1. Ada
  2. Editorial
  3. Tiba & afya
  4. Kampuni ya Ada yarudisha huduma ya afya ya kidijitali kwa lugha ya Kiromania na Kiswahili

Kampuni ya Ada yarudisha huduma ya afya ya kidijitali kwa lugha ya Kiromania na Kiswahili

Ada language update

Leo, tunarejesha huduma kwa lugha ya Kiromania na Kiswahili katika app ya Ada.

Mapema mwaka huu, kampuni ya Ada iliondoa Kiromania na Kiswahili kwenye app yake na kuziondoa kwenye orodha ya maduka ya app nchini Romania. Hata hivyo, maoni ya watumiaji wa app husika yaliweka wazi kwamba: lugha hizi ni muhimu.

Watumiaji wa app kutoka Romania na Tanzania walituambia jinsi wanavyothamini kupata taarifa za afya katika lugha zao za asili. Maoni hayo yalitufanya kubadili uamuzi wetu. Kuanzia leo, app ya Ada inapatikana kwa mara nyingine tena katika lugha saba: Kiingereza, Kijerumani, Kihispania, Kifaransa, Kireno, Kiromania na Kiswahili.

Tunaamini kwamba kupata taarifa za afya zakuaminika huwa na thamani zaidi pale zinapopatikana katika lugha unayoielewa ipasavyo. Kanuni hii imekuwa siku zote msingi wa uboreshaji wa app ya Ada, na inaendelea kuwa sehemu muhimu ya jinsi tunavyowahudumia watu ulimwenguni.

Ikiwa hapo awali ulitumia app ya Ada kwa Kiromania au Kiswahili, app iko tayari kwa ajili yako tena. Pakua au fungua tena app ya Ada kwenye App Store au Google Play, chagua lugha unayopendelea, na endelea ulipoishia. Historia yako ya tathmini ya dalili pia imerudi na sasa unaweza kufungua tathmini zako za awali za afya moja kwa moja ndani ya app.

App ya Ada bado haipatikani kwenye maduka ya app nchini Romania. Hata hivyo, itapatikana nchini humo hivi karibuni.

Kwa maelezo zaidi, unaweza kutembelea fomu yetu ya mawasiliano au kuwasiliana nasi kwa [email protected].

Mwandishi:

Ada

Your health companion