Vigezo na Masharti ya Ada Health

Imebadilishwa mwisho: 05 Juni 2020

1. Karibu katika Ada

1.1. Karibu katika Ada. Vigezo na Masharti yafuatayo (ambayo yanajulikana hapa kama “Vigezo na Masharti”) yanaunda sehemu ya makubaliano kati yako na Ada Health GmbH (ambayo inajulikana hapa kama “Ada”,”sisi”, au “yetu”), mwendeshaji wa jukwaa ambalo hukuwezesha, (utatambuliwa hapa kama “wewe”, “yako” au “mtumiaji”), kumfikia rafiki yetu katika afya (health companion) bila malipo, matumizi ya tathmini ya dalili, na huduma zozote husika. Rafiki yetu katika afya ana vipengele vingi kama vile: kikagua dalili pamoja na taarifa za kibinafsi za afya, uwezo wa kufuatilia dalili, na ufikiaji wa hifadhidata yetu ya kitiba (“Maktaba ya Magonjwa”) inayowezeshwa na mfumo wa kipekee wa akili bandia wa Ada.

1.2. Rafiki katika afya anapatikana kama app kwa kupakuliwa bure kupitia simujanja yako (inajulikana hapa kama “App ya Ada”), na (kwa wakati na mahali inapopatikana) kupitia programu iliyo katika tovuti yetu (ambayo hapa inajulikana kama “Tovuti”). Ada pia imekuza kifaa cha ukaguzi (hapa kinajulikana kama “Kifaa cha Ukaguzi”) na huduma husika. Tovuti, App ya Ada,  na Kifaa cha Ukaguzi, pamoja na programu yoyote, huduma au teknolojia nyingine ambazo Tovuti, App ya Ada, na Kifaa cha Ukaguzi vinatokana, vinajulikana hapa kama “Jukwaa la Ada.” 

TAFADHALI TAMBUA KWAMBA JUKWAA LA ADA HALITOI UTAMBUZI WOWOTE WA UGONJWA. UNAPOHOFIA AFYA YAKO, TAFADHALI TAFUTA USHAURI WA MTAALAMU WA AFYA. KATIKA HALI YA DHARURA, UNAPASWA KUWASILIANA NA WATOA HUDUMA ZA DHARURA HARAKA IWEZEKANAVYO. SIKUZOTE SHAURIANA NA DAKTARI WAKO AU MHUDUMU MWINGINE WA AFYA ALIYEFUZU IWAPO UTAKUWA NA MASWALI YOYOTE KUHUSU MASUALA YOYOTE YA KITIBA. HAUPASWI KUPUUZA USHAURI WA KITAALAMU KUTOKA KWA DAKTARI AU KUTOHUDHURIA MIADI NA DAKTARI KWA KUTEGEMEA MAELEZO ULIYOSOMA AU KUSIKIA KWENYE JUKWAA LA ADA.

1.3. Jukwaa la Ada linaendeshwa na Ada Health GmbH, kampuni iliyoanzishwa nchini Ujerumani na kusajiliwa na Mahakama ya Munich, chini ya nambari ya usajili wa kibiashara nambari 189710, na ofisi yake iliyosajiliwa ikiwa Neue Grünstraße 17, 10179 Berlin, Ujerumani.

1.4. Kama ungependa kuwasiliana nasi, tafadhali tuma barua pepe kwa [email protected].

1.5. Unalizimika kuwa na umri wa angalau miaka 16 ikiwa ungependa kutumia Jukwaa la Ada. Ikiwa una umri wa chini ya miaka 18, matumizi ya Jukwaa la Ada, na kukubaliana kwako na Vigezo na Masharti haya, kutalazimika kuwa kumeidhinishwa na mlezi wako mwenye mamlaka ya kisheria juu yako.

1.6. Ili uweze kutumia Jukwaa la Ada kikamilifu, unalazimika kukubaliana na Vigezo na Masharti haya. Iwapo hutakubali hivi Vigezo na Masharti, huenda ukashindwa kutumia au kufikia sehemu yoyote ya Jukwaa la Ada.

