Mchakato wetu wa uundaji wa maudhui ya kitiba
Tunaamini upatikanaji wa taarifa za kuaminika na rafiki kwa mgonjwa unaweza kusaidia kufanya usimamizi wa afya kuwa jambo wezeshi na chanya. Timu yetu ya maarifa ya kitiba inaunda maudhui asilia ambayo yamehakikiwa na wataalamu wa tiba, yanasasishwa mara kwa mara, na rahisi kuyaelewa.
Wakati taarifa za afya sasa zinapatikana kwa urahisi zaidi kuliko hapo awali, inaweza kuwa ngumu kupata chanzo cha kutegemewa zaidi, chenye kuhusu, na cha kuaminika. Tumeufanya huu mchakato kuwa rahisi kwako kadiri iwezekanavyo. Tunataka ujiamini na kujihisi salama ukijua kwamba taarifa za afya tunazochapisha ni sahihi. Kwahiyo, utawezaje kujua kama unachosoma ni cha kuaminika? Katika Ada, tunaamini imani inapatikana kupitia ukweli na uwazi, hivyo basi tunashirikisha namna tunavyoendelea kuunda maudhui ya tiba kwenye tovuti yetu.
Nani anaunda maudhui yetu ya kitiba?
Waundaji wetu wa maudhui ya kitiba ni madaktari, madaktari bingwa, na wastadi wa tiba. Kila sehemu ya maudhui ya kitiba yamepitiwa na angalau wataalamu watatu wa tiba waliopo ndani ya Ada.
Mchakato wetu wa uundaji wa maudhui ya kitiba upo vipi?
Kila muundaji wa maudhui ya tiba anatakiwa kumaliza kwa utimilifu mchakato wa uundaji maudhui, hakiki taarifa, mapitio ya wenzi, na uhariri - ili kukupatia taarifa za kuaminika zaidi. Maudhui ya tiba ya Ada yanasasishwa mara kwa mara na kufanywa yaendane zaidi na taarifa za sasa. Tumetoa vyanzo vyetu vya taarifa hapo chini.
Acha tukuonyeshe mchakato wetu wa kuunda maudhui ya kitiba yanayochapishwa kwenye tovuti yetu:
Tunatumia tafiti za kisasa, miongozo ya mashirika makubwa ya afya, na takwimu za magonjwa ya mlipuko.
Tunaandika kwa lugha nyepesi ambayo ni rahisi kwa mgonjwa kuielewa, na wakati huo huo tunadumisha usahihi wa kitiba.
Tunakagua usahihi wa taarifa kupitia wataalamu wenza wa tiba waliofuzu.
Tunafanya uhakiki wa mwisho kwa ajili ya ubora wa maudhui na uaminifu wa kitiba.
Zaidi, timu yetu ya maarifa ya kitiba inakagua mara kwa mara vyanzo vya taarifa za kitiba vinavyotambulika rasmi na machapisho mapya ili kuhakikisha maudhui yetu yote yanaendeana na wakati. Bodi yetu ya kitiba, inayojumuisha madaktari wazoefu na wastadi wa kanuni zinasosimamia masuala ya tiba, wanahakiki na kusaidia uundaji wa maudhui ya tiba kama bodi ya usimamizi ndani ya Ada.
Nini kinachofanya sisi kuwa tofauti?
Hakuna matangazo - Hatuchapishi kwenye tovuti yetu maudhui yaliyofadhiliwa.
Maudhui yetu ni halisi, yaliyoandaliwa kutoka ndani - sio kwa ushirika kutoka vyanzo vingine.
Maudhui yameunganishwa kwenye mfumo wetu mzima wa Ada, ili kusaidia watu kutathmini afya zao baada ya kusoma.
Tunaunda maudhui ambayo tunajua watu wanataka kujifunza, kwa kuzingatia ufahamu wetu wa masuala ya afya ulimwenguni.
Tunatumia vyanzo gani?
Mchakato wetu wa uundaji wa maudhui ya kitiba unategemea vyanzo vilivyochaguliwa kwa umakini na vya kuaminika, na machapisho yaliyopitiwa na wataalamu wengine kwa ajili ya kutoa data za magonjwa ya mlipuko, simptomatolojia, na miongozo ya usimamizi.
Ada inapaswa kutumiwaje?
Ada imeundwa kurahisisha majadiliano baina ya mtumiaji na mtaalamu wa tiba mwenye sifa. Pia, Ada imeundwa kutoa taarifa za afya. Ni muhimu kukumbuka kwamba hatufanyi tambuzi za magonjwa. Ikiwa una mashaka kuhusu afya yako au una maswali yeyote kuhusu masuala ya kiafya, tafadhali tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa tiba. Wakati wa dharura, wasiliana na huduma za dharura mara moja. Kamwe haupaswi kupuuza ushauri wa kitaalamu wa daktari au kufuta miadi na daktari kwasababu unategemea taarifa zilizotolewa na Ada.
Sera yetu ya matangazo inasemaje?
Hatupokei fedha kupitia matangazo ya kwenye tovuti au maudhui yaliyofadhiliwa. Tunajivunia kushirikiana na mifumo mikubwa ya afya na mashirika ya kimataifa yasiyotafuta faida (non-profit organizations).
Tupo na tutabaki kuwa huru kabisa na wepesi kubadilika katika sera yetu ya tahariri. Washirika wetu hawashawishi maudhui tunayochapisha.
Kwanini maoni yako yana manufaa?
Kutoa taarifa bora na sahihi za afya ni muhimu kwetu. Ikiwa unaona tatizo lolote katika maudhui yetu, tafadhali tufahamishe ili tuweze kuchukua hatua. Tutayapitia maoni yako, fanya maboresho yeyote ya lazima, na kuchapisha tena maudhui yaliyorekebishwa kuakisi sasisho za hivi karibuni na kuhakikisha usomaji wako wa taarifa zetu za kiafya unakuacha na hisia chanya na kukuongezea uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu afya yako.