Machapisho na utafiti
Utafiti shirikishi
- Je, app za tathmini ya dalili za kidijitali zina usahihi gani katika kupendekeza magonjwa na kutoa ushauri wa dharura?: Tafiti za kitiba za kulinganisha na madaktari.
- Manufaa ya vikagua dalili hutegemea usalama, ujumuishaji wa wagonjwa, na usahihi.
- Ushauri wa Ada ulikuwa salama katika 97% ya kesi, ikiwa na 99% ya ujumuishaji wa magonjwa na usahihi wa 70% kwa 3 bora ya mapendekezo yanayofaa ikilinganishwa na wastani wa 38% za mshindani wa karibu.
BMJ Open 2020 - Matumizi ya wagonjwa na mtazamo wa teknolojia ya tathmini ya dalili na ushauri inayotokana na akili bandia katika chumba cha kusubiria huduma ya msingi nchini Uingereza: Utafiti wa majaribio ya uchunguzi.
- 97.8% ya washiriki waliikadiria Ada kuwa rahisi au rahisi sana kutumia, na 12.8% ya washiriki wangechelewesha miadi yao au wangetumia huduma ya afya ya kiwango cha chini zaidi.
JMIR Hum Factors 2020 - Ufahamu wa ufuatiliaji wa ugonjwa kutoka kwenye app ya tathmini ya dalili kabla na wakati wa ukabilianaji wa COVID-19 nchini Ujerumani na Uingereza: Matokeo kutoka kwa urudiaji wa changanuzi wakilishi.
- Mapitio ya data kutoka kwa watumiaji 950,000 yalibainisha kuwa Ada inaweza kusaidia kuwezesha uelewa wa athari za sera za afya ya jamii kama zuio la watu kutembea wakati wa kukabiliana na COVID-19.
JMIR mHealth uHealth 2020 - Je, mfumo wa kusaidia ufanyaji maamuzi unaweza kuharakisha utambuzi wa ugonjwa adimu? Kutathmini uwezekano wa athari ya utambuzi wa magonjwa (DX) wa Ada katika utafiti wa kutazama matukio ya nyuma.
- 89.25% ya mapendekezo ya juu ya Ada yalilingana na utambuzi uliothibitishwa, na 33% ya wagonjwa wangeweza kutambuliwa kuwa na ugonjwa adimu katika ziara ya kwanza ya kitiba iliyoandikishwa na Ada.
Orphanet J Rare Dis 2019 - Kuboresha mazungumzo ya mgonjwa na daktari wa kitengo cha dharura kupitia kifaa cha kurekodi dalili kinachowezeshwa na akili bandia: Utafiti wa majaribio wa muundo wa mwelekeo wa hatua.
- Ada iliwezesha mazungumzo na kuboresha maelewano kwa 90% ya wagonjwa, 73% ya madaktari, na 100% ya wauguzi.
Unasubiri kuchapishwa - Uwezekano wa kurekodi dalili za mgonjwa wa kidijitali kupitia programu za tathmini ya dalili ili kuboresha utoaji huduma kwa mgonjwa na kupunguza wakati wa kusubiri katika Vituo vya Huduma ya Dharura: Utafiti wa hali bandia.
- Ada inaweza kupunguza wastani wa muda wa mgonjwa kusubiri kumuona muuguzi wa kutathmini dharura ya tiba (triage) kwa 54%.
JMIR Form Res 2021 - Utafiti tarajiwa wa uwezekano wa Mfumo mpya wa Usaidizi wa Uamuzi wa Utambuzi (DDSS) kwa ajili ya wataalamu wa kitiba.
- Sampuli kifani ya DDSS ya Ada inaweza kusaidia madaktari katika ufanyaji maamuzi kwa kuwaonyesha njia mpya na tambuzi zinazowezekana.
- Ada ilitoa msaada sahihi wa uamuzi katika mazingira ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa tatizo la upumuaji (dyspnea).
Unasubiri kuchapishwa - Mbinu mpya katika ufuatiliaji wa ugonjwa kama wa homa ya mafua (ILI): uchunguzi wa data kutoka kwa app ya tathmini ya dalili Ada, Uchunguzi wa kesi ya utafiti nchini Ujerumani.