1.7. Lugha zinazotumika katika mkataba ni Kijerumani na Kiingereza.

2. Uhusiano wa kisheria kati yako na Ada

2.1. Vigezo na Masharti haya yanahusu utumiaji wa Jukwaa la Ada na yana masharti yanayodhibiti utumiaji wako wa Jukwaa la Ada. Ni muhimu uwe umesoma na kuelewa Vigezo na Masharti yaliyopo kwa sasa pamoja na Sera yetu ya Faragha kabla ya kutumia Jukwaa la Ada. Iwapo unapata shida kuelewa sehemu yoyote ya hati hizi, tafadhali wasiliana nasi kupitia [email protected] na tutakupa maelezo zaidi.

2.2. Unaweza tu kufungua Akaunti ya Mtumiaji katika Jukwaa la Ada iwapo tu unakubaliana na Vigezo na Masharti haya. Iwapo hautakubaliana na Vigezo na Masharti haya, unaweza kushindwa kufungua Akaunti ya Mtumiaji kwenye Jukwaa la Ada.

3. Maelezo tunayokusanya kukuhusu

3.1. Kulinda faragha yako na data yoyote inayohusiana na wewe (ambayo inajulikana hapa kama “Data Binafsi”) ni muhimu sana kwetu. Kwa sababu hiyo, Data yoyote binafsi inayotokana na matumizi ya Jukwaa la Ada itakusanywa tu, kuhifadhiwa na kuchakatwa nasi kwa kufuata Kanuni ya Ulinzi wa Data ya 2016/679 ya Aprili 27, 2016 (“GDPR”). Tafadhali soma Sera zetu za Faragha ili uelewe jinsi, na ni kwa sababu gani tunakusanya na kutumia maelezo yako ili kukupa huduma nzuri zaidi iwezekanavyo.

3.2. Hapa unatupatia haki ya kudumu, ya duniani kote, inayoweza kuhamishwa, na inayoweza kugawanywa, kutumia data, ambayo utambulisho wake umefichwa kwa mujibu wa sheria inayotumika ya ulinzi wa data, kwa njia yoyote, iwe inayojulikana au haijulikani sasa. Unatambua na unakubali kuwa tunamiliki haki zote, mada na maslahi kwa data yoyote tunayoitoa sisi kutoka kwa data kama hiyo ambayo utambulisho wake umefichwa. 

4. Jukwaa la Ada

4.1. Jukwaa la Ada linakupa fursa ya kutambua kinachoweza kusababisha hali yako ya sasa ya afya. Jukwaa la Ada linatumia msingi wa maarifa ya kitiba kupendekeza uwezekano wa visababishi vya dalili zako  (inajulikana hapa kama “Ripoti ya Tathmini”).

4.2. Jukwaa la Ada linatolewa kwako bila malipo, na unaruhusiwa kufanya idadi isiyo na kikomo ya tathmini ya dalili na Ripoti za Tathmini.

4.3. Tafadhali fahamu kuwa tunatoa Jukwaa la Ada kwa madhumuni ya taarifa tu. Sio ushauri wa kimatibabu. Jukwaa la Ada sio njia mbadala mwafaka ya kupata ushauri wa matibabu unaopatikana kutoka kwa daktari wako, mtaalamu wa jumla au mtoaji mwingine wa huduma ya afya.

4.4. Jukwaa la Ada HALITOI utambuzi wa magonjwa, wala halitoi maagizo ya namna ya kutibu maswala yoyote ya kiafya unayoweza kuwa nayo. Hii inaweza kufanywa tu kwa kushauriana na mtaalamu wa tiba (kama vile mtaalamu wa jumla au “general practitioner”).

4.5. Mwisho, ikiwa una matatizo yoyote ya kiafya kutokana na maelezo uliyotoa kwenye Jukwaa la Ada, ni jukumu lako kuamua kushauriana na mtaalamu wa tiba na/au kutafuta ushauri wa kitiba.

5. Kufungua Akaunti ya Mtumiaji

5.1. Kabla ya kutumia App ya Ada, utahitajika kuwa na kitambulisho cha Apple au akaunti ya Google. Kisha unaweza kupakua App ya Ada kutoka Duka la App la Apple au Duka la Google Play (ambayo inajulikana hapa, kipekee au kwa ujumla, kama “Duka la App”) kwa kifaa chako cha mkononi au kompyuta kibao. Pia unaweza kulifikia Jukwaa la Ada moja kwa moja kupitia programu iliyo kwenye tovuti au kupitia program, kupitia kwetu moja kwa moja au kupitia mmoja wa washirika wetu.

