Usalama

Kuhakikisha viwango vya juu zaidi vya faragha na usalama kwa watumiaji wetu ni muhimu sana katika namna tunavyokuza teknolojia yetu, bidhaa, na kusimamia biashara yetu. Ni kanuni ambayo inabeba msingi wa kuanzishwa kwa Ada. 

Watumiaji wa bidhaa yetu wanaweza kuwa na hakika kwamba taarifa za afya binafsi wanazoipa app ya Ada ni siri, zimesimbwa kwa usalama (securely encrypted), na hazigaiwi bila idhini yao.

Hivi ndivyo tunavyosimamia usalama

Tunaendelea kufanya kazi kwa uwazi pamoja na washirika muhimu, watunga sheria, na tasnia ya teknolojia kusaidia kuongeza uwazi na uelewa kuhusiana na namna tunavyodumisha usalama wetu ndani ya Ada, ikiwa ni pamoja na:

Taarifa
Tunafuata ‘usalama kwa njia ya muundo,’ hii ina maanisha Ada inatekeleza usalama kuanzia mwanzoni mwa uhai wa bidhaa, na sio baada na wala sio kama kitu cha ziada. Kwa maneno mengine, usalama na bidhaa za Ada vinakwenda sambamba.

Hifadhi
Tunatenganisha wasifu wa mtu na taarifa zake za kiafya na kuhifadhi tofauti kila moja ya taarifa hizo kwenye mifumo ya kuhifadhi (servers) taarifa za intaneti Ulaya.

Waajiriwa
Afisa wetu wa Usalama wa Taarifa, anahakikisha kila mfanyakazi wa Ada anatimiza majukumu yake binafsi ya kiusalama.

Ofisi
Tunasimamia usalama wa ofisi zetu ili kulinda taarifa, kuanzia kwenye kompyuta mpakato zenye viwambo vinavyojizima vyenyewe (automatic screenlocks) mpaka kwenye milango ya chuma.

Majaribio
Mara kwa mara huwa tunajaribu miundombinu yetu ya usalama ili kubaini sehemu dhaifu na kuzirekebisha.

Ukaguzi
Ada inakaguliwa mara kwa mara na mamlaka za nje na za ndani ya kampuni ili kuhakikisha tunakidhi matakwa ya kisheria, na pia kuwa na bidhaa zenye viwango vinavyokubalika.

Ada inatimiza matakwa ya kisheria yafuatayo:

  • Inakidhi mahitaji ya EU-GDPR

    Inakidhi mahitaji ya EU-GDPR
    Sheria za jumla za Uthibiti wa Data katika Umoja wa Ulaya

  • Nembo ya CE

    Nembo ya CE
    Bidhaa zetu za kifaa cha kitiba zina nembo ya CE

  • ISO 27001

    ISO 27001
    Imethibitishwa kwa kiwango cha ubora wa usalama wa taarifa (data)

  • ISO 13485

    ISO 13485
    Mfumo wa usimamizi wa ubora uliothibitishwa

Kutana na baadhi ya watu kwenye timu

Luke Doherty
Luke Doherty
Head of Information Security
Michael Tsesis
Michael Tsesis
Data Protection Officer
Andrea Akinsete
Andrea Akinsete
Senior Information Security Analyst
Fatih Tahmilci
Fatih Tahmilci
Senior Information Security Analyst
Tarik Kobalas
Tarik Kobalas
Lead Security Engineer
Honey Kurian
Honey Kurian
Software Security Engineer

Bado unataka kujua zaidi kuhusu suala la usalama ndani ya Ada?

Soma Privacy Policy, Terms & Conditions, FAQs yetu, au wasiliana na sisi kupitia [email protected].