1. Ada
  2. Magonjwa
  3. Ugonjwa wa polio

Ugonjwa wa polio

Imeandikwa na Timu ya Ada ya Maarifa ya Kitiba

Imesasishwa tarehe

Polio ni nini?

Maambukizi ya virusi vya polio ni maambukizi yanayoathiri mfumo wa neva na huweza kusababisha udhaifu wa misuli au kupooza, ambayyo ni kushindwa kusogeza misuli. Inasababishwa na misuli, na pia huitwa polio.

Ugonjwa huu ni adimu, kwa kuwa chanjo imepunguza uwepo wa virusi hivi katika nji nyingi. Polio hutokea zaidi kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Watu ambao bado hawajapata chanjo wapo kwenye hatari ya kuambukizwa.

Wale wanaosafiri au kuishi kwenye maeneo ambayo bado kuna virusi vya polio wapo kwenye hatari zaidi. Virusi vya polio husambazwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Polio inasambazwa kwa kukohoa, kupiga chafya au kugusa kinyesi. Mara chache sana, watu waliopata chanjo huweza kuwapa wale ambao hawajachanjwa virusi vya polio.

Dalili huweza kujumuisha homa, koo kuuma, maumivu ya kichwa na misuli kuuma. Baadhi ya watu hupata udhaifu wa misuli. Maambukizi ya polio hayawezi kutibiwa, na matibabu kawaida hudhibiti dalili tu. Matokeo baada ya maambikizi ya polio hutegemea dalili ni kali kiasi gani. Inaweza kusababisha ulemavu wa kudumu na kifo.

Je, polio huambukizwaje?

Polio husambazwa kwa kugusana na mtu aliyeambukizwa, au kamasi na kinyesi chenye maambukizi. Polio imeondolewa katika nchi nyingi duniani, lakini kesi au milipuko ya ugonjwa huu bado hutokea.

Milipuko ya polio hutokea zaidi katika kipindi cha kiangazi. Watu wenye umri wowote huweza kuathirika. Watoto wenye umri chini ya miaka 5 huathirika zaidi. Watu ambao hawajapata chanjo dhidi ya polio wapo kwenye hatari ya kuambukizwa. Wale wanaotembelea maeneo ambayo bado kuna polio wapo kwenye hatari zaidi.

Dalili za polio ni zipi?

Dalili za awali za maambukizi ya polio hufanana na dalili za mafua na hujumuisha homa, maumivu ya kichwa, kutapika, hisia ya kuumwa na maumivu ya koo. Dalili hizi mara nyingi hupona ndani ya siku chache na watu wengi hawatakuwa na dalili zingine.

Virusi hivi vikisambaa kwenye mfumo wa neva, vinaweza kusababisha udhaifu wa misuli ya miguu, mikono, mgongo na shingo. Hii husababisha matatizo ya kutembea na kufanya shughuli za kawaida, hata kupumua. Baada ya muda, hii husababisha viungo kubana, misuli kunywea au hata kupooza. Dalili huweza kujirudi miaka baada ya maambukizi ya awali.

Utambuzi wa ugonjwa wa polio

Utambuzi hufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa kimwili. Historia ya mtu ya matibabu na kusafiri ni muhimu kujua, kuwa watu ambao hawajapata chanjo na wale wanaosafiri kwenye maeneo yenye polio wana hatari zaidi ya kupata maambukizi.

Vipimo huweza kufanywa ili kuthibitisha utambuzi. Vipimo vya damu huweza kuchunguza uwepo wa kingamwili (antibodies), ambazo ni protini za mfumo wa kinga zinazopambana na virusi vya polio. Kipimo cha uti wa mgongo (lumbar puncture) huweza kufanyika ili kuchunguza kama virusi vipo kwenye mfumo wa neva. Hii inahusisha kuchukua sampuli ya majimaji kutoka kwenye uti wa mgongo.

Matibabu

Hamna tiba maalum ya maambukizi ya virusi vya polio. Matibabu hulenga kupunguza dalili. Dawa za maumivu huweza kutolewa kwa ajili ya maumivu ya kichwa na misuli.

Watu wenye udhaifu wa misuli unaoendelea huweza kuhitaji fiziotherapi (tiba ya mazoezi) ili kusaidia kuboresha nguvu ya misuli. Ikiwa misuli ya kupumua imeathirika na kuwa dhaifu, mashine huweza kuhitajika ili kumsaidia aliyethirika kupumua.

Kinga

Maambukizi ya virusi vya polio huweza kuzuiliwa kwa chanjo. Ni muhimu kufuatilia ratiba ya chanjo iliyopendekezwa.

Utabiri

Matokeo ya hali hii hutegemea kama mfumo wa neva umeathirika. Kwa matukio ambayo mfumo wa neva haujaathirika, kuna uwezekano wa kupona kabisa. Mfumo wa neva ukiathirika unaweza kusababisha ulemavu au kifo kama misuli ya kupumua imeathirika.


Washirikishe wengine kwenye makala hii: