Mpango Wetu wa Afya Duniani

Mpango Wetu wa Afya Duniani

Shirikiana nasi kutengeneza dunia isiyo na ubaguzi wa afya

Watu bilioni nne, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani, hawana huduma za msingi za afya. Hasara za changamoto hii ya afya duniani zinawakabili zaidi watu katika nchi za kipato cha chini na cha kati (LMICs). Mpango Wetu wa Afya Duniani unachangia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kwa kutumia teknolojia ya Ada kwa manufaa ya dunia. Tunakaribisha ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), serikali za nchi za kipato cha chini na cha kati (LMICs), na mashirika ya kimataifa ya afya ili kutusaidia kuongeza upatikanaji wa taarifa za afya za kibinafsi na kuboresha utoaji wa huduma ya msingi ya afya kwa wale ambao wanaihitaji zaidi.

Changamoto ya afya duniani

Changamoto ya afya duniani
 • Ukosefu wa Upatikanaji wa Huduma za Afya

  Watu bilioni 4 wanakosa upatikanaji wa huduma za msingi za afya

 • Mhudumu wa Afya

  Milioni 7 ya upungufu wa wahudumu wa afya duniani

 • Eneo la Kijijini

  Watu 75% wanaishi maeneo ya vijijini katika nchi zinazoendelea

 • Daktari wa magonjwa ya akili

  Daktari wa magonjwa ya akili .05 kwa kila watu 100,000 katika nchi za kipato cha chini na cha kati (LMICs)

Fursa za afya ya kidijitali

Fursa za afya ya kidijitali
 • Simujanja

  Watu 42% katika nchi za LMIC walimiliki simujanja (smartphone) mwaka 2017

 • Uwekezaji

  Uwekezaji wa kila mwaka wa dola bilioni 30 za Marekani kwenye afya ya kidigitali kufikia mwaka wa 2020

 • Mhudumu wa Afya kwenye Mtandao

  Milioni 21.2 ya wahudumu wa afya ya jamii ifikapo mwaka wa 2030

 • App za Simujanja

  $2 za Marekani kwa kila mtu kwa mwaka ili kuboresha afya ya akili ya watu wa nchi za LMIC

Maeneo tunayowekea msisitizo

Afya ya familia

Wahudumu wa afya ya jamii

Afya ya akili

Angalia kujifunza zaidi

Afya ya dunia na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko

Ada hutoa ufahamu wa ndani katika muda halisi wa watu kwa njia ya ukusanyaji wa takwimu za wagonjwa, ambao majina yao yamefichwa (anonymous). Kadri Ada inavyoendelea kwa kasi kuwa rafiki wa watu duniani katika afya, takwimu hizi zinahudumu kama darubini kwa watunga sera kukadiria mahitaji ya afya ya jamii, kutambua mienendo, na kudhibiti milipuko ya magonjwa.

Jumuiya yetu

Tunawekeza kwenye Akili Bandia (AB) kama suluhisho la upungufu wa idadi ya wahudumu wa afya duniani na hitaji la haraka la kuboresha afya ya mtoto na kijana. Ushirikiano wetu unakabiliana na hitaji hili ndani ya Afrika ya Mashariki na Rumania, kwa kuleta athari chanya kwa vijana na pia ufahamu kwa Fondation Botnar na Ada ili kutanua hii mbinu ya kibunifu kwenye nchi nyingine za kipato cha chini na cha kati.

Dk. Stefan Germann, Afisa Mkuu Mtendaji wa Fondation Botnar
Dr. Stefan Germann, CEO Fondation Botnar

Shirikiana nasi

Kuna njia nyingi za kuweza kufanya kazi pamoja kutengeneza athari chanya kwa watu walio kwenye mazingira ya kudhurika kirahisi. Mashirika ya Fondation Botnar na Bill & Melinda Gates tayari yanaunga mkono kazi yetu. Kama ungependa kujiunga nasi ili kuongeza upatikanaji wa taarifa za afya za kibinafsi na kuboresha utoaji wa huduma ya msingi ya afya kwa wale wanaoihitaji zaidi, tafadhali wasiliana na Hila Azadzoy, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wetu wa Afya Duniani (Global Health Initiative).

Hila Azadzoy
Mkurugenzi Mtendaji, Global Health Initiative
globalhealth@ada.com

Jifunze zaidi


Shirika la Fondation Botnar
Massachusetts Institute of Technology
Shirika la Bill & Melinda Gates
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Muhimbili