1. Ada
  2. Magonjwa
  3. Mafua ya kawaida

Mafua ya kawaida

Imeandikwa na Timu ya Ada ya Maarifa ya Kitiba

Imesasishwa tarehe

Mafua ni nini?

Mafua ni maambukizi ya virusi kwenye pua na koo. Kwa kawaida husababisha dalili kama vile kutokwa kamasi na kikohozi. Virusi vinavyosababisha hali hii husambazwa kwa matone madogo kwenye hewa baada ya kukohoa au kupiga chafya.

Kuchukua hatua ili kuepuka kusambaza maambukizi huweza kusaidia kupunguza usambazaji wa virusi hivi. Kwa mfano, mtu anapaswa kufunika pua na mdomo anapo kuhoa na kupiga chafya. Watu wenye mafua kwa kawaida hupata nafuu ndani ya wiki.

Dalili hizi hufanana na dalili za ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Hivyo basi, inashauriwa kujitenga, na kukaa nyumbani kulingana na ushauri katika eneo unaloishi. Ni muhimu kuepuka sehemu za kazi, shule au sehemu nyingine za kijamii.

Watu wanapaswa kuosha mikono kwa kutumia maji na sabuni mara kwa mara na kuepuka kugusa uso. Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi. Ikiwa mtu anahisi kuishiwa pumzi, anapaswa kufuata mwongozo wa kupata huduma ya haraka katika eneo analoishi.

Mwongozo na hatua za kufuata huweza kutofautiana kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona. Kwa taarifa zaidi, tafadhali angalia Maktaba ya Hali ya Ada.

Dalili za mafua

Dalili za mafua kwa kawaida hujumuisha:

  • Kutokwa makamasi na pua kuziba
  • Kikohozi kikavu, na
  • Maumivu ya koo.

Vihatarishi vya mafua

Mafua husababishwa na virusi ambavyo huambukiza pua na koo. Virusi hivi huenea kupitia matone katika hewa wakati mtu aliyeathirika anapokohoa au kupiga chafya. Ni hali ya kawaida ambayo inaweza kuathiri watu wa umri wowote. Watu wengi hupata mafua mara moja kwa mwaka, na watoto wanaweza kupata mafua kama mara 5 au mara 6 kwa mwaka.

Utambuzi

Utambuzi kwa kawaida hufanywa kulingana na dalili.

Matibabu / dawa ya mafua

Kwa kawaida mafua hayahitaji matibabu. Hata hivyo, baadhi ya watu huchukua hatua za kupunguza dalili zao. Hizi huweza kujumuisha kunywa vinywaji vya moto au kutumia peremende zenye dawa (lozenges) ili kupooza koo. Baadhi ya watu huona kuwa dawa za kupulizia puani husaidia kuzibua pua. Mvuke unaotoka wakati wa kuoga na maji ya moto pia huweza kusaidia kufungua pua na koo.

Kinga ya mafua

Kudumisha usafi mzuri husaidia kupunguza usambazaji wa virusi na kuepuka kupata mafua. Ni muhimu kuosha mikono mara kwa mara na kufunika mdomo na pua wakati wa kupiga chafya au kukohoa.

Ubashiri

Kwa kawaida mafua huisha kabisa ndani ya wiki hata bila matibabu maalum.


Washirikishe wengine kwenye makala hii: