Sera ya Kidakuzi ya Ada Health GmbH

Ilibadilishwa mwisho: 23 Juni 2022

Ada Health GmbH (“Ada”, “sisi”, au “yetu”) inatumia vidakuzi na vifaa vinavyofanana na hivyo katika tovuti yake ya ada.com (“Tovuti”) ili kusaidia kukupatia Tovuti , rafiki, rahisi kutumia, salama na yenye ufanisi. Sera hii inaeleza namna tunavyofanya hivyo.

Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya ufuatiliaji wakati wowote kupitia .

1. Maelezo ya jumla kuhusu vidakuzi

Vidakuzi ni faili ndogo za maandishi ambazo tovuti inaweza kuhifadhi katika kifaa chako unapoitembelea kwa mara ya kwanza. Kidakuzi husaidia tovuti kutambua kifaa chako unapoitembelea mara nyingine. Tunatumia neno “vidakuzi” katika sera hii kumaanisha faili zote zinazokusanya maelezo kwa njia hii.

Kuna kazi nyingi vidakuzi hutekeleza. Kwa mfano, vinaweza kutusaidia kukumbuka jina lako la mtumiaji na vitu unavyopendelea, kuchanganua ubora wa utendaji kazi wa tovuti, au hata kuturuhusu kupendekeza maudhui tunayoamini yatakufaa zaidi.

2. Tovuti hii hutumia aina gani ya vidakuzi?

Kwa jumla, vidakuzi vyetu hutekeleza angalau mojawapo wa ya kazi zifuatazo:

  • Lazima. Vidakuzi vya lazima ni muhimu ili kukupatia Huduma zetu. Vinawezesha kazi za msingi kama vile kuvinjari kwenye ukurasa na kufikia sehemu salama za Huduma.
JinaMtoa hudumaDhumuniMwishoAina
cookie_settingsada.comHuwezesha tovuti kuhifadhi maamuzi ya watumiaji kuhusu matumizi ya vidakuzi katika tovuti.Siku 365HTTP Cookie
locale_redirectedada.comHuwezesha tovuti kutambua kama mtumiaji ameshaelekezwa kwenye lugha yake ili kuzuia uelekezaji mwingine wa moja kwa moja.Siku 365HTTP Cookie
recent_help_articlesada.comHuwezesha tovuti kuhifadhi makala 5 za mwisho zilizopitiwa ili kurahisisha matumizi ya mtembeleaji wa tovuti. Taarifa hii inahifadhiwa na kutumika tu kwenye kifaa.Siku 365HTTP Cookie
  • Takwimu na Utendaji. Vidakuzi vya takwimu na utendaji husaidia wamiliki wa tovuti kuelewa jinsi watumiaji hutumia tovuti kwa kukusanya na kutoa ripoti ya matumizi.
JinaMtoa hudumaDhumuniMwishoAina
_pk_id#ada.comHuandikikisha kitambulisho (ID) cha kipekee kinachotumika kutoa data ya kitakwimu kuhusu jinsi mtumiaji anavyotumia tovuti kupitia Matomo.Siku 365HTTP Cookie
_pk_ref#ada.comInatumiwa na Matomo kuhifadhi taarifa za sifa/tabia.Siku 180HTTP Cookie
_pk_ses#ada.comInatumiwa na Matomo kuhifadhi kwa muda data za mtembeleaji wa tovuti.Dakika 30HTTP Cookie
_pk_cvar#ada.comInatumiwa na Matomo kuhifadhi kwa muda data za mtembeleaji wa tovuti.Dakika 30HTTP Cookie
  • Masoko. Vidakuzi vya masoko hutumika kufuatilia watembeleaji wa tovuti na maeneo wanayobofya wakiwa kwenye tovuti. Kusudi lake ni kuwa na matangazo yenye walengwa na kupima ufanisi wa kampeni zetu.

Tovuti hii haitumii vidakuzi vyovyote vya masoko kwa wakati huu.

3. Vifaa vya watoa huduma wengine vinavyotumika katika Tovuti yetu

Tunatumia au kuruhusu mtoa huduma mwingine afuataye kutumia vidakuzi ambavyo vipo katika makundi yaliyoainishwa hapo juu:

Matomo Cloud. Tunatumia Matomo Cloud (Matomo), huduma ya uchanganuzi wa wavuti ya “InnoCraft Ltd” (7 Waterloo Quay PO625, 6140 Wellington, New Zealand) kwa dhumuni la kuzifanya tovuti zetu kuwa katika muundo unaoendeana na mapendeleo yako kama mtumiaji na kuendelea kufanya maboresho. Data za Matomo zimehifadhiwa nchini Ujerumani. Vidakuzi vinaweza kutumika katika muktadha huu. Vidakuzi hivi hutathmini jinsi unavyotumia tovuti yetu - kama mtumiaji asiyetambulika (data zinazokusanywa hazifichui utambulisho wako). Pia, data husika hazitolewi kwa washirika wengine au kutumika kwa madhumuni mengine yoyote.  

Taarifa zinazotokana na vidakuzi ni hizi zifuatazo:

  • aina/toleo la kivinjari,
  • mfumo wa uendeshaji unaotumika,
  • URL ya refari (tovuti ya mwisho kutembelea),
  • jina la kompyuta inayotumika kufikia (anwani ya IP – anwani za IP huondolewa utambulisho ili zisihusishwe na mtu yeyote maalum [ kufunikwa kwa IP]),
  • wakati wa ombi la seva.

Unaweza kuzuia usakinishaji wa vidakuzi kwa kupangilia programu ya kivinjari chako ipasavyo. Hata hivyo, kutokana na mipangilio hiyo, huenda usiweze kutumia kikamilifu vipengele vya Tovuti. 

Maelezo zaidi kuhusu faragha inayohusiana na matumizi ya Matomo yanaweza kupatikana hapa:Matomo na faragha.

4. Haki ya kukataa

Zaidi ya haki yako ya kukataa kwa mujibu wa Kifungu cha 21 GDPR, unaweza kukataa kukusanywa na kuchakatwa kwa maelezo ya ufuatiliaji kwa kufuata maagizo ya kujiondoa ya mtoa huduma husika kama ilivyoelezwa hapo juu.

Aidha, ikiwa ungependa kuzima vidakuzi basi unaweza kufanya hivyo kwa kubadilisha mipangilio katika kivinjari au simu yako ya mkononi. Tafadhali kumbuka kuwa iwapo utachagua kuzima vidakuzi, unaweza kukuta kwamba vipengele fulani vya tovuti haviyafanyi kazi vizuri.

Kwa maelezo zaidi kuhusu haki zako chini ya Kanuni za Jumla za Ulinzi wa Data na namna tunavyochakata data katika huduma zetu, rejea Sera yetu ya Faragha.