa na Facebook, ambayo hatuidhibiti ikiwa utachagua kuingia kwa kutumia Facebook, inaweza kusalia kwenye seva za Facebook. Ikiwa unafuta akaunti yako ya Facebook na unataka kutumia App, utaelekezwa kuingia kwa kutumia anwani ya barua pepe au utaratibu mwingine wa kuingia.

3.4 Unda kesi

 • Aina za data: Jina la maelezo mafupi (Profile name) ya kesi ya tathmini na data husika za afya binafsi zinazohitajika ili kutoa tathmini kama vile dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, mzio, hali ya ujauzito, na historia muhimu na/au inayohusiana na matibabu, na muda na tarehe ya tathmini.
 • Matumizi ya data hizo: Ili kukupa Huduma zetu, kwa mfano, lakini haiishii tu kwenye kupendekeza uwezekano wa visababishi vya dalili zilizotolewa (tathmini), fuatilia dalili zako, au kutoa majibu ya vipimo vya maabara.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR). Unaweza kubatilisha/ kuondoa idhini yako wakati wowote. Hata hivyo, haiwezekani kukupa Huduma zetu (yaani, tathmini) bila idhini yako.
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itafutwa au haitatambuliwa kwa majina (na haiwezi kuhusishwa na mtu mahsusi asilia) unapoomba kufutwa kwa akaunti yako ya mtumiaji au kufutwa kwa kesi mahsusi au unapofuta akaunti yako au kesi kwenye App.

3.5 Uchanganuzi wa maelezo ya kesi ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa mfumo wetu wa tathmini za kitiba

 • Aina za data: Kitambulisho cha akaunti ya Ada (inapofaa), Kitambulisho cha maelezo mafupi (inapofaa), Kitambulisho cha kesi, muda na tarehe ya tathmini, eneo la kijiografia la tathmini, data zilizotolewa kwenye kesi (data binafsi zinazohitajika ili kutoa tathmini kama vile umri, jinsia, dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, mizio, hali ya ujauzito, na historia muhimu na/ au inayohusiana na matibabu), nakala ya mrejesho, matokeo ya tathmini, na data kuhusiana na maunzi laini na kifaa (kama vile namba za toleo, mfumo wa uendeshaji, na Kitambulisho cha kifaa).
 • Matumizi ya data hizo: Ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa Huduma zetu, ni muhimu kukagua ubora wa matokeo ya tathmini (“Uchanganuzi”). Timu ya usalama na ubora (“Wastadi wa Tiba”) hutumia data ya majina bandia, na inapofaa, data za jumla, ili kutathmini matokeo ya tathmini na kubaini kama uboreshaji wowote unahitajika ili App yetu na bidhaa yoyote ya kitiba tunayounda ikidhi viwango vya juu kabisa vya ubora na usalama.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji huo unahitajika ili kutimiza viwango vinavyohitajika vya ubora na usalama wa App yetu ambayo inakidhi sifa za kuwa kifaa cha matibabu chini ya kanuni za kifaa cha matibabu na kama ilivyotolewa katika maandishi ya kisheria yafuatayo (Sehemu ya 22 (1) nambari 1 c) BDSG, Kifungu cha 9 (2) (i) GDPR), kwa msingi wa majukumu ya Uchunguzi wa baada ya mauzo chini ya Sehemu ya 6 (1), (2) MPG kuhusiana na Sehemu ya 7 (4) ya Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Kijerumani kuhusiana na Viambatisho vya X, VII, (4) vya Maagizo ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (93/42 / EC) (au kutumika moja kwa moja kuanzia tarehe 26.05.2020 na siyo mbele ya hapo, lakini ikichukuliwa kama tayari inatumika ili kuhakikisha viwango vya juu vya ubora na usalama wa App yetu, Kifungu cha 83 na Kiambatisho cha III cha Sheria ya Vifaa vya Kitiba vya Umoja wa Ulaya (2017/745/EU). 
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unategemea kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data za kesi yako hazitotumika tena kwa dhumuni hili.

3.6 Tathmini ya ufaafu wa kushiriki katika utafiti wa kitiba na mwaliko

 • Aina za data: Anwani ya barua pepe, jina la maelezo mafupi, tarehe ya kuzaliwa, dalili za ugonjwa, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio na data nyingine ambazo umetupa.
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia data zilizo hapo juu kukagua ufaafu wako wa kushiriki katika utafiti wa kitiba na kukualika kushiriki katika utafiti wa kitiba na mmoja wa washirika wetu wa utafiti wa kitiba ambaye anaweza kuwa na maslahi kwako. Tungependa kukuhakikishia kuwa hatutatuma data yoyote binafsi kwa washirika wetu wa utafiti wa kitiba bila idhini yako.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR).
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitatumika tena kwa dhumuni hili.

3.7 Matumizi ya data za kiafya kwa madhumuni ya takwimu na utafiti

 • Aina za data: Kitambulisho cha akaunti ya Ada (inapofaa), Kitambulisho cha kesi, Kitambulisho cha maelezo mafupi (inapofaa), umri, jinsia, dalili za ugonjwa, eneo (nchi), sababu hatarishi, matokeo ya tathmini kama vile uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio, muda na tarehe ya tathmini, na data nyingine husika na zinazohusiana unazoweza kuwa umetupatia.
 • Matumizi ya data hizo: Tunachakata data zilizofichwa utambulisho ili kukusanya takwimu za jumla za ueneaji wa kijiografia wa aina fulani za dalili na magonjwa, na kuwasilisha muhtasari wa aina hizo za takwimu kwa washirika wetu katika utaratibu ambao zinakuwa zimefichwa utambulisho usiobatilishika.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji huo ni muhimu kwa madhumuni ya kitakwimu na tunawapa washirika wetu muhtasari tu wa takwimu zilizofichwa utambulisho ambapo haiwezekani kumtambua mtu mahsusi asilia (Kifungu cha 9 (2) (j) DSGVO; Sehemu ya 27 (1) BDSG). Maslahi yetu halali katika uchakataji wa data kwa madhumuni haya ni kusaidia maendeleo ya utafiti wa kitiba sambamba na malengo yetu ya kiujasiriamali ambayo pia ni kwa maslahi ya umma kuboresha huduma za afya. Kwa sababu zinazotokana na hali yako mahsusi, unaweza kukataa kufanyika kwa uchakataji huo wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa dpo@ada.com (unaweza kupata maelezo zaidi katika sehemu ya 8).
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data yako kwa msingi wa uundaji takwimu hizi unategemea kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitatumika tena kwa madhumuni haya. Utambulisho wa takwimu umefichwa.

3.8 Matumizi ya data za kiafya kwa madhumuni ya afya ya jamii

 • Aina za data: Kitambulisho cha akaunti ya Ada (inapofaa), Kitambulisho cha kesi, Kitambulisho cha maelezo mafupi (inapofaa), Kitambulisho cha kifaa, umri, jinsia, dalili za ugonjwa, eneo (nchi), mambo yenye kuhatarisha, matokeo ya tathmini kama vile uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa, historia ya matibabu, mizio, muda na tarehe ya tathmini, na data nyingine husika na zinazohusiana unazoweza kuwa umetupatia.
 • Matumizi ya data hizo: Tunachakata data za kiafya zilizofichwa utambulisho kwa madhumuni ya afya ya jamii (kama ilivyoelezewa na GDPR kariri 54) kama vile kuchanganua data za kesi zinazohusiana na mwenendo wa afya ya jamii, magonjwa adimu na matishio na kutambua mambo yatakayoweza kuboresha afya ya jamii kama vile kutafuta kuhusu ueneaji wa magonjwa mahususi, sifa za magonjwa mahususi na kupata ufahamu kwenye vipengele mahususi vya tathmini. Tunashiriki na kuwasilisha matokeo kama muhtasari wa takwimu kwa washirika wetu zikiwa zimefichwa utambulisho usiobatilishika. Tunaweza pia kuchakata data za aina hiyo ili kukupatia mwongozo bora kabisa kadiri iwezekanavyo, kwa mfano, kwa kukuelekeza kwenye kituo cha huduma kinachofaa zaidi na kupunguza huduma zisizo za lazima kwenye mifumo ya afya iliyoelemewa.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Uchakataji ni lazima kwa sababu ya maslahi ya jamii katika eneo la afya ya jamii (Kifungu cha 9 (2)(i) DSGVO, kifungu cha 22 (1) (1) c) BDSG)). Maslahi yetu halali katika kuchakata data kwa madhumuni haya ni kusaidia maendeleo ya afya ya jamii kwa kudhibiti vitisho vikubwa vya kimipaka kwa afya. Kwasababu zinazotokana na hali yako mahsusi, unaweza kukukataa kufanyika kwa uchakataji huo wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa dpo@ada.com.
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako zilizofichwa utambulisho katika msingi ambao tunaunda takwimu unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitotumika tena kwa madhumuni haya.

3.9 Masoko ya moja kwa moja kwa bidhaa na huduma zetu zinazofanana

 • Aina za data: Anwani ya barua pepe, jina la maelezo mafupi, pendekezo la jinsia.
 • Matumizi ya data hizo: Kupokea matangazo ya moja kwa moja (bidhaa na huduma) au mawasiliano kuhusu utafiti wowote ambao tunaamini utakuwa na maslahi kwako. Unaweza kurekebisha mipangilio yako ya matangazo wakati wowote kwa kutumia kiungo kilicho chini ya kila barua pepe ya matangazo, au kutuma ombi lako la kujiengua kwa barua pepe kwenda dpo@ada.com.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR) / (Kifungu cha 7 Sehemu ya 3 UWG (Sheria ya Kijerumani dhidi ya Ushindani Usio wa Haki)).
 • Muda wa kuhifadhi: Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.

3.10 Kutoa huduma salama zaidi kwa kufuatilia matumizi ya App

 • Aina za data: Dalili za ugonjwa wako, uwezekano wa visababishi vya dalili za ugonjwa wako, Kitambulisho cha mtumiaji (itakapofaa), umri, jinsia, eneo (nchi), anwani ya IP, Kitambulisho cha kifaa.
 • Matumizi ya data hiyo: Tunatumia seti ndogo ya data ya utumiaji (pamoja na data ya afya binafsi) kufuatilia utumiaji ili kuhakikisha kuwa App yetu inakidhi viwango vya juu vya ubora na usalama vinavyohitajika kwa vifaa vya kitiba na kuboresha utendaji wa jumla wa App yetu.
  Tunatumia tu data ya utumiaji iliyoondolewa majina ambayo tunakusanya kupitia mchakataji wetu maalum, Amplitude Inc, 501 2nd Street, Suite 100 San Francisco, CA 94107, Marekani. Data iliyokusanywa katika muktadha huu haitumiki kuhusisha maelezo yoyote mafupi (profile) ya utumiaji na data zako binafsi. Data zako binafsi zitatumwa na kuhifadhiwa kwenye seva za Amplitude Inc. ambayo imeidhinishwa chini ya Ulinzi wa Faragha wa Mataifa ya Muungano wa Ulaya/Marekani (uamuzi wa utoshelevu wa Tume ya Ulaya). Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera ya faragha ya Amplitude: https://amplitude.com/privacy.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR). Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya ufuatiliaji wakati wowote kwenye mipangilio ya faragha katika App.
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa hadi wakati ambapo haitahitajika tena kwa dhumuni ambalo ilikusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data zako kwa dhumuni hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2. Unapoomba kufutwa kwa kesi mahsusi au ukifuta kesi katika App, data ya kesi yako haitatumika tena kwa kwa dhumuni hili.

3.11 Kuwasaidia watu duniani kote kupitia vipimo vya utendaji na tabia

 • Aina za data: Kitambulisho cha mtangazaji, upakuaji na usanikishaji wa App kwenye kifaa chako cha mkononi, maelezo ya namna ulivyofahamu kuhusu sisi (kwa mfano kupitia mitandao ya kijamii au makala ya mtandaoni), ikiwa usajili wako na uundaji wa kesi mpya kwenye App yetu ulifanikiwa, na ukadiriaji wako wa App yetu kwenye Maduka ya App, muda na tarehe.
 • Matumizi ya data hizo: Ikiwa unatumia App yetu, tunatumia maelezo tu (ambayo hayajumuishi data za afya binafsi) ili kuboresha mipango yetu ya masoko na kusaidia watu ulimwenguni kote kufikia App yetu. Tunatumia tu data ya utumiaji iliyoondolewa majina ambayo tunakusanya kupitia mchakataji wetu wa kandarasi adjust GmbH (Saarbrücker Str. 38a, 10405 Berlin, Ujerumani) kutupatia maarifa ya namna tunaweza kutoa Huduma zetu kwa watu duniani kote ambao bado hawazitumii, kwa wakati unaofaa, na kwa lugha inayofaa. Hatutogawa kamwe taarifa zako binafsi za afya kwa watengeneza matangazo au watu wengine kwa madhumuni haya, wala hatutatumia taarifa hizi kukuonyesha matangazo yoyote.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Idhini (Kifungu cha 6 (1) (a) GDPR).
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa hadi wakati ambapo haitahitajika tena kwa madhumuni ambayo ilikusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data yako kwa madhumuni haya unalingana na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.

3.12 Kufuatilia matumizi ili kuhakikisha utumiaji sahihi, utendaji, udumishaji na uboreshaji wa mfumo wetu wa fikra za kitiba na huduma nyingine husika

 • Aina za data: Kitambulisho cha kifaa, anwani yako ya IP, mfumo wa uendeshaji na aina ya kivinjari, urefu wa muda uliotumia kwenye kurasa fulani, na maelezo ya matumizi kwenye ukurasa, kama vile misogeo, ishara za vidole, mibofyo na matumizi ya kiteuzi, muda na tarehe.
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia kiasi kidogo cha data za utumiaji (ambacho hakijumuishi data za afya  binafsi) kuhakikisha utumiaji sahihi, utendaji, udumishaji na uboreshaji wa Huduma zetu kwa watumiaji wote.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea matumizi yaliyotajwa awali ya madhumuni hayo ya data. Hatutatumia data tuliyoikusanya kubaini utambulisho wako katika hali yoyote ile. Tunaweza kukutumia barua pepe za ushughulikiaji (kwa mfano, barua pepe ya uthibitisho wa uundaji wa akaunti, barua pepe ya kupanga upya nywila, barua pepe ya kukubali-mara mbili kuhusiana na kujisajili kwenye jarida, barua pepe ya ukaribisho) na kushughulikia mwingiliano wa ukurasa ipasavyo, ili kuhakikisha mapokezi sahihi na kutathmini huduma ili kuiboresha. Kwasababu zinazotokana na hali yako mahsusi, unaweza kukataa kufanyika kwa uchakataji huo wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa dpo@ada.com (unaweza kupata maelezo zaidi katika sehemu ya 8).
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa mpaka itakapokuwa haihitajiki tena kwa malengo iliyokusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data yako kwa madhumuni haya unakwenda  sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.

3.13 Ripoti za utendaji

 • Aina za data: Hitilafu, ripoti za kuacha kufanya kazi, na anwani ya IP, muda na tarehe.
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia data zilizo hapo juu (ambazo hazijumuishi data za afya binafsi) ili kuhakikisha utendaji wa Huduma zetu. Huduma zetu haziwezi kufanya kazi vizuri bila uchakataji huu. Tunatumia tu data ya utumiaji ya majina bandia ambayo tunakusanya kupitia huduma ya “Sentry” ya Programu yetu ya mchakataji wetu wa kandarasi Functional Software Inc., 132 Hawthorne Street, San Francisco, California 94107 Marekani. Data hii itatumwa na kuhifadhiwa kwenye seva za Functional Software Inc. ambazo zimethibitishwa chini ya Ulinzi wa Faragha wa Mataifa ya Umoja wa Ulaya/Marekani (uamuzi wa utoshelevu wa Tume ya Ulaya). Ili upate maelezo zaidi, tafadhali tazama sera ya faragha ya Sentry: https://sentry.io/privacy/.
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea matumizi yaliyotajwa awali ya madhumuni hayo ya data. Hatutatumia data tuliyokusanya kubaini utambulisho wako katika hali yoyote ile. 
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itaondolewa baada ya siku 14, isipokuwa tukio linalohusiana na usalama likitokea (kwa mfano, shambulio Pana la Kufungwa kwa Huduma). Tukio linalohusiana na usalama likitokea, faili za kumbukumbu za seva zitahifadhiwa hadi tukio hili linalohusiana na usalama limeondolewa na kufafanuliwa kabisa.

3.14 Maoni / Uchunguzi

 • Aina za data: nakala ya maoni, anuani ya barua pepe, (hiari), data zilizotolewa kwenye kesi (kama tu umetupa anwani yako ya barua pepe inayoturuhusu kukutambua, kwa madhumuni tu yaliyoainishwa hapo chini).
 • Matumizi ya data hizo: Tunatumia maoni unayoweza kutupa (hiari) kuchanganua ikiwa umeridhika au haujaridhika na bidhaa na huduma zetu, na kutathmini mtazamo wako kwa ujumla. Hii ni nyenzo ya msingi kwetu katika kuboresha urahisi wa utumiaji wako na kurekebisha matendo yetu kulingana na mahataji yako. Tunaweza pia kutumia maoni unayoweza kutupatia (hiari) kukuhakikishia viwango vya juu vya ubora na usalama wa Huduma zetu, kama ilivyoelezewa katika Sehemu ya 3.5 hapo juu. 
 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR). Maslahi yetu halali yanategemea matumizi yaliyotajwa awali ya madhumuni hayo ya data. Katika hali yoyote ile hatutatumia data tuliyokusanya kubaini utambulisho wako // Maoni yako yanaweza kuchakatuliwa ili kutekeleza hitaji la lazima la viwango vya ubora na usalama wa Huduma zetu ambazo zinatupa sifa za kutambulika kama kifaa cha kitiba chini ya sheria za kifaa cha tiba, kama ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 3.5 hapo juu. 
 • Muda wa kuhifadhi: Data yako itahifadhiwa mpaka itakapokuwa haihitajiki tena kwa lengo ililokusanyiwa. Muda wa kuhifadhi data zako kwa lengo hili unakwenda sambamba na kipindi cha uchakataji kwa mujibu wa Sehemu ya 3.2.

4. Vidakuzi na ufuatiliaji kwenye Tovuti yetu

Tovuti yetu hutumia vinavyojulikana kama “vidakuzi”. Vidakuzi ni faili za maandishi zilnazohifadhiwa kwenye kivinjari cha Intaneti au na kivinjari cha Intaneti kwenye kifaa cha mtumiaji (kompyuta, kompyuta kibao au simu). Tunatumia neno “vidakuzi” kurejelea vifaa vyote ambavyo vinakusanya data kwenye Tovuti yetu (k.m. anwani za IP, mahali na wakati watumiaji wanatembelea tovuti). Data ya watumiaji inayokusanywa kwa njia hii haitambuliwi kwa majina yao. Data haihifadhiwi pamoja na data nyingine binafsi ya mtumiaji. Uchakataji huu hufanywa kwa msingi wa kisheria au, inapohitajika kisheria, kwa mujibu wa idhini yako. 

Ili upate maelezo ya kina kuhusu ufuatiliaji wa watumiaji wetu na vidakuzi tunavyotumia, madhumuni ya kuvitumia na kudhibiti mapendeleo yako ya Vidakuzi, rejelea Sera ya Vidakuzi.