5.2. Baada ya kupakua App ya Ada (au kutumia kupitia programu inayopatikana kwenye tovuti yetu) unaweza kujisajili kwenye Jukwaa la Ada kwa kufungua Akaunti ya Mtumiaji ikiwa na jina la mtumiaji na nenosiri (ambayo inajulikana hapa kama “Akaunti ya Mtumiaji”). Usajili unajumuisha ombi la Mtumiaji kutii Vigezo na Masharti haya. Tunaweza (lakini hatulazimiki) kukubali ombi hili kwa kuwezesha matumizi ya Jukwaa la Ada kwa mara ya kwanza kupitia Akaunti ya Mtumiaji. Tutakutumia uthibitisho wa usajili kwa njia ya kielektroniki.

Kwa kutumia, kupata, au vinginevyo kutumia Jukwaa la Ada HATA KAMA HAUFUNGUI AKAUNTI YA MTUMIAJI, unakubali, tambua na kujipatia mwenyewe hivi Vigezo na Masharti.

5.3. Tutahifadhi maandishi ya mkataba wa Vigezo na Masharti yaliyokubaliwa. Zaidi ya hili, hatutakuwa na jukumu lolote kuhusiana na upatikanaji wa masharti yaliyokubaliwa na Mtumiaji. 

5.4. Tunawashauri Watumiaji wetu kutumia tu nywila ‘madhubuti’ kwa Akaunti zao za Mtumiaji (nywila madhubuti ni nywila ambazo zinajumuisha mchanganyiko wa nambari, herufi kubwa na ndogo, na alama). Wakati unaposajili Akaunti yako ya Mtumiaji au kuwasilisha maelezo mengine kwetu, unatamka kuwa maelezo yaliyotolewa kwetu ni sahihi na kamili. Endapo kutatokea mabadiliko yeyote katika maelezo hapo baadaye, unatamka kwamba utatuarifu mara moja kuhusu mabadiliko kama hayo kwa kusasisha maelezo.

5.5. Huenda ikawezekana kuingia kwenye Jukwaa la Ada kupitia akaunti unayomiliki kupitia mtoa huduma mwingine (kama vile Facebook). Ikiwa unaingia kwenye Jukwaa la Ada kupitia watoa huduma wengine kama hao, unatupatia pia ruksa ya kutumia maelezo fulani ambayo umetoa kwa mtoaji huyo mwingine wa huduma (mfano jina, tarehe ya kuzaliwa, anwani ya barua pepe, nambari ya simu), kama na kwa kadiri inavyoruhusiwa na vigezo na masharti ya mtoaji wa huduma na Sera yetu ya Faragha.

5.6. Una jukumu la kudumisha usiri wa maelezo yako ya kuingia na jambo lolote katika Akaunti yako ya Mtumiaji. Ikiwa utakuwa na mashaka kwamba akaunti yako ya Mtumiaji inaweza kuwa imetumika vibaya, unakubali kutufahamisha mara moja kuhusu mashaka haya kwa kutuma barua pepe kwa [email protected].

6. Haki yako ya kutumia Jukwaa la Ada

6.1. Jukwaa la Ada na nyenzo zote na yaliyomo ndani yake ni mali yetu au mali ya watu ambao wametupa leseni inayotumika (hii inahusiana pia na maunzi laini ya watoa huduma wengine yaliyoorodheshwa kwenye App ya Ada). Tunakupa haki ya kutumia nyenzo na maudhui haya, lakini kwa madhumuni tu ya kutumia Jukwaa la Ada kwa ajili yako binafsi au kwa niaba ya mtu mwingine sikuzote kwa mujibu wa Vigezo na Masharti haya. Ikiwa unatumia Jukwaa la Ada kwa niaba ya mtu mwingine, bado unawajibika kikamilifu kuhakikisha kuwa matumizi kwa niaba ya mtu huyo yanaruhusiwa kwa mujibu wa faragha na mahitaji mengine halali ya kisheria. Hasa, unalazimika kupata idhini inayofaa kutoka kwa mtu huyo na kumjulisha kuhusu Vigezo na Masharti yetu na Sera ya Faragha.