- Ada iligundua mienendo sawa na wa ILI kwenye mfumo rasmi wa Kijerumani wa ufuatliaji na ingeweza kusaidia kutambua mielekeo ya afya katika nchi ambazo hazina mifumo ya ufuatiliaji wa idadi ya watu.
JMIR Public Health Surveillance 2021 - Ubora wa mapendekezo ya ugonjwa na ushauri wa dharura uliotolewa na app ya Ada ya tathmini ya dalili vilitathminiwa kwa kesi zilizozalishwa kwa uhuru na zilizoboreshwa kwa ajili ya Australia.
- Pendekezo la juu la Ada lilikuwa sahihi katika 65% ya kesi, na ugonjwa sahihi ulikuwa katika mapendekezo 3 ya juu katika 83% ya kesi.
- 63% ya ushauri wa dharura wa Ada ulilingana na kiwango cha kipimo cha ubora.
CSIRO Publishing - Je, magonjwa adimu ni adimu kivipi kwa Ada, kikagua dalili cha kitiba?
- Ada ilipendekeza magonjwa adimu kwa 4% ya tathmini milioni 15, kulingana na viwango vya idadi ya watu.
Iliyowasilishwa katika Mkutano wa RE(ACT) Congress - IRDiRC Conference, Berlin, 2020 - Uwezo wa Uchunguzi wa Dalili kwa njia ya Kidijitali ili Kupunguza maambukizi ya SARS-CoV-2: Utafiti wa Uigaji
- Vifaa vya uchunguzi wa dalili kwa njia ya kidijitali vinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya COVID-19.
- Programu kama Ada (pamoja na ufanyaji vipimo na watu kujitenga) zinaweza kuzuia 8% zaidi ya idadi ya watu wanaoambukizwa.
Unasubiri kuchapishwa
Utafiti huru
- Kutumia Sifa Bainifu na Upaumbele wa Dharura wa Kikagua Dalili cha Kidijitali katika Mfumo Mkubwa wa Afya Uliounganishwa: Utafiti Huru Unaohusu Watu
- 46.4% ya tathmini ya dalili 26,646 za Ada zilikamilishwa nje ya muda wa masaa ya kazi ya ofisi ya daktari.
- Mapendekezo ya Ada yalikuwa sawa na ya wauguzi wa vipaumbele vya tiba.
J Med Internet Res 2020 - Usahihi wa vikaguzi vya dalili vya mtandaoni na uwezekano wa athari kwenye matumizi ya huduma.
- Ada ilikuwa na usahihi wa 73% ikilinganishwa na 38% ya wastani wa app zote na mpangilio wa usalama kwa 97% ikilinganishwa na wastani wa 83% wa app zote.
PLOS ONE - Usahihi wa Chatiroboti (Ada) katika utambuzi wa magonjwa ya akili: Utafiti wa kulinganisha kesi kwa kutumia watumiaji wa kawaida na wataalamu.
- Ada inaweza kusaidia kutambua matatizo ya afya ya akili kwa watu wazima.
JMIR Form Res 2019 - Kutoka kwenye dalili hadi kutathmini upya vikagua-dalili: Je, vikagua dalili hatimaye vinatosha na sahihi kutumia? Sasisho kutokana na mtazamo wa ENT.
- Ada ilikuwa app ya pili bora zaidi kiutendaji kati ya app 24 zilizojaribiwa katika utaratibu wa ENT.
HNO 2019 - Nini kilitokea wakati Pulse ilijaribu app za kukagua dalili.
Ada ilikuwa sahihi kuliko app zote 4 zilizojaribiwa na ilikuwa na kasi na rahisi kutumia.
Pulse Today 2019 - Je, unaweza kweli kuamini app za kitiba kwenye simu yako?
- Ada ilikuwa 'kwa mbali sana app bora zaidi’ iliyojaribiwa, ikiuliza maswali yanayoeleweka na kutoa mapendekezo ya magonjwa ambayo ni bora kuliko app nyingine zote zilizojaribiwa.
Wired UK 2017
Machapisho mengine
- Magonjwa adimu 2030: Jinsi AI iliyoboreshwa itakavyosaidia utambuzi na matibabu ya magonjwa adimu katika siku zijazo.
- Ada inaweza kusaidia kutambua magonjwa ya kinga nafsia ya kurithi kama vile homa ya mediterania ya kurithi.
Ann Rheum Dis 2020