Ubora wa kitiba

Tafiti za kitiba zinaonyesha ubora wa kitiba unatofautiana kati ya machaguo ya mshirika wako wa teknolojia ya afya. Hivi ndivyo njia yenye ushahidi inaweza kukusaidia kufanya chaguo sahihi.

Mambo ya kuzingatia

Nguzo zetu 5 za ubora wa kitiba ni msingi wa masuluhisho yetu ya biashara ya afya.

  • CE kifaa cha kitiba daraja la I, Daraja la II inasubiri uamuzi
  • Cheti cha ISO 27001 (Usimamizi wa InfoSec)
  • Cheti cha ISO 13485
  • Inatekeleza matakwa ya GDPR
  • Inatekeleza matakwa ya HIPAA
  • Viongozi wa kikundikazi:  Mpango wa WHO wa kusanifisha alama teule

Kwanini ubora wa kitiba ni muhimu

 • Utawala wa kitiba na udhibiti wa tasnia huleta michakato huru ya kudhibiti ubora unayoweza kuiamini.

 • Uzoefu mzuri wa mtumiaji inamaanisha watu hutoa maoni sahihi ili kupata mwongozo sahihi kutoka kwenye teknolojia.

 • Uwepo wa taarifa pana za magonjwa inamaanisha magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida (adimu) hayakosi kutambuliwa au kutambuliwa kimakosa.

 • Usahihi wa kitiba unaweza kusaidia kupunguza muda wa kugundua ugonjwa ili kuharakisha matibabu.

 • Usalama wa ushauri unaweza kusaidia kuhakikisha wataalamu wa huduma za afya wanawaona wagonjwa wanaohitaji huduma zao zaidi katika mpangilio sahihi.

Jinsi AI ya Ada inavyofanya kazi

Awali iliundwa kusaidia ufanyaji wa maamuzi ya kitiba, madaktari wetu waliunda Ada ili ifikiri kama daktari. Usahihi wa kitiba na usimamizi wa kitiba kutoka kwa madaktari wa kibinadamu umekuwa kwenye DNA yetu tangu mwanzo kabisa. Wafahamu baadhi ya wataalamu wetu wa tiba.

Endelea kusoma

Wezeshwa na Ada

Toa matokeo bora zaidi kupitia masuluhisho ya biashara yaliyo na nguvu.

Pata maelezo zaidi

 1. Miller, S., Gilbert, et al. JMIR (2020), doi: 10.2196/19713.

 2. Scheder-Bieschin, J., et al. (2020), doi: 10.1101/2020.11.13.20230953.

 3. Gilbert, S. et al. BMJ Open, (2020). doi: 10.1136/bmjopen-2020-040269.

 4. Ronicke, S. et al. Orphanet. (2019). doi: 10.1186/s13023-019-1040-6.

 5.  Morse, K. et al. J Med Internet Res, (2020). doi: 10.2196/20549.