6.2. Tunakupa haki wewe binafsi ya kufikia na kutumia Jukwaa la  Ada. Ni marufuku kuhamisha haki hii kwa mtu mwingine yeyote, au kuuza, kutoa au kuhamisha Akaunti yako ya Mtumiaji kwa mtu mwingine yeyote. Haki yako ya kufikia na kutumia Jukwaa la Ada haituzuii kuwapa watu wengine haki ya kufikia na kutumia Jukwaa la Ada.

6.3. Haki yako ya kutumia jina “Ada” au alama yoyote ya biashara, nembo, majina ya miliki au sifa nyingine bainifu za alama yoyote ya biashara ina mipaka kwenye wigo ulioelezwa katika Vigezo na Masharti haya.

6.4. Kutokana na uthibitisho wako wa kutii Vigezo na Masharti haya, tunakupa haki yenye mipaka, isiyohamishika, isiyo milikishwa kwa kwa mtu mwingine, ya kibinafsi, isiyo ya kipekee, inayoweza kukatizwa ya kupakua App ya Ada kwenye kifaa chako au kufikia Tovuti au Kifaa cha Ukaguzi chini ya masharti yaliyowekwa katika Vigezo na Masharti au sera ya faragha, au chini ya masharti yoyote yanayohusiana na Duka la App ambalo unaweza ukawa umepakulia App ya Ada.

6.5. Kama Mtumiaji, isipokuwa tabia kama hizo zinaruhusiwa ipasavyo kulingana na Vigezo na Masharti haya, au isipokuwa zimeruhusiwa chini ya sheria ya lazima ya hakimiliki pale inapolazimika kwa matumizi ya Jukwaa la Ada kulingana na madhumuni yake yaliyokusudiwa, na/au ni muhimu kupata maelezo yanayofaa kufikia upatanisho na programu nyingine, unakubali kujiepusha na yafuatayo: 

  1. Wewe, Mtumiaji, unakubali kutorudufu au kunakili Jukwaa la  Ada, aidha lote au sehemu yake.
  2. Wewe, Mtumiaji, unakubali kutouza au vinginevyo kufanya Jukwaa la Ada lipatikane, aidha kikamilifu au sehemu yake, kwa mtu mwingine yeyote.
  3. Wewe, Mtumiaji, unakubali kutobadilisha Jukwaa la Ada, kikamilifu au sehemu yake,  katika namna yoyote ile.
  4. Wewe, Mtumiaji, unathibitisha kwamba hautajaribu kugundua au kufikia chanzo cha msimbo wa Jukwaa la Ada, kikamilifu au kwa sehemu, isipokuwa ikiwa imechapishwa nasi waziwazi na kutolewa hadharani.

6.6. Unajua kuwa sisi, na/au watu ambao wametupa leseni katika swala hili, tunayo haki ya maelezo yoyote ya siri, haki za utumiaji, na urejeshi- na haki zingine zozote  za  uvumbuzi zilizopo kwa ukamilifu au sehemu ya haki hizo - kuhusu Jukwaa la Ada.

6.7. Maoni / uchunguzi. Ikiwa utatoa maoni, mawazo au mapendekezo, au ikiwa unajibu  maswali yatokanayo na uchunguzi wenye uhusiano na Huduma zetu (hapa itajulikana kama “Maoni”), unakubali kwamba Maoni sio siri na kwamba unatupa leseni (ruksa) ya duniani kote, isiyo ya kipekee, isiyo badilishika, ya kudumu, ya bure na isiyo na kikomo ya kutumia Maoni yako kwa njia yoyote, kwa sababu yoyote, na kupitia chombo chochote au teknolojia inayofahamika sasa hivi au haifahamiki, iwe kwa ukamilifu au sehemu yake, na ikiwa imebadilishwa au haijabadilishwa. Tutatumia Maoni yako sikuzote kwa kufuata Vigezo na Masharti hayo, Sera yetu ya faragha na sheria zingine zozote zinazohusika.

