1. Ada
  2. Help
  3. Signing Up & Getting Started

Je, ninawezaje kuhariri au kuongeza taarifa za afya kwenye profaili yangu ya afya katika app ya Ada?

Profaili yako ya Afya hurekodi taarifa fulani kwa kila profaili ndani ya akaunti. Taarifa za afya ni pamoja na: 

  • Taarifa za msingi: Jina, Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa
  • Taarifa za kibinafsi: Urefu, Uzito
  • Historia ya afya binafsi: Hali ya uvutaji sigara, Shinikizo la damu, Kisukari
  • Taarifa kuhusu dawa zinazotumika sasa pamoja na mizio

Kila aina ya taarifa ya afya hubainisha ikiwa inatumika au haitumiki kwa ajili ya kukamilisha tathmini zako.

Unaweza kuhariri  profaili yako kuu ya afya, lakini huwezi kuifuta. Una uhuru wa kuhariri au kufuta profaili wakilishi za afya (secondary health profiles). 

Unaweza kufanya yafuatayo, Ili kutumia na kuhariri profaili ya afya: 

  1. Fungua app ya Ada. 
  2. Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia njia iliyotumika kuingia wakati wa kuunda/kufungua akaunti. 
  3. Chagua Profaili kwenye mwambaa wa menye chini ya skrini yako.
  4. Chagua profaili unayotaka kuhariri.
  5. Chagua aina ya taarifa unayotaka kuhariri.
  6. Andika taarifa mpya. 
  7. Chagua Hifadhi.

Have more questions? Submit a request