Mpango wetu wa Afya Duniani
Nusu ya dunia haina huduma muhimu za afya. Idadi ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati (LMICs) wanakabiliwa na viwango vinavyoongezeka vya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na kuongeza gharama za huduma ya afya.
Tunafanya kazi kuongeza kasi ya bima ya afya kwa wote ili kuboresha utoaji wa huduma ya afya kwa wale wanaoihitaji zaidi.
Ukubwa wa changamoto ya afya duniani
Kukabiliana kwa pamoja na ukosefu wa usawa wa huduma za afya
Tunashirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), serikali, mashirika ya afya duniani, na biashara zingine ili kuimarisha ubora wa tiba, kuongeza upatikanaji wa huduma ya afya, na kuboresha ufanisi wa huduma kwa watu wenye uhaba nazo na walio katika mazingira hatarishi.
Pamoja tunaweza
Tunafanya kazi kuelekea usawa wa afya duniani na
Tunafanya kazi na Fondation Botnar ili kuifanya Ada kuendeana na mazingira ya Tanzania na Romania. Kwa kuifanya Ada ipatikane kwa Kiswahili na Kiromania, tunawezesha watu milioni 119 kufikia mwongozo wa tiba wa kibinafsi wa kuaminika ili kusimamia afya zao. Taarifa kwa waandishi wa habari.
Tulifanya kazi na Bill na Melinda Gates Foundation ili kuchunguza jinsi tunaweza kupatanisha vipimo vya utambuzi wa njia ya huduma ya tiba na AI yetu inayoendeshwa kitiba ili kusaidia wahudumu wa afya katika nchi za kipato cha chini na cha kati (LMICs).
Tunawekeza kwenye Akili Bandia (AI) kama suluhisho la upungufu wa idadi ya wahudumu wa afya duniani na hitaji la haraka la kuboresha afya ya mtoto na kijana. Ushirikiano wetu unakabiliana na hitaji hili ndani ya Afrika ya Mashariki na Rumania, kwa kuleta athari chanya kwa vijana na pia ufahamu kwa Fondation Botnar na Ada ili kutanua hii mbinu ya kibunifu kwenye nchi nyingine za kipato cha chini na cha kati.
Remais, J., et al. “Convergence of non-communicable and infectious diseases in low- and middle-income countries.” 13 October 2012. Accessed 13 September 2020.
WHO. “Public Spending on Health: A Closer Look at Global Trends.” 2018. Accessed 13 September 2020.
WHO. “Health financing: Key policy messages.” Accessed 13 September 2020.
WHO. “Global health workforce shortage to reach 12.9 million in coming decades.” 11 November 2013. Accessed 13 September 2020.