Toleo la Muhtasari wa Sera ya Faragha

Tarehe: 15. Mei 2018

Uchakataji wa taarifa nyeti na binafsi za afya, kama vile dalili zako na historia ya hali yako ya kiafya ni muhimu sana katika kukusaidia kusimamia na kuelewa afya yako kupitia app. Kukubaliana kwako na hii Sera mpya ya Faragha kunatoa ruksa ya uchakataji wa taarifa zako.

Tafadhali, kuwa na hakika kwamba hatutogawa taarifa zako kwa mtu yeyote bila idhini yako.

Huko mbeleni utakuwa pia na chaguo la kama uonyeshwe baada ya tathmini machaguo ya matibabu yanayokufaa kulingana na ugonjwa wako. Pia, utaweza kutoa ruksa kama tunaweza kuwasiliana na wewe kwa barua pepe kuhusu fursa za kushiriki kwenye tafiti za tiba ambazo zitakuvutia.

Kwa maelezo zaidi juu ya namna tatakavyotumia na kuchakata taarifa zako binafsi, tafadhali soma Sera ya Faragha.