Je app ya Ada inaweza kufanya utambuzi wa ugonjwa (diagnosis), ushauri wa kitiba, au kupendekeza machaguo ya matibabu?
Kwa kuandika dalili zako kwenye app ya Ada, unaweza kubaini kinachoweza kuwa kinasababisha ujihisi mgonjwa na ni machaguo gani ya matibabu unaweza kuyapata. Hata hivyo, haimaanishi kwamba app ya Ada imekwisha tambua rasmi ugonjwa unaokusumbua na timu yetu ya huduma kwa watumiaji wa app haijafunzwa au kuthibitishwa kutoa ushauri wa kitiba. Daima unapaswa kuwasiliana na wataalamu wa afya kwa ajili ya utambuzi rasmi wa ugonjwa, matibabu, au ushauri wa kitiba.
Angalizo: Katika baadhi ya nchi, tunashirikiana na mashirika ya afya ili kuunganisha wagonjwa wao na huduma za afya zinazofaa. Ikiwa uliunganishwa kwenye app ya Ada kupitia moja ya huduma hizi, tafadhali tufahamishe ni huduma gani uliyotumia.
Have more questions? Submit a request