1. Ada
  2. Magonjwa
  3. Rheumatoidi arthritisi

Rheumatoidi arthritisi

Imeandikwa na Timu ya Ada ya Maarifa ya Kitiba

Imesasishwa tarehe

Ugonjwa wa arthritisi ya rheumatoidi ni nini?

Arthritisi ya rheumatoidi (Rheumatoid arthritis) ni ugonjwa wa inflamesheni (sehemu ya mwili kuvimba, kuwa nyekundu, yenye joto na maumivu) kwenye viungo. Huu ni ugonjwa wa kinga nafsia (autoimmune), ambayo humaanisha ni matokeo ya mfumo wa kinga kushambulia tishu zenye afya kimakosa.

Wanawake huathirika zaidi kuliko wanaume, na mara nyingi utambuzi hufanywa kati ya umri wa miaka 35 hadi 50. Dalili za ugonjwa huu ni viungo kuvimba na kuuma. Viungo vidogo kwneye mikono na miguu huathirika zaidi.

Utambuzi hufanywa kulingana na dalili, uchunguzi wa mwili na vipimo vya damu.Hamna tiba ya ugonjwa huu. Matibabu hujumuisha dawa za maumivu na dawa za kupunguza ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga.

Arthritisi ya rheumatoidi kawaida huendelea kuwa mbaya zaidi baada ya muda, na huweza kusababisha uharibifu mkubwa wa viungo. Matibabu ya mapema huweza kuzuia baadhi ya uharibifu wa viungo.

Vihatarishi

Arthritisi ya rheumatoidi ni ugonjwa wa kinga nafsia. Hii humaanisha mfumo wa kinga hushambulia tishu zenye afya mwilini kimakosa. Sababu ya ugonjwa huu kutokea haueleweki vizuri. Unaweza kusababisha uharibifu wa gegedu na mifupa kwenye viungo. Matokeo yake, viungo huweza kulemaa na kushindwa kusogea kama kawaida.

Vitu vingi huweza kuchangia arthritisi ya rheumatoidi. Wanawake huathirika zaidi kuliko wanaume, na ugonjwa huu hutambuliwa kwa watu wengi wenye umri kati ya miaka 35 na 50.

Dalili

Dalili za kawaida ni pamoja na:

  • Maumivu
  • Kuvimba na ugumu wa viungo vingi

Viungo kwenye mikono na miguu huathirika zaidi, lakini ugonjwa huu unaweza kuathiri kiungo chochote. Ugumu wa viungo huwa ni mbaya zaidi mida ya asubuhi, na hupungua kadri siku inavyoendelea.

Dalili nyingine hujumuisha:

  • Uchovu
  • Kupungua uzito
  • Homa

Dalili za ugonjwa huu hutokea polepole na huwa mbaya zaidi baada ya muda. Ugonjwa huu unaweza kuathiri sehemu nyingine za mwili, kama vile ngozi, mapafu na moyo.

Utambuzi

Utambuzi hufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa kimwili. Kipimo cha damu huweza kuonyesha uwepo wa "autoantibodies", ambazo ni protini zinazoshambulia tishu zenye afya mwilini. Pia inaweza kuonyesha dalili za kawaida za inflamesheni. X-ray au CT scan ya viungo huweza kukadiria uharibifu wa viungo.

Matibabu

Matibabu hulenga kupunguza ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga. Dawa zinazojulikana kitaalamu kama 'disease-modifying-antirheumatic drugs’ (DMARDs), huweza kutumika katika matibabu. Hizi hulenga kupungza dalili na kuzuia uharibifu wa viungo. Pia zinaweza kuuzia mfumo wa kinga kushambulia sehemu nyingine za mwili, kama vile ngozi na moyo. Dawa za maumivu na dawa dhidi ya inflamesheni pia huweza kusaidia.

Mchanganyiko wa tiba pia huweza kutumika. Kahakikisha unajishukulisha kimwili huweza kusaidia viungo kufanya kazi kama kawaida. Ikiwa kuna uharibifu mkubwa wa viungo, upasuaji ili kuweka viungo bandia huweza kuhitajika.

Ubashiri

Watu wengi wenye ugonjwa huu huweza kudhiti dalili zao vizuri. Hii kwa kawaida hufanywa kwa kutumia dawa dhidi ya inflamesheni. Matibabu pia ni muhimu katika kuzuia uharibifu wa viungo. Bila matibabu, hatari ya kupata madhara zaidi ni kubwa. Madhara haya hujumuisha uharibifu wa viungo, baadhi ya saratani na magonjwa ya moyo au mapafu.


Washirikishe wengine kwenye makala hii: