Kazi yetu katika magonjwa adimu

Kwa bahati mbaya, magonjwa adimu si rahisi kuyatambua na yanaathiri sana jamii zetu. Mtu wa kawaida anayeishi na ugonjwa adimu anahimili safari ndefu ya miaka mitano ya utambuzi. Hiyo mara nyingi inamaanisha ziara za huduma zisizo za lazima, matibabu yaliyocheleweshwa, na matokeo hafifu. 

Watu wengi wanaoishi na ugonjwa adimu hawatopata kamwe utambuzi sahihi maishani mwao.

Tunafanya kazi ili kufupisha muda wa utambuzi na kuboresha matokeo kwa watu wanaoishi na magonjwa adimu.

Changamoto ya utambuzi wa ugonjwa adimu

Kuna zaidi ya magonjwa adimu 7,000 yanayojulikana. Mengi yana chanzo cha kinasaba na mengi dalili zake zinafanana zaidi na magonjwa ya kawaida. Hii inafanya iwe vigumu sana kwa binadamu yeyote kugundua magonjwa yote adimu bila msaada.

Rufaa ya mtaalamu mara nyingi hucheleweshwa kwasababu madaktari (GPs) hawashuku ugonjwa adimu. Katika sehemu nyingi duniani, ukosefu wa upatikanaji wa huduma unamaanisha kuna uwezekano wa watu kushindwa kamwe kupata utambuzi wa ugonjwa adimu wanaouhitaji sana kwa huduma za afya toshelevu.

Adimu lakini yameenea: Ugonjwa wowote ambao unaathiri chini ya watano katika watu 10,000 unachukuliwa kuwa adimu katika Ulaya. Lakini ukiwa na watu milioni 300 duniani kote wanaoishi na ugonjwa adimu, adimu imeenea.

Kumsaidia adimu inaanza na kumpata adimu

Katika Ada, tuna maono ya dunia ambayo kila mtu mwenye ugonjwa adimu anapata huduma ya afya anayoihitaji katika muda unaofaa. 

AI yetu na msimamo wetu katika kuunda mifano (modeling) ya magonjwa adimu inaweza kubadilisha vifaa vya kila siku majumbani na mahospitalini duniani kote kuwa vyombo vyenye nguvu katika kuboresha utambuzi wa ugonjwa, muda wa kufanya utambuzi, na upatikanaji wa huduma.

“Kwa kutumia AI kuongeza shaka ya ugonjwa adimu mapema, tunaweza kuharakisha rufaa kwenye kliniki za wataalamu kwa utambuzi. Hiyo inaweza maanisha hatua za ugonjwa adimu zilizorahisishwa na kupunguza kuelemewa kwa watu wanaoishi na ugonjwa adimu, madaktari, na mifumo ya afya.”

Vanessa Lemarié
Vanessa Lemarié
Afisa Mkuu wa Mahusiano na Washirika

Pamoja, tunaweza:

    • Elimisha watu kwa taarifa sahihi kuhusu magonjwa yanayowezekana.
    • Toa upatikanaji wa haraka wa mwongozo wa jumla, rasilimali, na huduma.
    • Unganisha na elimisha washikadau ili kujenga utetezi.

Tumeunda mamia ya mifano ya magonjwa adimu, kuanzia ugonjwa wa amiloidi kwenye neva mpaka ugonjwa wa Zollinger-Ellison.

Tunafanya kazi katika magonjwa adimu na

Pfizer
Takeda