5. Tunahifadhi wapi data zako binafsi

Data binafsi ambazo tunakusanya kutoka kwako huhifadhiwa katika Umoja wa Ulaya kwenye Cloud Servers za Amazon Web Services EMEA S.A.R.L. (“AWS”) zenye makao ya kibiashara nchini Luxembourg na kwenye Cloud Servers za Google Commerce Limited (“GCL”), kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Ireland, yenye ofisi zake katika Gordon House, Mtaa wa Barrow, Dublin 4, Ireland. Hata hivyo, data hizi zinaweza kuchakatwa na wachakataji wadogo wanaofanya kazi nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya (“EEA”) kulingana na makubaliano ya uchakataji wa data ikiwa masharti ya ziada ya Kifungu cha 44 (na kadhalika) GDPR kuhusu uchakataji katika nchi nyingine unaambatana na kiwango sahihi cha ulinzi katika nchi nyingine na uhakikisho muafaka chini ya Kifungu cha 46 GDPR (kama vile vifungu vya kawaida vya ulinzi wa data, au hali za kipekee chini ya Kifungu cha 49 GDPR).

Maelezo nyeti yanayotumwa kutoka kivinjari chako na Tovuti yetu hutumwa yakiwa yamesimbwa kwa kutumia Usalama wa Safu ya Kutuma (“TLS”). Wakati wa kutuma maelezo nyeti, unapaswa kuhakikisha kuwa kivinjari chako kinaweza kuthibitisha cheti chetu.

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu usalama maalum unaotumika wakati wa kutuma data zako binafsi nje ya EEA.

6. Kufichuliwa kwa data zako binafsi

6.1 Tunatumia watoa huduma za kiufundi kuendesha na kudumisha Huduma zetu, ambao hutumika kama wachakataji wetu kulingana na makubaliano ya uchakataji wa data.
Orodha nzima ya wachakataji wetu wengine, wanaochakata data zako binafsi kwa niaba yetu na kwa udhibiti mkali kwa mujibu wa Sehemu ya 3 hapo juu inaweza kupatikana hapa.
Watoa huduma ambao huchakata data binafsi kwa niaba yetu nje ya EEA (au “nchi nyingine”) watatumika tu ikiwa mpokeaji amepokea Uamuzi wa Tume ya Ulaya kuhusu ufaafu au dhamana mwafaka au zinazofaa kwa nchi hii nyingine. Isitoshe, hatutatuma data zako binafsi kwa watu wengine - isipokuwa kwa madhumuni yaliyoorodheshwa hapa chini.

 • Uhalalishaji wa matumizi: Msingi wa kisheria wa kutuma data binafsi kwa mchakataji na uchakataji unaofanywa na mchakataji unategemea msingi wa kisheria ambao sisi, kama wadhibiti wa data, tunategemea (rejelea sehemu ya 3 hapo juu)..

6.2 Ikiwa tunauza au kununua biashara au mali yoyote, tunaweza kufichua data zako binafsi kwa muuzaji mtarajiwa au mnunuzi wa biashara au mali hiyo.

 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR) (ya kuuza biashara au mali yetu)/ inapohitajika na sheria husika: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR (kwa data za afya binafsi).

6.3 Ikiwa sisi au, kwa kiasi kikubwa, mali zetu zote zitanunuliwa na mtu mwingine, data binafsi kuhusu watumiaji wetu zitakuwa moja ya mali zitakazohamishwa.

 • Uhalalishaji wa matumizi: Maslahi halali (Kifungu cha 6 (1) (f) GDPR) (kuuza Kampuni au mali yetu)/ inapohitajika na sheria husika: Idhini (Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR (kwa data za afya binafsi).

6.4 Ikiwa tunalazimika kwa mujibu wa sheria za EU au sheria za nchi Mwanachama kufichua au kushiriki data zako binafsi.

 • Uhalalishaji wa matumizi: Wajibu wa kisheria, Kifungu cha 6 (1) (c) GDPR.

6.5 Tunaweza kufichua data fulani kwa mashirika yanayojishughulisha na majaribio ya kitiba na aina nyingine za utafiti pale mbapo umeturuhusu waziwazi kufanya hivyo.

 • Uhalalishaji wa matumizi: Idhini Kifungu cha 9 (2) (a) GDPR.

6.6 kiwa unatumia Huduma zetu kupitia programu iliyopachikwa kwenye tovuti (web-embed application) iliyopo Marekani, tunaweza kufichua data fulani kwa mshirika ambaye ni mwenyeji wa programu hiyo ya kwenye tovuti, kama inavyohitajika kwenye  Sheria ya Marekani ya Utoaji wa Bima ya Afya na Uwajibikaji (“HIPAA”) au sheria nyingine zozote husika. 

 • Uhalalishaji wa matumizi: Wajibu wa kisheria, Kifungu cha 6 (1) (c) GDPR.

