Ubora wa kitiba
Tafiti za kitiba zinaonyesha ubora wa kitiba unatofautiana kati ya machaguo ya mshirika wako wa teknolojia ya afya. Hivi ndivyo njia yenye ushahidi inaweza kukusaidia kufanya chaguo sahihi.
Mambo ya kuzingatia
Nguzo zetu 5 za ubora wa kitiba ni msingi wa masuluhisho yetu ya biashara ya afya.
Kwanini ubora wa kitiba ni muhimu
Utawala wa kitiba na udhibiti wa tasnia huleta michakato huru ya kudhibiti ubora unayoweza kuiamini.
Uzoefu mzuri wa mtumiaji inamaanisha watu hutoa maoni sahihi ili kupata mwongozo sahihi kutoka kwenye teknolojia.
Uwepo wa taarifa pana za magonjwa inamaanisha magonjwa hatari na yasiyo ya kawaida (adimu) hayakosi kutambuliwa au kutambuliwa kimakosa.
Usahihi wa kitiba unaweza kusaidia kupunguza muda wa kugundua ugonjwa ili kuharakisha matibabu.
Usalama wa ushauri unaweza kusaidia kuhakikisha wataalamu wa huduma za afya wanawaona wagonjwa wanaohitaji huduma zao zaidi katika mpangilio sahihi.
Jinsi AI ya Ada inavyofanya kazi
Awali iliundwa kusaidia ufanyaji wa maamuzi ya kitiba, madaktari wetu waliunda Ada ili ifikiri kama daktari. Usahihi wa kitiba na usimamizi wa kitiba kutoka kwa madaktari wa kibinadamu umekuwa kwenye DNA yetu tangu mwanzo kabisa. Wafahamu baadhi ya wataalamu wetu wa tiba.
Endelea kusoma
Miller, S., Gilbert, et al. JMIR (2020), doi: 10.2196/19713.
Scheder-Bieschin, J., et al. (2020), doi: 10.1101/2020.11.13.20230953.
Gilbert, S. et al. BMJ Open, (2020). doi: 10.1136/bmjopen-2020-040269.
Ronicke, S. et al. Orphanet. (2019). doi: 10.1186/s13023-019-1040-6.
Morse, K. et al. J Med Internet Res, (2020). doi: 10.2196/20549.