Zingatia kazi yenye afya zaidi

Katika Ada, kazi yako inaweza kusaidia mamilioni ya watu, ikiwemo na wewe mwenyewe. Tafiti zinaonyesha kwamba kusudi la juu katika maisha linahusiana na maisha marefu zaidi, na yenye afya zaidi.1

Timu yetu kupitia darubini

Dhamira moja

Kila mtu anastahili kupata huduma bora za afya. Katika Ada, kila mshiriki wa timu huchangia kipaji chake cha kipekee kwenye utendaji wetu wa kazi ili kufanikisha dhamira yetu ya kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya duniani kote. Tunapenda sana kile tunachofanya, na hilo linaonekana.

Mitazamo mbalimbali

Kama timu, tunawakilisha mataifa 54 na uzoefu wa mifumo mbalimbali ya afya duniani kote. Utofauti wetu unatuwezesha kuunda masuluhisho ambayo yanakidhi mahitaji ya watu na mashirika ya afya ulimwenguni.

Kwa matokeo bora

Mwaka 2011, baadhi ya watu wenye fikra erevu kabisa katika tiba na uhandisi wa kompyuta waliunda jukwaa la kwanza la afya la AI duniani. Tunaendelea kuongeza kiwango cha ubora, kwa mbinu inayotegemea ushahidi wa kitafiti na inayotoa kipaumbele kwenye ubora wa kitiba na uzoefu wa mtumiaji wa bidhaa.

Maadili yetu

  • Uadilifu

    Uadilifu
    Kufanya jambo lililo sahihi

  • Ubora

    Ubora

    Kuongeza kiwango cha ubora


  • Unyenyekevu

    Unyenyekevu
    Kutafuta kujifunza

  • Kusudi

    Kusudi
    Kuboresha maisha ya watu

  • Ushirikiano

    Ushirikiano
    Kufanikiwa kama timu

  • Uvumbuzi

    Uvumbuzi
    Kujenga muskakabali

Kuboresha afya kunaanzia ndani

Tunatoa kifurushi cha faida kilichoandaliwa kwa kuzingatia afya yako ya akili na mwili.

Fanya kazi mahali popote

Fanya kazi popote unapojihisi raha zaidi - nyumbani, ofisini, au mchanganyiko kidogo wa sehemu zote mbili. Utapata msaada wa kifedha ili kukuwezesha kutayarisha mahali pa ofisi yako ya nyumbani. Utafiti unaonyesha kwamba kuna uhusiano kati ya mazingira mazuri ya kazi na afya bora.2 3 

Ahmet Kivrak

Ahmet Kivrak
Mkuu wa Upatikanaji wa Vipaji & Uchanganuzi wa Watu

Vanessa Lemarié

Vanessa Lemarié
Afisa Mkuu wa Mahusiano na Washirika

Rungwe Hashim

Rungwe Hashim
Mwandishi na Meneja wa maudhui (Kiswahili)

Ifahamu timu

Kila mtu yuko hapa kwasababu anataka kushiriki kujenga mustakabali wa huduma za afya.

Jifunze zaidi kuhusu maisha na watu wanaofanya kazi Ada

Unataka #ujiungenaAda?

Idara zote
Maeneo yote

Hizi ndiyo hatua utakazopitia ili kujiunga nasi

Tuma maombi ya fursa ya kazi inayokufaa katika Ada.

Fahamiana na mshirika wetu wa upatikanaji wa watu wenye vipaji.

Ongea na meneja ajira. Katika hatua hii, unaweza kuhitajika kufanya jaribio dogo la ujuzi wa kazi husika.

Fahamiana na timu na wadau wengine.

Pokea ofa yako ya kazi.

Pokea kisanduku chako cha ukaribisho na anza safari yako ya Ada.

Ifahamu Timu yetu ya Upatikanaji wa Vipaji

Ahmet Kivrak
Ahmet Kivrak
Mkuu wa Upatikanaji wa Vipaji
Sara Korycki
Sara Korycki
Mshirika Mwandamizi wa Upatikanaji wa Vipaji
Martin Forry
Martin Forry
Mshirika Mwandamizi wa Upatikanaji wa Vipaji

  1. JAMA network (2019). Association Between Life Purpose and Mortality Among US Adults Older Than 50 Years. Access on 30 August 2022.

  2. Oxford Academic, (2010). Effects of the physical work environment on physiological measures of stress. Access on 30 August 2022.

  3. BMC Public Health (2020), A rapid review of mental and physical health effects of working at home: how do we optimise health? Access on 30 August 2022.

  4. Nature (2017). Work–life balance: Break or burn out. Access on 30 August 2022.

  5. NIH (2018). Good jobs, good pay, better health? The effects of job quality on health among older European workers. Access on 30 August 2022.

  6. CMAJj (2006). Health benefits of physical activity: the evidence. Access on 30 August 2022.

  7. Future Medicine (2010). Promotion of cognitive health through cognitive activity in the aging population. Access on 30 August 2022.

  8. Sage journal (2010). Social Relationships and Health: A Flashpoint for Health Policy. Access on 30 August 2022.