6.7 Ikiwa unatumia Kifaa chetu cha Ukaguzi (Screening Tool), tunaweza kufichua data fulani kwa mshirika ambaye ni mwenyeji wa Kifaa hicho cha Ukaguzi, ikiwa ni lazima kwa utendaji wa jukumu linalotekelezwa kwa maślahi ya jamii, na sikuzote katika kutii sheria husika (kwa mfano, inajumuisha lakini haiishii kwenye GDPR na Sheria ya Kijerumani ya Kinga ya Maambukizi (“IFSG”)).

 • Uhalalishaji wa matumizi: Wajibu wa kisheria, Kifungu cha 6 (1) (c) GDPR / Maslahi ya jamii, Kifungu cha 6 (1) (e) GDPR.

7. Tunahifadhi data zako binafsi kwa muda gani?

Tutahifadhi data zilizo hapo juu kwa muda mrefu kiasi inavyohitajika ili kukupa Huduma, kushughulikia maswala yoyote mahsusi ambayo yanaweza kutokea au, vinginevyo, kama inavyohitajika na sheria au chombo chochote husika cha usimamizi wa sheria. Vipindi maalum vya kuhifadhi kuhusiana na shughuli za uchakataji vimeelezewa kwa kina katika Sehemu ya 3 hapo juu.

Baada ya akaunti yako kufungwa, tutafuta data binafsi zinazohusiana na akaunti yako ndani ya mwezi 1. 

Ikiwa ulikuwa mtumiaji wa huduma za UK Doctor Chat (ambazo hazipatikani tena tangu tarehe 23 Machi 2018), maelezo yako ya mashauriano yanaweza kuhifadhiwa na sisi kwa kipindi cha hadi miaka 10 kulingana na Ratiba ya Kuhifadhi ya Maadili ya Usimamizi wa Rekodi nchini Uingereza, au ikiwa inahitajika vinginevyo na Tume ya Ubora wa Huduma “CQC”).

Ikiwa data yako binafsi itatumiwa kwa sababu mbili tofauti, tutaihifadhi hadi madhumuni ya kipindi kirefu zaidi yakamilike, lakini tutaacha kuitumia kwa madhumuni ya kipindi kifupi mara tu kipindi hicho kifupi kitakapomalizika.

Tunadhibiti ufikiaji wa data yako binafsi kwa watu isipokuwa tu wale wanaohitaji kuitumia kwa dhumuni/ madhumuni husika. Vipindi vyetu vya kuhifadhi vinategemea mahitaji ya kibiashara yenye mashiko, na data yako ya binafsi ambayo haihitajiki tena aidha inafichwa utambulisho na kutoweza kutambulika tena kwa jina (na data iliyofichwa utambulisho inaweza kuhifadhiwa) au kuharibiwa kwa njia salama.

8. Haki zako

Chini ya GDPR, una haki mbalimbali kuhusiana na data zako binafsi (kama ilivyoorodheshwa hapa chini).

Haki hizi zote zinaweza kutekelezwa kwa kuwasiliana nasi kupitia dpo@ada.com.

Verification: in order to verify your request, we will take reasonable steps such as asking you to send us a confirmation from the email address associated with your account, so that we can verify that you are the owner of this email account. If there is no email address associated with your account, we may ask you for proof of ID.