7. Utumiaji wako wa Jukwaa la Ada

7.1. Pamoja na vifungu vingine katika Vigezo na Masharti haya, sehemu hii inafafanua kanuni fulani zinazohusiana na matumizi ya Jukwaa la Ada (ambazo zinajulikana hapa kama “Kanuni”).

7.2. Ifuatayo ni orodha ya mambo ambayo ni marufuku katika muktadha wa kutumia Jukwaa la Ada. Ni marufuku:

  1. Kuzuia, ondolea uwezo, au vinginevyo miliki kwa hila vipengele vyovyote vya usalama vya Jukwaa la Ada au vipengele vyovyote muhimu zinavyozuia kutumia au kunakili maudhui yanayopatikana kupitia Jukwaa la Ada,
  2. Kufungua Akaunti nyingi za Mtumiaji katika Jukwaa la Ada (hata hivyo, kwa kadiri utendaji wa Jukwaa la Ada unavyoruhusu, unaweza kuunganisha mitandao yako ya kijamii au akaunti zingine tunazoziunga mkono na Akaunti ya Mtumiaji kwenye Jukwaa la Ada),
  3. Kutoa maelezo ya uongo au potofu katika maelezo ya Akaunti ya Mtumiaji,
  4. Kuruhusu mtu mwingine yeyote kutumia Jukwaa la Ada kwa niaba yako au mahali pako,
  5. Kutumia Jukwaa la Ada ikiwa tumesimamisha kwa muda haki yako ya utumiaji, au kukukataza kuendelea kulitumia,
  6. Kutuma barua pepe taka, jumbe za kukera au zinazojirudia,
  7. Kutenda kwa njia yoyote isiyo ya kisheria au isiyo halali,
  8. Kubadilisha, kukatiza, kushambulia au kuvuruga Jukwaa la Ada, au kukatiza ujumbe,
  9. Kutumia vibaya Jukwaa la Ada au kulipenyezea virusi, vitegeshi, kirusi mnyoo,”logic bombs” au kitu chochote kingine ambacho kinaweza kuumiza Jukwaa la Ada au mtumiaji mwingine yeyote wa kifaa cha Jukwaa la Ada,
  10. Kudondoa maelezo kutoka kwenye Jukwaa la Ada kinyume na inavyoruhusiwa chini ya Vigezo na Masharti haya,
  11. Kutuma au kuchangia mambo yoyote yenye kutusi, ya vitisho, yenye machukizo, ya kupotosha, yasiyo ya kweli, ya kukera au maudhui ya kutusi, au maudhui ambayo yana muundo wowote wa uchi au vurugu, na
  12. Kuweka maelezo au maoni kuhusu mtu mwingine yeyote bila idhini ya mtu huyo husika.

7.3. Kutotii Sheria zilizoorodheshwa katika aya ya 7.2 kunawakilisha uvunjaji muhimu wa Vigezo na Masharti haya, na inaweza kusababisha sisi, kwa hiari yetu, kuanzisha hatua zifuatazo - aidha rejareja au kwa pamoja:

  1. Kusimamisha mara moja kwa muda, au kuondoa kabisa haki ya kutumia Jukwaa la Ada,
  2. Kukutumia onyo,
  3. Uanzishaji wa mashitaka ya kisheria dhidi yako, pamoja na dai la kutakiwa kurudisha gharama zozote na matumizi yaliyofanyika kutokana na uvunjaji wa makubaliano (pamoja na kiasi cha gharama za uendeshaji na malipo ya wanasheria), na zaidi ya hayo
  4. Kufichua maelezo kwa mamlaka za utekelezaji wa sheria, ikiwa na kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria na tunavyoona sisi ni lazima.

7.4. Mwitikio wa uvunjaji wa makubaliano uliofanywa na wewe hauishii tu kwenye hatua zilizoelezewa katika aya iliyotangulia ya 7.3, yaani tunayo haki ya kuchukua hatua yoyote zaidi kulingana na Vigezo na Masharti haya na / au sheria ya mashtaka ya uhalifu.

8. Kuhitimisha uhusiano wetu wa kimkataba

8.1. Ikitokea kwamba unahisi kuwa huwezi kukubaliana tena na Vigezo na Masharti ya sasa au Sera ya faragha, wakati wowote, unakubali kuacha kutumia Jukwaa la Ada mara moja.

