1. Ada
  2. Help

Je, app ya Ada inaweza kuwa mbadala wa huduma ya daktari?

Hapana. App ya Ada haijakusudiwa kuwa mbadala wa huduma ya daktari na haiwezi kufanya utambuzi wa ugonjwa (diagnosis). Madaktari wameunda app ya Ada ili kusaidia madaktari wengine kufanya kazi zao kwa ufanisi na daima tutaendelea kushirikiana na madaktari kwa ajili ya mustakabali bora wa afya kwa wote.

Timu yetu ya wataalamu wa Maarifa ya Kitiba ina madaktari zaidi ya 60 wenye taaluma mbalimbali kutoka zaidi ya nchi 20 tofauti. Utofauti huu unazipa teknolojia zetu uwezo wa kuhudumia watu wa aina tofauti. Ili kuhakikisha usahihi, usalama, na ujumuishaji wa hali ya juu, Timu yetu ya Maarifa ya Kitiba huunda na kukagua mara kwa mara maudhui kulingana na tafiti mpya zilizothibitishwa na wataalamu wengine, data za uambukizaji na udhibiti wa magonjwa, na miongozo ya usimamizi yenye viwango vya ubora unaokubalika katika masuala ya kitiba.

Have more questions? Submit a request