 • Haki ya kuondoa idhini: Una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote kwa kutuarifu kwa barua pepe kupitia anwani ifuatayo: dpo@ada.com. Kwa kuondoa idhini yako, uhalali wa kuchakata maelezo kwa mujibu ya idhini ulliyotoa hadi wakati wa kujiondoa hautaathiriwa. 
 • Haki ya kupinga: Una haki ya kupinga chini ya masharti ya Kifungu cha 21 DSGVO. Utapata maelezo zaidi hapa chini:
  Haki ya kupinga ambapo uchakataji unategemea msingi wa maslahi halali: Kama mtoaji data, una haki ya kupinga, kwa misingi inayohusiana na hali yako maalum, wakati wowote, uchakataji wa data yako ya kibinafsi kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) (e) au (f) GDPR, pamoja na kupinga kupangwa kwa maelezo kwa msingi wa vifungu hivyo. Pingamizi linalohusiana na hali yako likitokea, hatutachakata tena data yako ya kibinafsi isipokuwa kama tunaweza kuonyesha sababu mwafaka za kuchakata data ambazo zinazidi maslahi yako, haki na uhuru au ili kuanzisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria. 
  Haki ya kupinga ikiwa tunachakata data yako binafsi kwa madhumuni ya kuzalisha takwimu: Ikiwa tutachakata data yako ya kibinafsi kwa sababu za kuzalisha takwimu kulingana na Kifungu cha 9 (2) (j) DSGVO, Sehemu ya 27 (1) BDSG, una haki ya kupinga uchakataji kama huu kwa sababu zinazotokana na hali yako maalum. Pingamizi kama hilo likitokea, hatutachakata tena data binafsi husika kwa madhumuni haya isipokuwa kama uchakataji unahitajika kutimiza jukumu la manufaa kwa jamii, au usitishaji wa uchakataji kunaweza kuzuia au kuathiri sana utekelezaji wa madhumuni ya kitakwimu na kuendeleza uchakataji kunahitajika ili kutimiza madhumuni ya kitakwimu.
  Haki ya kupinga matangazo ya moja kwa moja: Pale data zako binafsi zitachakatwa kwa madhumuni ya matangazo ya moja kwa moja, una haki ya kupinga wakati wowote uchakataji wa data zako binafsi kwa madhumuni ya matangazo ya aina hiyo, ikijumuisha kupanga maelezo kwa kiwango ambacho kinahusiana na matangazo ya moja kwa moja ya aina hiyo. Ikiwa utapinga uchakataji kwa madhumuni ya matangazo ya moja kwa moja, hatutochakata tena data zako binafsi kwa madhumuni haya. Ili kutumia haki zako za pingamizi, unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa dpo@ada.com
 • Haki ya kufahamishwa: Kama mtoaji data, una haki ya kufikia data na kupata maelezo kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 15 GDPR. Hii inamaanisha hasa kwamba una haki ya kupata uthibitisho kutoka kwetu kuhusu kama tunachakata data zako binafsi. Ikiwa ni hivyo, pia una haki ya kuwezeshwa kufikia data binafsi na maelezo yaliyoorodheshwa katika kifungu cha 15 (1) GDPR. Hii inajumuisha maelezo kuhusu madhumuni ya uchakataji, aina za data binafsi ambazo zinachakatwa, pamoja na wapokeaji au aina za wapokeaji ambao wamepewa au watapewa data binafsi.
 • Haki ya kufuta / ‘Haki ya kusahaulika’: Kama mtoaji data, una haki ya kufuta (“haki ya kusahaulika”) chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 17 GDPR. Hii inamaanisha kwamba kwa ujumla una haki ya kupata kutoka kwetu ufutwaji wa data yako binafsi na tunawajibika kufuta data zako binafsi bila kukawia pasipo sababu wakati sababu moja iliyoorodheshwa katika kifungu cha 17 (1) GDPR imetimia. Unaweza kufanya hivyo kwa kufuta akaunti yako wakati wowote. Ikiwa tumeweka data binafsi hadharani na tunawajibika kuifuta, tunawajibika pia, kwa kuzingatia teknolojia iliyopo na gharama ya utekelezaji, kuchukua hatua stahiki, ikijumuisha hatua za kiufundi, kuwataarifu wadhibiti wanaochakata data binafsi ambayo umeomba wadhibiti hao wafute viungo vyovyote vya maelezo, au kunakili au kurudufisha data hizo binafsi (Kifungu cha 17 (2) cha GDPR. Isipokuwa, haki ya kufuta (“Haki ya kusahaulika”) haitekelezeki ikiwa uchakataji ni lazima kwa moja ya sababu zilizoorodheshwa katika Kifungu cha 17 (3) GDPR. Hii inaweza kuwa hivyo, kwa mfano, ikiwa uchakataji ni lazima katika kutimiza wajibu wa kisheria au kuanzisha, kutumia, au kulinda madai ya kisheria (Kifungu cha 17 (3) (b) na (e) GDPR).
 • Haki ya kuzuia uchakataji: Kama mtoaji data, una haki ya kuzuia uchakataji kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 18 GDPR. Hii inamaanisha kuwa una haki ya kupata kutoka kwetu uzuiaji wa uchakataji wakati sababu moja iliyoorodheshwa katika kifungu cha 18 (1) GDPR imetimia. Hili linaweza kutokea, kwa mfano, ikiwa unapinga usahihi wa data binafsi. Katika hali kama hiyo, hatua ya kuzuia uchakataji hudumu kwa kipindi ambacho kinatuwezesha kuthibitisha usahihi wa data binafsi (Kifungu cha 18 (1) (a) GDPR). Kuzuia kunamaanisha kuwa data binafsi zilizohifadhiwa huwekwa alama kwa lengo la kuzuia uchakataji wake wa baadaye (Kifungu cha 4 Nambari 3 GDPR).
 • Haki ya kuhamisha data: Kama mtoaji data, una haki ya kuhamisha data kwa mujibu wa masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 20 GDPR. Hii inamaanisha kuwa kwa ujumla una haki ya kupokea data zako binafsi ambazo umetupatia katika muundo, unaotumika kwa kawaida, na unaosomeka na kompyuta na kuzipeleka data hizo kwa mdhibiti mwingine bila kipingamizi kutoka kwetu ikiwa uchakataji umetokana na idhini kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) (a) au Kifungu cha 9 (2) GDPR au kwa mkataba kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (1) (a) GDPR na uchakataji unafanyika kwa njia za kiotomatiki (kwa kompyuta) (Kifungu cha 20 (1) GDPR). Katika kutumia haki yako ya kuhamisha data, pia una haki kwa ujumla ya kutaka data zako binafsi kuhamishwa moja kwa moja kutoka kwetu kwenda kwa mdhibiti mwingine ikiwa inawezekana kiufundi (Kifungu cha 20 (2) GDPR). 
 • Haki ya Marekebisho: Kama mtoaji data, una haki ya kurekebisha maelezo chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 16 GDPR. Hii inamaanisha hasa kwamba una haki ya kupokea kutoka kwetu, bila kuchelewa, marekebisho ya makosa katika data zako binafsi na kukamilishwa kwa data binafsi ambazo hazikukamilika.
 • Haki ya kulalamika: Kama mtoaji data, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usimamizi chini ya masharti yaliyotolewa katika Kifungu cha 77 GDPR. Mamlaka ya usimamizi inayohusika na masuala yetu ni Mamlaka ya Ulinzi wa Maelezo ya Berlin nchini Ujerumani (Berliner Beauftragte für Datenschutz und Informationsfreiheit, Anwani: Friedrichstr. 219, 10969 Berlin; Simu: 030 13889-0; Barua-pepe: mailbox@datenschutz-berlin.de).

