Kuhusu sisi

Ada ni kampuni ya afya ya kimataifa iliyoanzishwa na madaktari, wanasayansi, na mapainia wa sekta ya teknolojia ili kuleta uwezekano mpya katika afya binafsi. Msingi wa mfumo wa Ada unaunganisha maarifa ya kitiba na teknolojia erevu ili kusaidia watu wote kusimamia afya zao. Pia kusaidia wataalamu wa afya kutoa huduma kwa ufanisi. Ada inajivunia kushirikiana na mifumo ya juu ya afya na mashirika ya kimataifa yasiyotafuta faida (global non-profit organizations) kutimiza maono ya kuboresha ufanisi katika huduma za afya. Tathmini milioni 20 zimekamilishwa tokea Ada izinduliwe mwaka 2016 kwa matumizi ya ulimwengu mzima.

Ada katika namba

Ada Health

 • Miaka 9 ya utafiti na usitawishaji

 • Ofisi 5 Berlin (Mitte), Berlin (Kreuzberg), Munich, London, New York

 • € Milioni 60 ufadhili

 • 200 wafanyakazi

 • 50 wastadi wa ndani wa tiba

Ada

 • Milioni 10 watumiaji

 • Milioni 20 tathmini zimekamilishwa

 • 250,000 makadirio ya nyota-5

 • 7 Lugha

 • App namba 1 katika app za kitiba Tanzania

Tuzo

App Promotion Summit's Fastest Growing App

Vyeti vya Uthibitisho & Utekelezaji

 • Inakidhi mahitaji ya EU-GDPR

  Sheria za jumla za Uthibiti wa Data katika Umoja wa Ulaya

 • Nembo ya CE

  Bidhaa zetu zote zimesajiliwa kama kifaa cha matibabu daraja la kwanza katika Eneo la Kibiashara la Ulaya (European Economic Area) (EEA). Nembo ya CE inathibitisha ubora wa bidhaa ndani ya soko la Ulaya.

 • ISO 27001

  Imethibitishwa kwa kiwango cha ubora wa usalama wa taarifa (data)

 • ISO 13485

  Mfumo wa usimamizi wa ubora uliothibitishwa