8.2. Una haki ya kuacha kutumia Jukwaa la Ada wakati wowote na kuhitimisha makubaliano yako na Ada, pia ikiwa haukubaliani na mabadiliko kwenye Jukwaa la Ada au Vigezo na Masharti haya tuliyopendekeza. Tafadhali fuata maelekezo kwenye Jukwaa la Ada ili kufunga Akaunti yako ya Mtumiaji. Ikiwa unalifikia Jukwaa la Ada kupitia App ya Ada, unaweza kufuta Akaunti yako ya Mtumiaji kupitia menyu ya mipangilio (settings).

8.3. Ikiwa tutachagua kuhitimisha makubaliano yako nasi, tutakupa notisi ya majuma mawili. 

8.4. Haki ya kila upande kuhitimisha makubaliano kwa sababu fulani inabaki bila kuathiriwa. Sababu ambayo inatufanya kuhitimisha makubaliano inaweza kuwa, haswa lakini si pekee, ukiukaji wako wa vifungu muhimu vya  kimkataba (haswa kifungu 7.2) na ikiwa, kwa sababu ya hali za nje, inaweza kudhaniwa kuwa unatumia vibaya huduma zetu. Ikiwa kuna sababu nzuri, tuna ruhusa zaidi ya kuzuia ufikiaji wako wa Jukwaa la Ada, bila taarifa yoyote, na ikizingatiwa kwamba hakuna hatua nyingine ndogo za kuchukua zinazofaa.

8.5. Ikiwa wewe au sisi tunafunga Akaunti yako ya Mtumiaji kama ilivyoelezewa katika aya hii au kuondoa haki yako ya kutumia Jukwaa la Ada, tutafuta data yoyote binafsi kuhusu wewe iliyohifadhiwa kulingana na Sera yetu ya Faragha (na kama ilivyoainishwa katika vifungu vya kisheria vinavyotumika), ikizingatiwa kwamba haki zetu za kutumia data ya aina hiyo kwa utaratibu wa kuficha utambulisho zinabaki bila kuathiriwa kwa mujibu wa sehemu ya 3.2. Pia unapoteza haki uliyopewa hapo awali ya kutumia Jukwaa la Ada.

9. Ahadi yetu kwako

9.1. Maelezo yoyote kuhusu dalili ulizoeleza ambayo yanaletwa kwako kwa njia ya maandishi kupitia Jukwaa la Ada - kama taarifa iliyotolewa, au fahamika, kama ilivyoanishwa kwenye Kanuni ya § 126b ya Jinai ya Kijerumani- ni kwa madhumuni ya taarifa tu. Taarifa inatolewa na Ada kama ilivyo, bila hati, dhamana, au uwakilishi wa aina yoyote.

9.2. Haupaswi kuchukua hatua yoyote kutokana na maelezo yaliyotolewa katika Jukwaa la Ada bila kushauriana kwanza na daktari au mtaalamu mwingine wa tiba.

9.3. Kutokana na asili ya intaneti na teknolojia husika, hatuwezi kuahidi kwamba utaweza kutumia Jukwaa la Ada wakati wote bila usumbufu wowote, na bila cheleo au dosari, na kwamba Jukwaa la Ada wakati wote litakidhi matarajio yako. Kwa hivyo hatuwezi kuwajibika kuhusiana na utendaji au upatikanaji wa Jukwaa la Ada katika Vigezo na Masharti haya ya sasa. Tunaondoa wazi dhima yoyote kali ambayo itaweza kutumika kupitia utekelezaji wa sheria kutokana na kasoro za Jukwaa la Ada zilizokuwepo wakati makubaliano ya utumiaji wa Jukwaa la Ada kati yetu na wewe yalikamilishwa. 