Kutuomba tuache kuchakata data zako binafsi au kufuta data zako binafsi itaelekea kumaanisha kama hauwezi tena kutumia Huduma zetu, au angalau hautoweza kutumia sehemu za Huduma ambazo zinahitaji uchakataji wa aina za data binafsi ambazo umetuomba tufute, hatua ambayo inaweza kusababisha usiweze kutumia tena Huduma.

9. Taarifa ya Faragha kwa wakazi wa California

Ikiwa wewe ni mkazi wa California, Sheria ya California inatulazimu kukupatia maelezo kadhaa ya ziada kuhusiana na haki zako kwa kuzingatia “maelezo yako binafsi” (kama ilivyofasiliwa katika Sheria ya Faragha ya Mtumiaji (hapa itafahamika baadaye kama “CCPA”) ambayo imeanza kutekelezwa Januari 1, 2020).

Hatuku uza au kuhamisha data zako binafsi kwa watu wengine katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, hatufanyi hivyo sasa, na hatutofanya hivyo baadaye (na hatutofanya hivyo kamwe bila kukupatia haki ya kukataa).

Tunaweza kuhamisha data zako binafsi kwa wachakataji wengine ili kufanikisha madhumuni ya uchakataji yaliyoorodheshwa katika Sehemu ya 3 hapo juu, lakini tutafanya hivyo kwa kushirikiana na wachakataji wengine embao tuna makubaliano nao ya ulinzi wa data. Orodha kamili ya wachakataji wetu wengise inaweza kupatikana hapa.

CCPA inawapa watumiaji wa California haki zifuatazo (ambapo haingiliani na GDPR)):

 • Haki ya kuomba kufichua taarifa yoyote binafsi tuliyokusanya (Kifungu cha (1789.100) (a) CCPA). Hii inamaanisha kwa ujumla kwamba unayo haki ya kuomba kufichuliwa kwa aina ya taarifa binafsi tuliyokusanya kutoka kwako, pamoja na aina ya vyanzo vilivyotumika kupata taarifa hiyo, dhumuni la ukusanyaji, aina ya watu wengine ambao tumeshirikisha kwenye taarifa yako binafsi, na vipande maalum vya taarifa binafsi ambayo tumekusanya (Kifungu cha 1798.110 (a) CCPA).
 • Haki ya kuomba kufutwa kwa taarifa yoyote binafsi ambayo tulikusanya kutoka kwako (Kifungu cha 1798.105) CCPA). Hii inamaanisha kwamba baada ya kuthibitisha ombi lako la kutaka kufuta taarifa yako binafsi, tutaifuta taarifa hiyo kutoka kwenye rekodi zetu na kumuelekeza mtoa huduma wa moja kwa moja yoyote kufuta taarifa yako binafsi kutoka kwenye rekodi zao, isipokuwa wakati Kifungu cha 1798.105 (d) kinahusika (kwa mfano, taarifa binafsi ni ya lazima ili kutoa huduma, kubaini matukio ya kiusalama, kubaini na kukarabati makosa ambayo yanaharibu utendaji uliokusudiwa wa App, kufanya utafiti wa takwimu kwa maslahi ya jamii, au kutimiza wajibu wa kisheria).

Pamoja na uwezekano wa kuwasiliana nasi kwa kutuma barua pepe kwa dpo@ada.com, unaweza kutumia haki zozote chini ya CCPA au kuomba maelezo zaidi kuhusiana na haki zako kwa kutupigia simu kupitia namba ya dharura.

10. Mabadiliko kwenye sera hii

Mabadiliko yoyote ambayo tutafanya kwa Sera yetu ya Faragha katika siku zijazo yatachapishwa kwenye ukurasa huu, na inapofaa, utafahamishwa kwa barua pepe au taarifa kupitia App. Kwa hivyo tunakuhimiza uisome mara kwa mara ili uendelee kupata maelezo kuhusu jinsi tunavyochakata data zako.