9.4. Ikiwa utapata madhara yoyote kupitia matumizi ya Jukwaa la Ada, tunaweza tu kuwajibika kisheria kwa dhamira na uzembe mkubwa. Tunaweza kuwajibika zaidi kisheria kwa ukiukaji wa kizembe wa majukumu muhimu ya kimkataba, ambayo lazima yatimizwe kwa utaratibu ili kwa hata makubaliano haya yaweze kutekelezeka vizuri, na ukiukaji wake utahatarisha dhumuni la makubaliano ambalo wewe, Mtumiaji, unapaswa katika hali za kawaida kuamini litatimizwa. Katika kesi ya dhamira na uzembe mkubwa, tunaweza hata hivyo kuwajibika tu kisheria kwa madhara yanayohesabika. Hatuwezi kuwajibika kisheria tu kwa ukiukaji wa kizembe wa majukumu yoyote zaidi ya yale yaliyoainishwa katika sentensi zilizotangulia. Kujitoa kwa uwajibikaji wa kisheria kulikotangulia hakuhusiki kwenye ukiukwaji unaosababisha kifo au jeraha la kimwili na dhima yoyote chini ya Sheria ya Kijerumani ya Dhima ya Bidhaa.

10. Huduma za watoa huduma Wengine

10.1. Ikiwa, na kwa kadiri, Jukwaa letu la Ada lina viungo vya tovuti zingine au nyenzo zinazoendeshwa na watoa huduma wengine, viungo hivi vinapaswa kuchukuliwa kuwa vinatolewa kwako kwa ajili ya taarifa tu.

10.2. Hatuna uwezo wa kushawishi maudhui ya tovuti za aina hiyo au nyenzo zinazotolewa na watoa huduma wengine, na hatuwezi kuwajibika  kisheria kwa maudhui ya taarifa au tovuti zilizounganishwa kwetu. Hatutoweza kuwajibika kisheria kwa madhara yoyote ya kifedha au kimwili ambayo yanaweza kutokea kutokana na, au kuhusishwa na, matumizi ya tovuti au nyenzo za aina hiyo.

10.3. Unaelewa kuwa upatikanaji wa App ya Ada unategemea watoa huduma wengine ambapo ulipakua App ya Ada (Duka la App). Unatambua kuwa Vigezo na Masharti haya yanahusu mahusiano ya kimkataba kati yako na Ada, na sio mahusiano ya kimkataba kati yako na Duka la App.

11. Masasisho ya Jukwaa la Ada

11.1. Tunasasisha na kuboresha Jukwaa la Ada mara kwa mara. Tunajitahidi kila wakati kukupatia huduma na vipengele vipya vya kibunifu. Pia tunafanya maboresho na masasisho ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia, tabia na jinsi ambavyo watu hutumia intaneti.

11.2. Tunahifadhi haki ya kubadilisha muundo maalum wa huduma fulani kwa kusasisha Jukwaa la Ada, kuweka upya kipengele hicho na kusitisha huduma au uwezeshaji wa kipengele hicho. Mabadiliko haya yanaweza kuathiri utendaji wako kwenye Jukwaa la Ada. Mabadiliko yanaweza kujumuisha kuondoa, kurekebisha au kuweka upya vipengele unavyotumia. Tutakuarifu kuhusu mabadiliko na haki zako iwapo kuna mabadiliko kupitia taarifa inayojitegemea, kwa kiwango ambacho umejiandikisha kupata taarifa kama hizo (angalia aya ya 12.3.).

11.3. Masasisho yanaweza kutolewa nasi kwa nyakati au kupitia Duka la App ambalo ulipakulia App ya Ada. Mara kwa mara, ili kuweza kutumia Jukwaa la Ada, unaweza kulazimika kusasisha maunzi laini (software) ya watoa huduma wengine. 

12. Mabadiliko kwenye Vigezo na Masharti haya

12.1. Tuna haki ya kurekebisha, kubadilisha au kuongeza Vigezo na Masharti ya sasa mara kwa mara. Toleo la sasa la Vigezo na Masharti linaweza kupatikana kwenye Tovuti yetu (www.ada.com).

12.2. Mabadiliko yoyote katika Vigezo na Masharti haya yatakuwa kwa kawaida ni matokeo ya kuongezwa kwa vipengele vipya kwenye Jukwaa la Ada, au matokeo ya mabadiliko ya sheria au kanuni husika.

12.3. Tutawasiliana nawe kukujulisha mabadiliko yoyote au nyongeza katika Vigezo na Masharti haya na hati zilizorejelewa katika Vigezo na Masharti haya angalau siku 30 kabla ya mabadiliko yoyote au nyongeza kwenye Vigezo na Masharti haya kuanza kutumika. Ikiwa hautokuwa na pingamizi ndani ya siku 30 za kupokea taarifa, mabadiliko na nyongeza hizo zitazingatiwa kuwa zinatumika na kukubaliwa kuanzia tarehe ya mwisho na kuendelea. Tutakujulisha kuhusu haki yako ya pingamizi na matokeo ya pingamizi hilo kupitia taarifa yetu ya mabadiliko katika Vigezo na Masharti. Ikiwa, utapinga marekebisho ndani ya muda uliokubalika, haina mantiki kwetu kisheria, kiuchumini, au kiufundi kuendelea na utoaji wa Jukwaa la Ada, tunayo haki ya kuvunja makubaliano ndani ya muda usiozidi tarehe ambayo marekebisho yamepangwa kuanza kutumika kama ilivyoelezwa kwenye taarifa. Haki nyingine yoyote ya kuvunja makubaliano inabaki bila kuathirika.

13. Hati zinazosimamia uhusiano wa kimkataba kati yako na sisi

Toleo la sasa la Vigezo na Masharti linajumuisha vifungu vyote vinavyoongoza uhusiano wa makubaliano ya kimkataba kati yako na sisi. Matoleo ya zamani ya Vigezo na Masharti hayatumiki tena kwenye uhusiano wetu wa kimkataba na mahali pake pamechukuliwa kabisa na toleo la sasa.

14. Sheria na mamlaka yanayotumika

14.1. Makao yetu makuu yapo Ujerumani. Makubaliano yaliyofikiwa kwa mujibu wa vigezo na Masharti haya yapo chini ya sheria za Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani. Bila kuleta athari kwenye chaguo la mamlaka hapo juu, wakati wa makubaliano kati ya wafanyabiashara na watumiaji, vifungu vya sheria ya nchi ambamo mtumiaji anaishi na ambayo - chini ya sheria ya nchi hiyo - haiwezi kudharauliwa, inaweza kutumika kwa faida ya watumiaji ikiwa mfanyabiashara:

  1. anaendeleza shughuli zake za kibiashara au za kitaalam katika nchi ambako mtumiaji anaishi, au
  2. shughuli kama hizo zinaelekezwa kwa njia yoyote katika nchi hiyo au katika nchi kadhaa ikijumuisha nchi hiyo,

na makubaliano yapo katika wigo wa shughuli kama hizo.

14.2. Mahakama za Ujerumani zina mamlaka ya kipekee ya kusuluhisha mizozo yoyote inayoibuka sambamba na, au kusababishwa na matumizi yako ya Jukwaa la Ada.

14.3. Tume ya Ulaya inatoa jukwaa mtandaoni la kusuluhisha migogoro ambalo linapatikana kupitia http://ec.europa.eu/consumers/odr. Ada haishiriki katika kesi za utatuzi wa migogoro mbele ya bodi ya usuluhishi wa malalamiko ya watumiaji.

15. Mengineyo

15.1. Unaturuhusu kuwasiliana na wewe kwa njia ya kielektroniki (kama vile barua pepe au aina nyingine ya maandishi kama ilivyoainishwa katika § 126b ya Sheria ya Madai ya Kijerumani).

15.2. Tunaweza kukutumia taarifa kielektroniki kwa anwani ya barua pepe uliyotoa wakati wa kujiandikisha kwenye Jukwaa la Ada, au kupitia njia zingine za kielektroniki kwenye Jukwaa la Ada zinapopatikana.

15.3. Kushindwa kutekeleza haki zetu ni lazima isieleweke kama kutupilia mbali haki hizo.

15.4. Endapo kifungu chochote katika Vigezo na Masharti haya kitakuwa batili au kubatilishwa au kushindwa kutekelezeka, ufanisi wa vifungu vilivyobaki hautaathirika.

15.5. Mhusika wa mkataba tu ndio mwenye haki ya kuhakikisha vifungu vya kimkataba vinatekelezwa.

16. Mawasiliano

Ikiwa ungependa kuwasiliana nasi kuhusiana na Vigezo na Masharti ya sasa au hati nyingine yoyote iliyotajwa ndani yake, tafadhali tutumie barua pepe kupitia [email protected].